Enzi zile bwana

Enzi zile bwana

Shem shem shem.
Haya,ila wewe ulikuwa hujazaliwa na wala ki-embryo hujawa.

mie nimezaliwa kipindi hakuna soda, siku za sikukuu tulikua tunatengenezewa juisi ya malimao au machenza....
wali maharage ndio ilikua habari ya mjini...
kuku alikuwa haliwi mpaka azeeke, kama ni jogoo mpaka atage yai
 
Hahahaha
shem mbavu zangu jamami.
 
We Preta kweli!? mie zote nimepitia ukiongezea na kununuliwa nguo mwezi wa tano unazitunza hadi xmas, kuongeza maji kwenye soda ili isiishe, kuanika juani battery za radio ili zipate nguvu

Hii ya kuongeza maji kwenye soda Madame B kaifanya sana....
 
Last edited by a moderator:
mie nimezaliwa kipindi hakuna soda, siku za sikukuu tulikua tunatengenezewa juisi ya malimao au machenza....
wali maharage ndio ilikua habari ya mjini...
kuku alikuwa haliwi mpaka azeeke, kama ni jogoo mpaka atage yai

Blenda mlikuwa mnatumia kinu?
 
mademu wote chit chat lazima wataikumbuka hii HONGERA UMEVUNJA UNGO MJUKUU WANGU!
 
SIJUI KAMA SIKU HIZI IPO HII!
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili zisiishe
12.Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
13.Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Wewe unakumbuka nini...?
duh! u just made ma day
 
Watu nakumbuka enzi zilee mdogo wangu aliagizwa soda fanta 2 za wageni yeye akaleta moja.alafu akaifungua jikoni akaigawanya mara mbili akachanganya na maji akawaletea wageni mama kucheck hivi akaguna mmh hizi soda vipi hizi leo mbona imepauka rangi jamani kumbana vizuri akasema nimetia maji lol.
 
Back
Top Bottom