Eric Shigongo afiwa na baba yake

Uda

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
811
624
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Bw. Eric Shigongo, anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi na Mwenyekiti wa Global Publishers Ltd, Mzee James Bukumbi, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumapili Tarehe 26/8/2012 katika Hospitali ya Burhani jijini Dar es salaam.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Kijitonyama, Barabara ya Sayansi, jirani na Heko Motel, Dar es salaam.

Marehemu atasafirishwa kwenda Mwanza kwa mazishi Jumanne 28/8/2012 na maziko yatafanyika kijijini kwake Bupandwamhela,…

source blog yake mwenyewe

RIP baba shigongo,wanaJF tuweke ushabiki pembeni tumpe pole ndg shigongo
 
Pole sana Bw Shigongo.Inauma sana kupotelewa na mzazi. Mungu akupe ujasiri wa kuvumilia uchungu huu mkubwa. May the Lord give him eternal peace, Amen
 
RIP Mzee ila kama hatakuwa ameacha laana ya kumpiga marufuku Shigogo ku support chama kinachoimaliza nchi(CCM) usia wake utakuwa hauna mashiko
 
Mzee anabahati mbaya sana huyo! Mtoto wake japo anapata hela lakini anafanya biashara ya udaku nchini!
 
Shigongo achukue nafasi hii 'kujifunza'

hupaswi shabikia ugonjwa wa mtu wa kifo cha mtu

'anavyomfanyia Diamond now sio utu'
mbaya zaidi ni uzushi kuliko ukweli
 
Shigongo achukue nafasi hii 'kujifunza'

hupaswi shabikia ugonjwa wa mtu wa kifo cha mtu

'anavyomfanyia Diamond now sio utu'
mbaya zaidi ni uzushi kuliko ukweli
naona mpicha mkubwa wa wema sepetu ndio unapamba blog yake.
 
Kapumzike kwa amani mzee, japo umetuachia toto halina adabu linapamba picha za uchi za dada zetu kwenye vigazeti vyake
 
Pole sana Shigongo kwa kufiwa na Baba yako mzazi.
Wakati wa msiba wanaJF tuungane pamoja kutoa pole na kusaidia kinachowezekana, mambo ya lawama yafuate baada ya mwili wa marehemu KUPUMZISHWA ARDHINI.
Kwa mila za kiafrica ni aibu kuwananga mfu na mfiwa kabla ya mazishi.
 
Pole kwa shigongo
- naomba na vigazeti vyake viandike "freemason wamchukua baba wa shigongo" au "shigongo amtoa kafara baba yake"
 
Aisee babaangu MKE WANGU AMUUWA BABA YANGU naingoja hadidhii mzeee pumzika kwa amani

ngoja nisimamishe kunjwa mbege
 
Daah Pole Eric pesa imeshindwa kumuokoa baba yako, nilisikia kuwa ulimpeleka India kwa ajili ya matibabu lakini imeshindikana ukamrudisha nchini akiwa bado hana afya njema, umepigana sana kuokoa maisha yake lakini Mungu amempenda zaidi, pole.
 
pole sana mzee wa ku-modify hadithi eric shigongo kwa kufiwa na baba yako.
 
Back
Top Bottom