Epuka Sumu Hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epuka Sumu Hizi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chapa Nalo Jr, Feb 6, 2011.

 1. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Kwa wanandoa tu, haihusiani na uhusiano wa aina nyingine.

  Epuka maneno yenye mkao wa ki-selfish; Mfano- vyangu, changu, yangu, wangu, langu nk. Usiyaone madogo lakini yanaweza mfanya mwenza wako ahisi yeye si sehemu yako hivyo akaamua kukaa mkao wa tahadhari.

  Jitahidi kutumia maneno yenye viashirio vya umoja; Mfano- vyetu, chetu, letu, wetu nk. Haya maneno humfanya mwenzi wako awe na amani kwani umemfanya ajisikie kutotengwa. Tumia hayo maneno hata kama hakushiriki au changia pesa wakati unakinunua kitu husika. Si vizuri umenunua e.g friji basi siku zote wewe unatumia neno "friji langu", e.g. sentensi rahisi tu, "mpenzi hebu naomba unichukulie juisi humo kwenye friji langu", pamoja na lugha tamu iliyotumika lakini hapo kwenye "langu" pameshaharibu.

  Au mke umekaa na mmeo sebuleni halafu unasema "oh siku hizi mwanangu unanifurahisha sana", hapo unaweza mfanya mme wako ajihisi yeye si mshiriki katika kupatikana kwa huyo mtoto. Au mme umekaa na mkeo nyumbani halafu unasema " hii nyumba yangu inahitaji ukarabati mkubwa", ona sasa si ni vema angesema hii nyumba "yetu", pamoja na kwamba ameongea la maendeleo lakini mke rohoni mwake atakereka tu hata kama aliolewa jamaa akiwa na hiyo nyumba tayari, and vice versa. Mifano ni mingi.

  Ila kuna vitu vingine maneno yenye mkao wa selfish ni sawa tu kutumia; e.g. shati langu, gauni langu. mme/mke wangu nk.

  Nawasilisha na ndio imani yangu
   
 2. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ila wanaume wanapenda sana kusema "watoto wangu" anaweza kukwambia sipendi watoto wangu uwapeleke mahala fulani sijui kwa nini wanasema hivyo. Ila kweli kusema vyetu wetu inaleta raha sana
   
 3. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280

  Pengine wasema kweli ndugu, naomba hili liwe somo kwa wote ili kuwe na amani
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Au ukute mama hafanyi kazi either ni mama wa nyumbani tu wababa hapa wanatesa sana sana na hayo maneno. Mnamwaga chakula changu kwa sababu hamjui gharama, Umeifanya nini hii gari yangu. Hivi hii nyumba yangu mbona mnaichafua hivi. Changu, changu changu, haipendezi kwa kweli.

  Hekima ya Mungu itawale, na maneno ya vinywa vyetu yakolee munyu. Nawatakieni jpili njema.
   
 5. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  linguistically means, discourage the type one singular possessive pronoun 'MY' and encourage the plural 'OUR'
   
 6. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli tena hii tabia imezidi sana watu tujifunze kubadilika
   
 7. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,827
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Umenena vyema!nitazidi kumuomba Mungu,aniwezeshe kuepuka kauli na maneno ya aina hiyo ili ndoa yangu changa iweze kudumu.Asante kwa darasa murua.
   
 8. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280

  Asante ndugu kwa kusaidia kifikisha ujumbe kwa wale watumia kiingereza, ndio hivyo ifanyike kwa lugha mbalimbali hata hizi zetu za kikabila zina maneno ya kuleta umoja pia
   
 9. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kila kitu ni cha mume kwa taarifa yako....watoto wangu, nyumba yangu na hata mke ni wangu pia....they are all mine.

  kama anataka viwe vyetu, basi arudishe mahari.....na kusiwe na send off....na wote tuanze bila bila, halafu kila mtu akafanye kazi na tuchange hela 50/50 tununue vitu VYETU.
   
 10. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wenye tabia za umimi sana ni wanaume,

   
 11. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nakuandalia juic ya ukwaju unywe akili zikuzid zaid nxt tym useme tena mema
  thaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaax
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  umemaliza kuongea baba?
   
 13. m

  mankind Senior Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  we makandokando hebu kaa kando tu.
   
 14. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,659
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Sawasawa
   
 15. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Asante, ila hicho kinywaji huwezi badilisha kidogo nipate ile kitu inafanya mtu achangamke ili TBL izidi kutoa ajira kwa watanzania!
   
 16. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280

  Asikwambie mtu ndugu mambo yamebadilika kweli siku hizi nao wanawake wana pesa ile mbaya; hivi hujasikia mwanamke anamsitiri mchumba wake kisiri siri na kumpa hela akatoe kama mahali, yaani mbele ya jamii ionekane mwanaume ndio katoa kumbe kuna siri nyuma yake.

  Hata wanawake nao wanatakiwa ku adopt hali ilivyo isiwe manyanyaso kwa mwanaume kisa yeye waziri/au bosi fulani wakati mme wake ni mtumishi wa kawaida sehemu nyingine(ila sujui ngoma inakuwaje mke akiwa bosi katika ofisi hiyohiyo anayofanya mmewe)

  Kuhusu sendoff; nimesikia nao wanaume siku hizi eti wana kasherehe kanakofanana na sendoff yaitwa bag party (mimi sijawahi hudhuria)
   
 17. T

  The Man Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka ulicho zungumza ni kweli kabisa na mimi nimesha experience kutoka kwa fiancee wangu.....nilikuwa namazoea sana ya kusema yangu.. changu ...vyangu na akawa anasononeka sana lakini nashukuru mungu alikuwa muwazi na akanipa somo kama ulilo toa hapa. Pia nili-learn kutoka kwake chochote atakacho pata ( hata lama ni allowance ya kikao au safari) atasema tumepata hela hii na akitaka tushauriane tufanye nini....I have learned alot brother kwenye hili, i was not meant to be selfish at the beggining - but it just happened i was using such self possessive words.....Sasa hivi nimejifunza na mambo yanakwenda .....!!:A S thumbs_down:
   
Loading...