Equations that changed the world

Mambo hayo yalikuwa yananikela kweli ma pertubation, hilbert space, operator na hiyo shrodinger's ahh. Mi mpenzi sana wa classical physics mambo ya V = IR
Utakuwa ulikuwa hauelewi, hesabu ni moja ya starehe kubwa sana maishani baada ya kumeditate juu ya neno la Mungu wa Mbinguni.
 
Thanks! makaveli10 Volatility Mawembasa1979 nimepokea jawabu kutoka kwenu.
 
Baada ya kukosekana kwa equations za baba wa algebra na mgunduzi wa zero(0) ndg Muhammad ibn Musa al-Khwarizmi, pamoja na fundi pekee wa hisabati ndg Augustin-Louis Cauchy, ninadiriki kusema aliyeleta uzi huu ana mahaba binafsi na kazi za hao aliowataja.
 
Samahani! Hivi hizi equations huwa zinatumika wapi baada ya Kumaliza masomo?
-
Benki naona calculators
Ndege naona programmed systems
Engineers naona scientific calculators na programmed softwares
Doctors naona programmed systems & softwares
Ni lazima upass mitihani kabla hujafika huko. Sikuzote shule ni ngumu kuliko kazi.
 
😂😂😂
Na akina "aunt Ezekiel"
 
ninadiriki kusema aliyeleta uzi huu ana mahaba binafsi na kazi za hao aliowataja.


Hapo penye "mahaba" binafsi panahitaji ufafanuzi wa kina.
 
Kumradhi, hivi kwa hao waliovumbua wote kunaye Mweusi hata mmoja? Nani aliyeturoga, tuna nini hata kimoja cha kutumia ubongo na kufikirisha ambacho kilivumbuliwa na mweusi.
Maana huu uzi naona watu wanalalamika namna hizo formula zilivyo ngumu, ina maana sisi hata kuzitumia bado ni kwa mbinde licha ya kwamba hatujahusika kwenye kuzigundua.
Waafrika tuamke, tubukue, tutumie bongo zetu ili na sisi tutajwe humo wanapotajwa wengine....hehehe
 
Tumevumbua vumbi la congo
 
Kwenda na kasi ya dunia, unaonaje tukianza kufundisha hizo ready made programmed softwares & tools.

Mfano! Simu janja mtu anakuwa hana ufahamu lakini anajifunza hatua kwa hatua na kuweza kuhimili sio lazima afahamu metric, codes na system behind it.
Swala Zima la elimu na shule limekupita pembeni
 
Utakuwa ulikuwa hauelewi, hesabu ni moja ya starehe kubwa sana maishani baada ya kumeditate juu ya neno la Mungu wa Mbinguni.
Mimi hadi leo huwa nikichoshwa na mihangaiko ya Dunia huwa nachukua Kitabu cha Pure Mathematics (Back House au Tranter) napiga maswali matatu au manne hivi, then akili inakaa sawa.
 
wasomi hawathaminiwi africa.
 
Ajitokeze mtu mmoja afafanue applications ya hizi eqns katika uhalisia
 
Nyutoni kanuni zake tunaishi nazo siku zote za maisha yetu hapa Duniani kwa kujua ama kutokujua.

Vizazi vyote vijavyo Duniani lazima waziishi kanuni zake.

Nyutoni sijui alikua anafikiri nini kichwani mwake.
Alikuwa ni Genius yule jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…