Epuka Makosa Yafuatayo Kama Umeamua kuanza Biashara ya Cryptocurrency

Mr Fresh

Member
May 30, 2021
22
71
Mara nyingine huwa inaumiza sana kutazama watu wapya katika biashara ya crypto wakifanya makosa ambayo yanawapelekea kukata tamaa au kupoteza mitaji yao

Japo haikuhitaji kuwa mtaalamu sana ili ufaidike na cryptocurrency lakini kuna mambo kadhaa ya msingi unapaswa kuyafahamu

Leo nitakufundisha juu ya makosa 5 makubwa ambayo unatakiwa kuyaepuka kipindi utakapoaanza uwekezaji wa cryptocurrency

1. Kununua Sarafu Zenye Marketcap Kubwa Pekee

Marketcap ni thamani ya idadi ya sarafu zote za aina moja zilizopo kwenye mzunguko wa soko ukizidisha na gharama ya sarafu moja katika kundi hilo.

kununua Sarafu zenye marketcap kubwa kama Bitcoin na Etherium peke yake sio njia nzuri ya kutengeneza pesa kwenye crypto. Portifolio yako inapaswa kuwa na mchanganyiko wa sarafu zote zenye marketcap ndogo,size ya kati pamoja na marketcap kubwa.

Kitu cha kuzingatia ni kwamba sarafu zenye marketcap ndogo zinaweza kukutengenezea kipato kikubwa ila unahitaji umakini mkubwa sana katika kuzichagua ni zipi za kuwekeza ili usipoteze mtaji wako kwa maana kundi hili ndo linaongoza kwa kuwa na sarafu nyingi zaidi kuliko makundi yaliyobaki

2. Kununua Sarafu kipindi Ipo Juu(Buying The Top)

Watu wengi hufanya kosa hili kwa kuamini sarafu wanayotaka kuinunua itaendelea kupanda juu zaidi bila kushuka haliyakuwa hivyo sivyo ambavyo soko la cryptocurrency linavyojiendesha. subiri sarafu ishuke kidogo kisha nunua tena kwa kuigawa pesa yako katika mafungu 3, asilimia 40 manunuzi ya mwanzo,asilimia 30 manunuzi yanayofuata endapo ikishuka tena,na asilimia 30 manunuzi ya mwisho.

3. Kutokufanya Utafiti Binafsi Kabla Ya Kununua Sarafu

Kuna msemo katika cryptocurrency unaitwa "DYOR" wenye maana ya "Do your own Research". yan kufanya utafiti binafsi kabla hujanunua sarafu fulani,watu wengi ni wavivu sana juu ya hili swala na hii huwapelekea kununua sarafu ambazo si sahihi na kuishia kupata hasara kubwa au kupoteza kabisa mitaji yao

Vipo vyanzo vya uhakika vya kukusaidia wewe kufanya research yako kama coinmarketcap.com, coingecko.com, cointelegraph.com, rarity.tools, cryptobubbles.net n.k.

4. Kutokufahamu muda wa kuchukua faida/ kutoka sokoni

Mtu anaponunua coin nzuri kisha ikaanza kupanda thamani sokoni basi mara nyingi hujisahau na kuendelea kuiacha tu kwa kuamini kwamba itapanda zaidi hatimaye soko linashuka na kuchukua tena faida yake yote.

Hii inatokea kwa sababu ya kutokujiwekea malengo ya "nahitaji faida kiasi gani kwa uwekezaji huu ndani ya muda huu", "je muda huu ukifika na sijapata faida hiyo nifanyeje". Pia kuridhika na faida ndogo unayopewa na soko ni bora zaidi kuliko tamaa ya faida kubwa zaidi kisha uikose.

5. Kuuza Sarafu Kipindi Ambacho Soko Limeshuka

Hii ni sawa na kukubali hasara na si wazo zuri kulifanya, ni vyema kuendelea kuhold sarafu zako katika kipindi hiki kwa sababu ni kawaida ya soko la crypto kushuka na kupanda tena. Ila endapo una shida ya pesa kipindi soko limeshuka basi unashauriwa kuchukua mkopo wa crypto ambao unaweza kuupata kupitia soko la binance ndani ya dakika 1 tu. huu mkopo huwa ni kama robotatu ya pesa ulizonazo ndani ya soko na riba yake ni nafuu zaidi asilimia 1.8 tu ndani ya siku 180.
 
Izo ni theory unataka kufundisha watu upige pesa nenda kahold coin kama unajua sana
 
Nani mwingine anaona hayo madude kama mazingaombwe kama mimi
Siyo mazingaombwe mkuu mimi binafsi nilinunua binance coin 10 kwa $10 kila moja ambayo ilikuwa roughly sh 250,000/= za kitanzania alafu thamani yake ikapanda mara 50 nakaziuza dola $530 kila moja ambapo nkaziuza zote kumi kwa $5300 ambayo ni Mil 12 za kitanzania
 
Nani mwingine anaona hayo madude kama mazingaombwe kama mimi

IMG_3379.png

Endelea kuona mazingaombwe mkuu…
 
asilimia 40 manunuzi ya mwanzo,asilimia 30 manunuzi yanayofuata endapo ikishuka tena,na asilimia 30 manunuzi ya mwisho.
 
Shida ya watanzania ni ubishi na ujuaji ata kama hujui chochote sasa hv unaweza kufanya manunuzi yoyote mtandaoni kwa kitumia crypto currency alaf jinga na pumbavu mmoja anakuja kukejeli.
Mimi nawaombea tu uzima miaka ijayo waone kitakachotokea uzur haya mambo ata watu wa dini wanayasema sana kama ndio ile mwanzo wa hekaheka za mwisho wa Dunia.

Tunapoenda Dunia haitokuwa tena na hzi sarafu tunazoziona ndio maana nchi kama sweeden na Finland washaanza kuwekewa chip kwenye mikono yao ili waweze kufanya Transaction kokote.

Technology unatakiwa uende nayo kwa umakini sana usije ukadhan hyo Bitcoin aligundua Satoshi Nakamoto peke yake, kuna documentary na jalada nying zinasema hii system ni ya watu ambao ata gvt flan flan wanawafaham ambao waliwekwa bootcamp na kutoka na idea hyo ila tu dunia ndio imedanganywa.
 
Back
Top Bottom