Erasto Zambi amefariki dunia

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,594
446
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olympic Tanzania Mzee Erasto Zambi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake ubungo kibangu DSM habari zaid simu no 0652034505
 
RIP Erasto Zambi. Nakumbuka nilisoma na mwanae Lutengano sec school back in 80's Poleni sana wafiwa!
 
Ndio maana zambez bar ipo kimya pale riverside kumbe boss kaondoka R.I.P
 
mola aiweke roho yake panapomstahili,sote tuliumbwa kwa udongo na sote tutarudi udongoni
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olympic Tanzania Mzee Erasto Zambi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake ubungo kibangu DSM habari zaid simu no 0652034505

Mipango ya mazishi imekamilika atazikwa kesho jumapili 30/09/2012 katika kaburi lililoandaliwa katika shamba lake jirani na nyumba yake, wanaopenda kufika katika msiba huu, Kwake ni Ubungo Kibangu jirani na shimo la kajima jirani pia na bar ya Kwa Mlacha.
 
[h=3]
[/h]
8:53 AM


DAR ES SALAAM, TANZANIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea jana (Septemba 26 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi.



Zambi ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili (Septemba 30 mwaka huu) kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.


Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.


TFF inatoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Zambi mahali pema peponi. Amina
 
Back
Top Bottom