Epuka haya unapoanzisha mahusiano mapya ili mwanamke azidi kuvutiwa nawe

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Mwanzoni mwanamke anakuwa bado hajajiwekeza sana kwako, hasa miezi mitatu ya kwanza. Bado atakuwa anaangalia aendelee na wewe au la. Bado anakusoma kama atapata usalama kwako au la.
Kama nawe unamtaka kweli huyo mwanamke ni muhimu kuepuka haya;

Kujidhihirisha sana
Ukimwambia mwanamke kila kitu leo, kesho utamuambia nini, zaidi utaishia kumdanganya. Au kumuonesha mwanamke upendo sana utampunguzia changamoto ya kukufukuzia na atakuona wewe wa kawaida.

Unachotakiwa kufanya ni kuacha mwanamke ajidhihirishe kwako mara mbili zaidi ya wewe unavyojidhihirisha, na usimfukuzie sana, ikiwemo kumwambia ‘nakupenda’, usitangulie wewe kusema. Jikumbushe pia mwanamke anayekupenda na anakufukuzia hawezi kukuacha, lakini mwanamke unayempenda na unamfukuzia anakuacha muda wowote!

Kutaka mahusiano zaidi ya mwanamke
Labda mmekutana mara mbili au tatu, lakini kadri unavozidi kumuona unazidi kumpenda, hutaki kumpoteza. Utajikuta unamsisitiza mahusiano/ndoa kiasi kwamba utamuogopesha. Ndio maana utasikia “Mimi sipo tayari kwa mahusiano sasa,” lakini kesho unamkuta na njemba mwingine.

Mwanamke akikwambia hayupo tayari kuwa na mahusiano, na unaona anakukubali ujue unamlazimisha mahusiano. Kiasi kwamba hajisikii amani na usalama kwenye hayo mahusiano.

Cha msingi wewe mtengenezee mazingira ya mahusiano, bila kumlazimisha kwa kutenga muda kwa ajili yenu, kumfanya afurahi na ajisikie usalama/amani kwako na kufanya naye mapenzi. Mpe muda atake mahusiano kwa kasi yake.

Mpe penzi zuri kitandani
Umeshamfanya ajisikie salama kwako, umempa nafasi ya kukupenda kwa kasi yake, na mwanamke amekuelewa, muongoze kitandani na umpe penzi ambalo hatolisahau kwa muda kidogo litamfanya atake kurudi kwako tena.

Ngono ni kitu muhimu kwenye mahusiano na ukifanye mapema kadri uwezavyo. Sawa unaweza kutaka na mwanamke anayekuchelewesha, hapo inabidi ujiulize we mwenye na uangalie kama misingi yako inaruhusu lakini hakikisha upo vizuri kitandani na unamfikisha na mwenzio.

Usifanye mahusiano yawe ya ngono tu
Sawa ngono ni muhimu, lakini ni vizuri mkatengeneza kumbukumbu mbalimbali za sehemu tofauti. Muda mwingine mnaweza msifanye mapenzi pia, ila sio kwa muda mrefu.

Usibweteke
Mwanamke akikupenda atataka muda wote muwe pamoja. Kubweteka kunaanza pale unapompa mwanamke muda mwingi zaidi ya anavyostahili. Utajikuta unapwaya sehemu zingine za maisha katika juhudi za kumridhisha mwanamke.

Lakini angalia usije ukabweteka sehemu zingine ili uwe na mwanamke. Jifunze kupanga ratiba. Ratiba itakayokupa muda wa kuendelea kufanya unavyotaka wakati huo huo utaweza kumridhisha mwanamke wako.

Kama ulikuwa mtu wa mazoezi usibweteke kwa ajili ya mwanamke. Kama ni mshabiki wa mpira usibweteke kwa ajili ya mwanamke. Kama una kazi/biashara usibweteke kwa ajili ya mwanamke. Kama ni mtu wa kujiendeleza usibweteke kwa ajili ya mwanamke.

Usiache uongozi
Mwanamke akikupenda kuna ka ushawishi cha kupunguza kasi. Kuna ka sauti “Mwanamke ameshanijua sasa hivi, acha nione anasemaje kuhusu hili/acha nione kama atafurahia hili/ngoja nimuulize kama anataka tutoke/ngoja nimuulize kama yupo tayari kwa ngono leo.”

Angalia usitumbukie humo. Uongozi uliokuwa nao kabla hajakupenda, ndio huo huo endeleza. Usibadilike na kutaka kumfurahisha kila muda.

Pia kumbuka, mwanzoni unaweza ukahisi unamjua huyo mwanamke sana, lakini sio kweli. Baada ya muda utagundua haukumjua vizuri. Baada ya uzuri na ubaya kujitokeza zaidi. Hivyo usikurupukie kuingia kwenye mahusiano sababu tu unampenda.
 
 
Nikweli kabisa lakini hayo yote ni kwa mwanamke anaekupenda sio unaempenda.

Unaanzaje kumtongoza mwanamke unaempenda bila kumtamkia "NAKUPENDA", yaani usimwambie 'nakupenda' unatongozaje sasa au unamwambia 'nakuhitaji'
 
Mwanamke kuhitaji umnaniliu, ni lazima ujiulize huenda ni malaya na asiyetosheka.
 
Back
Top Bottom