Equity Bank Arusha imefilisika, BOT ingia kati mapema

Equity Bank Arusha imefilisika, BOT ingia kati mapema

Status
Not open for further replies.

morenja

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
4,518
Reaction score
1,855
Bank ya Equity Arusha leo siku ya 15 wameshindwa kutupatia pesa zetu tuliohifadhi katika bank hiyo, tunaomba bank kuu ifuatilie jambo hili haraka.

Kuna kila dalili bank hii imefilisika au kuna wizi mkubwa umefanyika. Isijekuwa kama bank ya Greenland wakati ule, kwani haiwezekani kutuambia hawatupi hela zetu kisa mtandao wa internet ni mbovu.

Bank kuu tunaomba mwingilie kati mara moja kabla hii bank kutoka Kenya haijatoweka na mamilioni yetu. Ajabu sana, yaani siku kumi na tano unanyimwa kuchukua pesa yako. Imekuwa Uturuki!? Na taarifa pia kwa ubalozi wa Kenya hapa Tanzania.

Nawasilisha
 
Polee mkuu wamezipeleka kwenye maduka ya M Pesa wanazizungusha kwanza
 
Ndugu morenja nadhani unachanganya mambo.Leo nimetoka Equity nimechukua 1,700,000/= bila shida yoyote.Equity ni moja ya bank zinazofanya vizuri katika soko.Mtandao kwenda down hiyo ni biashara nyingine kabisa hasa ukizingatia umeme ni tatizo sasa Arusha sijui mkoa mingine.
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa ni mzushi aisee....nimetoka leo asubuhi hapo kudroo pesa za kutosha kabisa....
 
... bank kuu ifuatilie jambo hila haraka.

Bank kuu tunaomba mwingilie kati mara moja.
Hakuna Kitu kama Bank Kuu TanZania bali kuna Benki Kuu, kuwa makini kama unataka kusaidwa na kusikilizwa!
 
Mimi nashangaa haka kabenki kamekuja juzi kanataka kushindana na wakina exim na crdb , unaweza kuta wanadanganya kwenye balance sheet zao tuwaone wanakua , Mkenya siku zote anatakiwa aangaliwe na jicho la tatu hapa kwetu.
 
Ndugu yangu benki ndogo hizi ni changamoto sana,no vizuri kuwekeza kwenye benki zetu zenye financial mascles kama NMB
 
Wewe Jamaa huelewi chochote kuhusu bank....hakika umenichekesha sana.....Hapo Arusha hako ni ka branch tu...Naapa kwa jina la mwenyezi Mungu CRDB inaweza kufilisika lakini siyo Equity Bank.Equity wako vizuri sana anytime soon wata-dominate soko la Tanzania.
 
Mimi nashangaa haka kabenki kamekuja juzi kanataka kushindana na wakina exim na crdb , unaweza kuta wanadanganya kwenye balance sheet zao tuwaone wanakua , Mkenya siku zote anatakiwa aangaliwe na jicho la tatu hapa kwetu.
Hata mimi kwa kweli nakashangaa Bank gani imeanza mwaka 2014 eti leo hii wana Branch Rwanda,Sudan,Tanzania,Uganda etc.... Nashangaa sana
 
Wewe Jamaa huelewi chochote kuhusu bank....hakika umenichekesha sana.....Hapo Arusha hako ni ka branch tu...Naapa kwa jina la mwenyezi Mungu CRDB inaweza kufilisika lakini siyo Equity Bank.Equity wako vizuri sana anytime soon wata-dominate soko la Tanzania.

Hakuna atakayedominate tofauti na wale wanaodominate sasa hivi.
 
Mimi nashangaa haka kabenki kamekuja juzi kanataka kushindana na wakina exim na crdb , unaweza kuta wanadanganya kwenye balance sheet zao tuwaone wanakua , Mkenya siku zote anatakiwa aangaliwe na jicho la tatu hapa kwetu.
Equity z one of de leading banks in East Africa...
 
Arusha ni branch Dar ndio head office ya TZ Equity Bank subsidiary. Kama mtaalamu wa masuala ya kibenki, branch haiwezi kufilisika, angalia vizuri labda account yako haina hela au ina tatizo lingine
 
Hakuna atakayedominate tofauti na wale wanaodominate sasa hivi.

Ukubwa wa bank na kutopewa pesa zetu inaniusu nini. Na wala asitudanganye, hii ni bank ya wamachinga Kenya, haiwezi kuja kushinda CRDB au NMB
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom