Erick Shigongo ni bora ungekaa kimya tu

Erick Shigongo ni bora ungekaa kimya tu

Desert Voice

Senior Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
159
Reaction score
410
Japokuwa kila mtu anayo haki kikatiba ya kutoa maoni yake, lakini wewe ni bora ungekaa kimya tu.

Tuache sisi tupige kelele kulilia Demokrasia na heshima ya nchi yetu iliyopotea kwa miaka miwili iliyopita.

Leo hii wewe unamwomba Rais Magufuli akutane na viongozi wa dini? wakutane ili iweje?

Umesahau kalamu yako? Unakumbuka ulichokuwa unaandika gazetini kumpigia debe Magufuli?

Unakumbuka jinsi ambavyo ulikuwa unakosa usingizi kwa hofu ya Lowassa akiwa Rais kampuni zako zitafilisika?

"Vipi mume wangu,mbona hadi sasa umeshindwa kulala? "
"Lowassa " .
"Aah, Lowassa hawezi kushinda wewe lala ".

Nimekunukuu andiko lako mwenyewe ktk gazeti la Ijumaa Wikienda.
Watu werevu tulidhani labda ulikuwa na ugomvi binafsi na Lowassa, kumbe una chuki kubwa mno na wapinzani, sikuwahi kutarajia mtu aliyepita mapito magumu kimaisha na mcha Mungu,eti umchukie mtu ambaye hajakukosea lolote.

Wapinzani tunapita ktk kipindi kigumu mno kuwahi kutokea chini ya awamu hii ya tano.

Na hadi sasa hivi viongozi wa dini walipotoa waraka wao kwa serikali kuitaka iheshimu katiba na kurekebisha hali ngumu ya uchumi iliyopo, wamekutana na majibu ya kejeli kuanzia CCM hadi kwa Rais mwenyewe.

Wana ccm wanawaita viongozi wa dini ni vibaraka wa upinzani, na rais kasema kuwa waombe viwanda vya dawa vijengwe na siyo kutoa waraka usio na mantiki.

Sasa wewe unashauri nini wakati ulikuwa hulali Ukitaka Magufuli ashinde?

Humu mitandaoni kuna jeshi kubwa la wana CCM wenzako ambao hawajawahi kuona kasoro zozote za rais Magufuli, kazi yao kubwa ni kusifia tu kila afanyalo rais, kwa nini usiungane nao kusifia, tena una vyombo vya habari.

Sioni sababu kwa nini unalalamika, ni bora ukae kimya kwa sababu utaonekana mnafiki sana.

Unakumbuka pia uliunga mkono Rais Magufuli alivyovunja katiba kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa?

Mimi ni msomaji Sana wa makala zako, uliandika hivi.

"Rais Magufuli yupo sawa kabisa, muda wa siasa umeisha, huu ni muda kufanya kazi ".

Ulishabikia Rais kuvunja katiba, kwa sababu katiba inaruhusu shughuli za vyama vya siasa na mikusanyiko yake.

Wanacholilia viongozi wa dini ni kile ambacho wewe Ulishabikia kiharibiwe.
Ndo maana nimekuambia kuwa ni bora tu ukae kimya.

Mwache Rais Magufuli afanye kazi, na tuache siye tulie, wewe kaa upande uliochagua.
 
Kwanini watu wanaolilia Uhuru wa kujieleza usiku na mchana hawataki kabisa Wengine kujieleza, inashangaza sana
Wewe umesema pointi kabisa. Hawapendi kwa sababu wao wanatafuta madaraka na siyo hiyo demokrasia wanayoisema. Nitajie nchi gani barani Afrika ambayo haiku was na demokrasia ila walipoingia wapinzani ndiyo wakawa na demokrasia hiyo waliyoihubiri majukwaani.
Nenda mitandaoni kwa yule chizi Mange, yeye anatukana watu asiowataka matusi ya nguoni eti anatafuta haki na demokrasia nchini. Cha ajabu ukimpinga tu (na wala hukumtukana) basi anakupiga ban. Sasa huyo anataka demokrasia? Akiingia madarakani ataiishi?
 
Umeongea ukweli sana,wanataka wote tufikiri kwa aina moja
 
Shigongo anakamkondo ka kumuingizia hela za hapa na pale. Huku anakoelekea itamletea shida
 
Umeongea ukweli sana,wanataka wote tufikiri kwa aina moja
nyie watu mmelaaniwa, laana ya kumwaga damu za watu kwa tamaa ya madaraka inawaponza na huyo Mwenyekiti wenu kwa uovu wake hafiki 2025,Mungu atampiga.
Nyie ndo mna chuki kubwa mno na wapinzani mnataka msikilizwe nyie tu, mwisho wenu umekaribia msidhani mtatamalaki tena.
 
Wewe umesema pointi kabisa. Hawapendi kwa sababu wao wanatafuta madaraka na siyo hiyo demokrasia wanayoisema. Nitajie nchi gani barani Afrika ambayo haiku was na demokrasia ila walipoingia wapinzani ndiyo wakawa na demokrasia hiyo waliyoihubiri majukwaani.
Nenda mitandaoni kwa yule chizi Mange, yeye anatukana watu asiowataka matusi ya nguoni eti anatafuta haki na demokrasia nchini. Cha ajabu ukimpinga tu (na wala hukumtukana) basi anakupiga ban. Sasa huyo anataka demokrasia? Akiingia madarakani ataiishi?
Mange chizi. Wanaom support anawaacha na wanaompinga anawapiga ban. Alafu ana generalize kuwa watu hawaioendi serikali. Kumbe wasioipenda ni wale wachche ambao hajawapiga ban
 
Mange chizi. Wanaom support anawaacha na wanaompinga anawapiga ban. Alafu ana generalize kuwa watu hawaioendi serikali. Kumbe wasioipenda ni wale wachche ambao hajawapiga ban
Mange ana followers wengi kuliko Magufuli
Anawapiga ban wale Waingereza wanawaita TROLLS
 
Kazoea udaku huyo achaneni nae, pia anawinda tenda za t.shirt na kofia apige pesa za ccm 2020 kama alivyofanya 2015.
 
Kama mtu unaejiona unaweza kutoa ushauri kwa wachungaji wa KKKT na kama huoni maovu yanayotendwa na watawala dhidi ya wale wenye mawazo tofauti na wao basi wewe ni mbumbumbu au una yako moyoni!
Ungekemea yanayoendelea Nchini ungeonekana una busara zako lkn najua huwezi kukemea kutokana na sababu kuu mbili
1. woga wa kufungiwa vijarida vyako vya udaku
2. Kukosa tenda za ccm ktk chaguzi.
 
Back
Top Bottom