Epuka windows iliyochakachuliwa inayoweza kuwa na virusi au matatizo, piga windows original na kui activate kwa njia salama

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Kuna hizi windows za kudownload kutoka mitandaoni hususan kwenye torrents huwa zimekuwa cracked, pre activated na nyingine zipo modded

Ndizo windows ambazo wengi hutumia hapa bongo sababu kuu ni kukwepa gharama ya window original, bei imechangamka inafikia takribani laki 3, hata baadhi ya ofisi za serikalini kuna IT wanapewa pesa kununua windows original lakini wanaingia tamaa kucheza mchezo wa kuingiza hizo pesa mifukoni, kwenye computer za ofisini wanaweka windows za kuchakachua.

Hatari ya windows za kuchakachua ni kwamba zimeguswa, mchakachuaji anayachezea mafaili ya window original ili itumike bure huwa anafuta, ku edit au kuongeza mafaili. sasa kuna baadhi ya mafaili huwa yakiguswa yanafanya window isumbue, inaweza kuwa ni hatua ya kampuni kukabiliana na uchakachuaji wa bidhaa zake, mchakachuaji akiyagusa basi window hio itakuwa na matatizo (bugs) kwa watumiaji, mfano unakuta pc inakua nzito, inapata joto, kuganda, n.k. matatizo yanakuja kugundulika kwa watumiaji baadae kabisa.

Wachakachuaji wengine wakizigusa hizi windows huwa kwa maksudi wanatia ndani mambo yao wanatia ndani spyware software za kukuchunguza unachofanya kwenye pc mfano kuitumia kamera yako bila wewe kujua, wanatia ndani virus aina ya ransomware wanaofungia mafaili kukutaka uyakomboe kwa kuwalipa pesa ama kuyafuta, wanatia ndani bots za kuwafanya waitumie pc yako bila ridhaa yako mfano kuitumia pc yako kuminya matangazo ya blogs zao, n.k.

Pia linapokuja suala la ku activate windows, kuna software nyingi kwenye windows ukiweka zinakamatwa kama virusi kwa hio inabidi uzime kabisa ulinzi ili zitumike, kuna matoleo ya software kama kmspico wadukuzi wamezivamia wametia ndani madubuwasha yao, hii ni hatari sana.


1. JINSI YA KUDOWNLOAD WINDOWS ORIGINAL

1. Fuata hatua hizi kudownload windows original kutoka official source ya microsoft



Unavyo install windows hakikisha umezima internet, kwenye hatua ya kuingiza key tumia google kama kwenye picha, hizi ni kwajili ya kupigia tu window, sio matumizi rasmi.

1667498929942.png



2. KU ACTIVATE WINDOWS KWA USALAMA BILA SOFTWARE
Software za ku activate nazo zimeingiliwa na wahuni sikuhizi wametia madubuwasha yao ndani na ubaya ni kwamba ili zitumike inabidi uzime kabisa anti virus, hii ni hatari sana unaweza fungulia mlango mafuriko ya virusi.

kwa maelezo yafuatayo utaweza ku activate windows kwa urahisi bila software yoyote:

a.ukimaliza kupiga window unga internet.

b.Fungua command prompt kama admin

1667499123968.png


Mwanzoni kule tunavyopiga window ile hatua ya kuweka key ilikuwa ni ya kupita kizuizi tu, sio hatua ya kudumu na tukiacha hivyo hivyo window itaanza kukera kudai key kila mara na hata tukitumia zile za google zinadunda, hata zikikubali zinaweza kukusumbua huko mbele.

c. fuata hizi hatua kwenye video ili kusakafia kabisa activation iwe ya kudumu, tumia hata keys zile zile ulizotumia kwenye kupiga window ila kwa kutumia mbinu ya kwenye video.



DONE!!!!

Tahadhari: hatua hizi ni za kukwepa tu hatari za window zilizoguswa zenye matatizo ama kuwekwa wadudu na kukwepa software za activation zenye wadudu, kwenye matumizi ya window unapoweka software zilizovunjwa kunaweza kukuhatarishia ulinzi, be careful unapo weka hizo siftware umezipata kutoka websites walau credible na wahusika waliovunja wana reputation ya kujali usalama.
 
Unaweka OS official alaf unakuja ku install Program iliyo cracked ...

Ni hivi

Kuwa Attacked hakukwepeki hasa kwa wale wenye Elim ndogo ya Cyber security and how attacks are performed.

Vijana endeleen na Cracked OS nothing serious.
Sio kila crack ina virus japo ni muhimukuchukua tahadhari..

Software ambazo zipo cracked inabidi nazo source zake ziwe za kuaminika, sio unashusha tu software kisa umeiona youtube, hapo unaweza vamia mtumbwi wa vibwengo....

Binafsi software zangu cracked huwa nazishusha kutoka team-os.com ... huku angalau kuna uadilifu na watumiaji wanatoa maoni yao wazi.
 
Gharama ya kununua window na Microsoft office pekee unapata laptop nyingine. Africa tungekaziwa na Microsoft Hadi leo tungekua tunatumia typewriter.
Ni laki 2, hio laki 2 mbongo kuitoa ni kazi sana maana hata idm ya elf 27 kashindwa lipia kaona bore aendelee kutumia iliyochakachuliwa
 
Sio kila crack ina virus japo ni muhimukuchukua tahadhari..

Software ambazo zipo cracked inabidi nazo source zake ziwe za kuaminika, sio unashusha tu software kisa umeiona youtube, hapo unaweza vamia mtumbwi wa vibwengo....

Binafsi software zangu cracked huwa nazishusha kutoka team-os.com ... huku angalau kuna uadilifu na watumiaji wanatoa maoni yao wazi.
Ok utawin kudownload Crack ktk website za kuaminika then unaenda ku connect Free Wifi ya Office au Shopping Mall. System inakuw compromised kama kawaida.

Hukwepi kuwa attacked hasa hasa ukiwa Target.
 
Hapo umenunua OS bado ile package ya MsOffice.. Ukimalizs uende kununua 3rd party Antivirus software let say Avast.. Ulipie subscription..

Mzungu mwenyewe na hela zake afanyi huu ukhanith
Mcorosoft office nayo inaweza kuvunjwa kwa usalama kabisa kwa kutumia MAS ... ila huko kwenye software zingine kupata cracks ambazo zipo salama ni ngumu sana.. Rafiki yangu alingiza IDM ya kupekechwa kilchofatia mafaili yake yote yalifungwa
 
Ok utawin kudownload Crack ktk website za kuaminika then unaenda ku connect Free Wifi ya Office au Shopping Mall. System inakuw compromised kama kawaida.

Hukwepi kuwa attacked hasa hasa ukiwa Target.
Hiz cracks huwa ni kama bangi, at least ununue sehemu ambayo kidogo pana uaminifu kwa miaka mingi na hata wateja hakuna aliechizika na hapa ndio huwa natumia team os endapo kuna uhitaji... ni bora kuliko kweda mitandao ambayo haina reputation ambayo ni sawa na sehemu wanazouza bangi wanaiwekea unga na sumu za panya mpaka wateja wengine wameshakuwa mateja na wehu
 
Kuna hizi windows za kudownload kutoka mitandaoni hususan kwenye torrents huwa zimekuwa cracked, pre activated na nyingine zipo modded

Ndizo windows ambazo wengi hutumia hata serikalini lakini hatari yake ni kwamba zimeguswa, Ubaya unapokuja ni kwamba kuna baadhi ya windows hizi zilizoguswa uki install kwenye mashine zinakuwa na matatizo (bugs) kwa sabbu mchakachuaji alibadili settings ama kucheza na mafaili ya windows kwa kudhani hayata athiri chochote ila matokeo yake yanakuja kuwa ndivyo sivyo kwa watumiaji.

pia kuna waandaaji wengine wa hizi windows wanazozigusa huwa wanatia ndani mitambo yao ya kukuchunguza (spy ware), kufungia mafaili yako hadi ulipe (ransomware), kuicontroll pc yako (bots), kuweka virus , n.k.

Pia kwenye ku activate windows kuna software nyingi zinakuomba uzime kwanza anti virus, hii ni hatari sana unaweza kuingiza wadudu,


JINSI YA KUDOWNLOAD WINDOWS ORIGINAL NA KUIVUNJA MWENYEWE KWA USALAMA BILA KUZIMA ANTI VIRUS

1. Fuata hatua hizi kudownload windows kutoka official source ya microsoft

View attachment 2406087

Unavyo install windows tumia hizi keys unaweza kuzigoogle, hizi ni kwajili ya kui nstall tu, Tutakuja kuweka tena baada ya kuinstall

View attachment 2406089

Baada ya kuinstall unga internet

Fungua command prompt kama admin

View attachment 2406090

Fata hii tutorial

View attachment 2406098

DONE!!!!

Tahadhari: Uki install kwa njia hii unakuwa salama lakini ukianza kuingiza software ambazo zipo cracke zenye virus ni kazi bure,, Kama unaweka software cracked jirishishe kwamba kuna maoni ya kutosha kwa walioiingiza kwenye pc zao,
Unajua nini maana ya digital ceetificate mkuu ama unaongea tu
 
Unaweka OS official alaf unakuja ku install Program iliyo cracked ...

Ni hivi

Kuwa Attacked hakukwepeki hasa kwa wale wenye Elim ndogo ya Cyber security and how attacks are performed.

Vijana endeleen na Cracked OS nothing serious.
Tatizo jamiiforums kila mtu anajifanya mjuaji! Appreciate kazi ya stu na limu aliyoitoa! Haigharimu chochote. Kamaa wewe ni IT mzuri tupe solution zako basi! kama ukiona jambo unalifahamu zaidi boresha au kosoa kwa namna ya kujenga! ;)
 
Tatizo jamiiforoum kila mtu anajifanya mjuaji! Appreciate kazi ya stu na limu aliyoitoa! Haigharimu chochote. Kamą wewe ni IT mzuri tupe solution zako basi! kama ukiona jambo unalifahamu zaidi boresha au kosoa kwa namna ya kujenga! ;)
amen
 
Tatizo jamiiforoum kila mtu anajifanya mjuaji! Appreciate kazi ya stu na limu aliyoitoa! Haigharimu chochote. Kamą wewe ni IT mzuri tupe solution zako basi! kama ukiona jambo unalifahamu zaidi boresha au kosoa kwa namna ya kujenga! ;)
Soma vzr nilichoandika. usikurupuke
 
Back
Top Bottom