Mwakumbuka Gurubiti za kijiti cha chelewa, Mabumunda je?? Good Good je? mwakumbuka tulikuwa twala mapera kwa wingi sana??
Nakumbuka hizo enzi nasoma Lake Primary School - Isamilo na Nyanza Primary pia nilisoma jamani kaaaaa sijui kama mwalimu Tumbo yupo mpaka leo
lol! yaani umenichekesha sana! umenikumbusha mbali kweli hasa Gulibiti!! haha haa na enzi zile pipi tulikuwa tunaita peremende na chewing gum ilikuwa bazoka!!
Du wale waliosoma Wilolesi Iringa kwa Kajiba, enzi hizo kila J3 na Alhamisi kuna parade, ilikuwa shule ya kikakamavu! du kulikuwa na adhabu za kulowekwa kwenye pipa!! mh nahisi angefanya hivyo kwa sasa wangemtia ndani Mwl. Kajiba! Lakini alikuwa ni mwl maalumu kwa kurekebisha tabia! Ukumbukwe mwl Kajiba popote ulipo nakupa heshima yako!
Nakumbuka asubuhi unawahi namba, mkononi una fagio la chelewa, kidumu cha maji, mbolea, maua and sometimes panga, fyekeo au jembe! du enzi zi la full Kayumba tulikomaje? sio sasa hivi watoto wetu hawajui lolote!!!!