Wadau,
Hata kama ni uwekezaji lazima ufuate sheria za nchi husika, lazima kuwe na win win situation.
Kwa bahati mbaya sivyo hivyo kwa haya mabenki ya nje yanayofurika nchini kila uchao, wanakuja kutuibia na kutuhujumu. Najiuliza, wanapata wapi ujasiri wa kukiuka masharti ya biashara na uwekezaji? Hivi ni kweli Benki Kuu haina mechanism ya kucheki kama haya mabenki yanafuata sheria za nchi.
Wiki tatu zilizopita nilienda Equity Bank pale Golden Jubilee kuchenji dola elfu mbili ili nipate shilingi niweze kufanya malipo mbali mbali ya kiofisi. Nilipofika Equity Bank nilielekezwa nipande ghorofani ambapo nilimpatia teller hizo dola ili anipe shilingi. Ajabu ni kuwa, nilipomwomba risiti akagoma ati hawatoagi risiti! Nikamwambia hicho kitu haiwezekani na hakipo, dada akasema ndivyo ilivyo na akamuuliza jirani yake ili nithibitishe, na mwenzake akanithibitishia! Ndipo nikawaambia wanirudishie dola zangu nikaenda kubadilishia Bureau de Change ambao baada ya kudai risiti walinipa.
Ijulikane kuwa hata hizo Bureau de Change nao ni hivyo hivyo, risiti ni hadi uidai. Wenzetu Uganda hata ukiwa unauza dola ili upate shilingi yao lazima wadai passport na wajaze fomu kadhaa na kukupa risiti yako, yaani huhitaji kuuliza.
Nachotaka kusema ni kuwa hawa Equity Bank wanahujumu uchumi wetu, wanatorosha dola zetu kupeleka kwako na hivyo kusababisha kushuka na kuporomoka kwa shilingi yetu.