T11
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 5,096
- 4,578
EPUKANA NA WATU WENYE SIFA HIZI 6 KWA AJILI YA AFYA YAKO YA AKILI
Afya ya akili siyo kipaumbele kwa watu wengi kwa sababu wengi huamini elimu ya darasani inatosha
Kama na wewe unaamini elimu ya shuleni pekee uliyohitimu inatosha kwa kila kipengele cha maisha yako basi upo kwenye upotevu.
Afya ya akili inachukua sehemu yote ya maisha yako kwa maana akili ikiwa timamu utafanya vitu kwa ufasaha na akili ikivurugika bila kujali kiwango cha elimu cheo,umaarufu,utajiri kila kiti kitavurugika
Ukiona unafuraha kuna sababu na ukiona unahuzuni kuna sababu ikiwa sababu huijui haina maana sababu haipo isipokuwa ni ufinyu wa elimu ndiyo kikwazo.
95% ya mafanikio yako yanaathiriwa na watu waliokuzunguka.
Ikiwa umekaa na maadui nafasi ya kufanikiwa ni ndogo sana na ikiwa umezungukwa na watu wenye malengo kama yako utafanikiwa haraka.
Tunaishi na watu ambao ukiwatumia sms wanakujibu baada ya masaa kibao kupita ila ukiwa nao wanakuwa bussy na simu kujibu sms za watu wengine
Tunaishi na watu ambao wakikukosea wanadai shetani,bahati mbaya,ajali ila wewe ukiwakosea watakulaumu kama vile wao ni malaika.
Kuna aina 6 za watu ukiwa nao utateseka sana ni wajibu wako kuwajua na kwa sababu kila mtu yupo huru kutumia akili yake basi ni hiyari kwako kufuata au kuacha ila hakuna mwenye lawama juu ya maamuzi yako.
1.MTU ANAEKUTUKANA KILA WAKATI
Huyu anaweza kuwa ndugu,rafiki,mwajiri,jirani n.k lakini kutokana na ukaribu wenu anakuwa anatumia muda mwingi kukutukana,kukukejeli,kukusema vibaya kwa watu,kukukatisha tamaa,kukosoa vikali juhudi zako,kukulaumu sana kila mambo yakienda tofauti.
2.ASIESAMEHE MAKOSA YAKO
Tunajua kuwa kila binadamu anakosea haijalishi ni msomi,tajiri,mwenye hekima,mpole,mkali n.k lakini kila mtu anakosea kwa wastani kila mtu anakosea kwa 70% ya maamuzi kila siku na maamuzi hayo hupanga afanikiwe au kufeli hivyo ukiona umefeli hakuna aliekufelisha bali maamuzi yako mwenyewe.
Watu wasioweza kukusamehe utajitahidi kuomba msamaha kila siku lakini ataendelea kutaja makosa yako kila wakati,utajitahidi kuwa mwema lakini atakuhukumu kwa makosa ya zamani mtu huyu hafai kabisa kuwa sehemu ya maisha yako kwa sababu kila siku utajiona mkosaji hata kama umebadilika sana kitabia
3.ANAETAJA MABAYA YAKO KILA WAKATI
Unaweza kuwa unatokea kijijini,familia maskini,hakuna msomi kwenu,hamna muonekano mzuri kimaumbile,hamna mtu maarufu ukoo mzima,wazazi wako wamezeeka sana n.k hivyo rafiko yako anatumia mwanya wa madhaifu yako kaa fimbo,labda amenunua zawadi atasimulia kila kona kuwa yeye ndiye aliekusaidia sana kimaisha,labda amekuwomesha kila wakati anahadithia kwa watu kuwa bila yeye usingetoboa kimaisha n.k mtu huyo hakufai atakufanya ujidharau sana kila ukimwona.
4.MTU MWENYE KUKUKEJELI SANA
Wapo watu ambao haijalishi utajituma sana kazini,ufanye usafi sana,uwe mstaarabu sana bado atakejeli juhudi zako,ataona mabaya yako,haijalishi utafanya mazuri kwa 99% bado atakulaumu kwa 1% ambayo hukufanya vizuri
Ikiwa anashida unamsaidia ila siku akipata shida usipoweza kumsaidia atasimulia kila kona ubaya wako.
5.MWENYE KUTAJA AIBU ZAKO KWA WATU
Wapo watu ambao ukiwa na shida kwa sababu hujuwajua tabia mwanzo ukiwaamini ukawapa siri zako ambazo zingine ni za aibu ila siku umkwazana nae atatumia mwanya huo kutaja aibu zako,kutaja mara ngapi amekusaidia,atakulaumu kuwa hufadhiliki,atakulaumu hata kwa makosa hujafanya,kikipotea kitu atadai umeiba wewe hata ukibainika uehaihidi kuwa si wewe bado ataendelea kukutuhumu,anaetaja dosari za mwili wako kwa kukusema vibaya kuhusu kasoro za sura na rangi hafai kuwa karibu yako.
Hakuna anaependa kutajiwa kasoro za sura na rangi kwa sababu huwezi kubadilisha sura wala asili yako hivyo yeyote anaetumia mwanya wa kukusema kwa kutaja kasoro za sura,rangi,maumbile,kabila,mqhali ulipozaliwa,historia yako hafai kuwa mtu wa karibu,utakuja kugundua kuwa sehemu kubwa ya stress zinatika kwa watu ambao tabia zao huzipendi.
Tafuta watu wenye tabia nzuri tumia muda mwingi kuwa nao.
Unapokaa na watu ambao tabia zao na zako haziendani lazima utapata matatizo ya hasira.
Hasira huchochewa sana na watu waliotuzunguka
kama tunatumia muda mwingi sana kuwa nao.
Mazingira yako kama yanachochea hasira yabadilishe,watu waliokuzunguka kama wamachochea hasira kwako tengana nao.
Kuna watu unaweza kununua kitu dukani ila watakavyokisema kwa dosari utasikia "mshamba wewe ndiyo maana unapigwa kila siku,nguo hiyo mimi siwezi kununua hata kwa bure sichukui" watu wa aina hii wanakusema kwa kejeli huku kusudio lao ujisikie vibaya
Hakikisha mtu ambar ukiwa nae unajiona mdogo,unajitoa dosari mwenyewe,unajiona mshamba,unajiona tabaka la chini,unajiona huna lolote la maana tengana nae bora ukae mpweke kuliko kukaa na watu wenye kukusababishia hasira kila wakati.
Ikiwa utatumia muda mwingi na watu wenye malengo kama yako huwezi kusikia ukikoselewa kwa lugha chafu,huwezi kusikia unadhalilishwa kwa sura,rangi au kabila au kusikoa sifa mbaya za mahali ulipotoka.
Kwanza hakuna mtu mzuri 100% na hakuna mtu mbaya 100% hivyo yeyote anaetaja ubaya wako na yeye ana mabaya yake.
Haijalishi mtu atasifika kwa tqbia nzuri kiasi gani bado kuna sifa mbaya amezificha hivyo usiwe na hofu kwa watu kukuandama kwa makosa yako kwa sababu hata wao wanakosea isipokuwa huwa wagumu kukubali makosa yao
Mtu anaetaja mabaya ya watu wengine muda wote huyo ndiye mbaya zaidi kwa sababu hawezi kukubali kama anakosea hata siku moja.
Ukiona umekosea kubali kosa jirekebishe ila ukiona mtu anajitetea sana huwa akikosewa atalaum kupita kiasi.
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam