Sukari yeyote ni hatari katika mfumo wa mwili, Wataalam wanathibitisha uwepo wa takribani vijiko 10 vya sukari katika kila chupa moja ya soda, kwa maana hiyo unapokunywa soda 5 kwa siku maanake unakula vijiko 50 vya sukari iliyo kwenye maji yaliyochanganywa na sukari (soda) pamoja na kemikali inayolinda soda isiharibike, kitaalam pia kwenye soda kuna kiwango kikubwa sana cha ACID (PH 2-3).
Kiwango cha kemikali kilichopo ndani ya tumbo la binadamu kinadaiwa kuwa na Ph ya 3 ambayo huweza hata kusaga mfupa uliomezwa kwa bahati mbaya,Hivyo basi, kemikali iliyopo kwenye soda ni kali zaidi ya hata iliyopo tumboni mwa mwanadamu.
INSULINI kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini,Kongosho ina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula (Mmeng’enyo).
Ikumbukwe kwamba kiwango cha sukari mwilini huchujwa sehemu ya kongosho, kongosho linapofail kuchuja ndipo sukari huanza kupanda taratibu, kiasi kwamba mtu hupata kisukari na magonjwa mengine, kongosho inapofail hapo ndipo binadamu huanza kutapata, hapo ni sawa na dreva kuambiwa apunguze speed anakaidi akitegemea BREAK, na Break inapofail hapo ndipo CHANGAMOTO huanzia.
Yamkini huenda BIA ikawa ni bora zaidi kuriko kunywa soda hizi tunazokimbilia kila siku.
Dalili za kisukari
a. Kukojoa mara kwa mara
b. Kiu Isiyoisha:
c. Njaa Kali:
d. Kuongezeka kwa uzito (unene):
e. Kupungua uzito kusiko kawaida:
f. Uchovu wa mwili:
g. Hasira:
h. Kutoona vizuri:
i. Vidonda kutopona vizuri au haraka:
j. Magonjwa ya ngozi:
k. Kuwashwa kwa ngozi:
l. Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba:
m.Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa:
n. Ganzi mikononi au miguuni:
Zifuatazo ni baadhi ya Athari za sukari ;
i. Sukari huweza kuathiri ukuaji wa homoni mwilini ( kitu ambacho ni muhimu kwa kumfanya mtu kuishi na afya njema wakati wote )
ii. Sukari ndiyo chakula cha saratani mwilini.
iii. Sukari huongeza lehemu ( cholesterol ) mwilini.
iv. Sukari huweza kusababisha kizunguzungu na kudhoofisha mwili kwa watoto.
v. Sukari huweza kudhoofisha nguvu ya macho
vi. Sukari huweza kuzuia utembeaji wa protini mwilini
vii. Sukari huweza kusababisha mzio wa chakula ( Food allergies )
viii. Sukari huchangia ugonjw a wa kisukari
ix. Sukari huweza kusababisha ugonjwa wa moyo.
x. Sukari huweza kuharibu, umbo la vinasaba vya mwili ( D.N.A )
xi. Sukari huweza kusababisha utukutu, utundu na kukosa umakini kwa watoto.
xii. Sukari huweza kuchangia kupunguza n kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yatokanayo na wadudu aina ya bacteria ( infectious diseases )
Hizo ni baadhi tu ya hizo sababu 146. Je, kwa kujua sababu zote zilizo thibitishwa kuhusu madhara yatokanayo na sukari, kuna sababu gani ya kuendelea kupenda kutumia sukari jamani?
Ingawa Hatuwezi kuiepuka sukari moja kwa moja kwani baadhi ya vyakula huwa havitamkwi moja kwa moja jina la kuwepo kwa sukari bali hutumia majina kama Glucose, fructose n.k Yakupasa wewe mwenyewe utokomeze ulaji wa sukari kwa kujiwekea mikakati yako, punguza matumizi ya soda,
kuna watu wakipata kiu badala ya kunywa maji hukimbilia soda, Soda ni kinywaji hatari sana kuriko BIA, Hasara ya Bia ipo kwenye gharama na ulevi unaomfanya mtu asijitambue, Lakini madhara ya soda/sukari ni Makubwa sana.