Enzi zile bwana

Enzi zile bwana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
SIJUI KAMA SIKU HIZI IPO HII!
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili zisiishe
12.Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
13.Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Wewe unakumbuka nini...?
 
11.
Ndala kuchemshwa ili zisiishe
12.Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
13.Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Wewe unakumbuka nini...?

hizo zote nimezipitia....ila hapo kwenye blue....ni pageni...
 
Mie nakumbuka kuvaa suruali za mchele mchele na shati la minazi wakati wa sikukuu...
 
dah... umenikumbusha mbali mkuu.... zote zinsnihudu isipokuwa na. 2... ila me nakumbuka tulikuwa tunaambiwa uking'oa jino unalitupa juu ya bati ili liwahi kuota... so hata ukiwa shule liking'ooka unalitunza unarudi nali home afu unalitupa juu ya bati......
 
daughter...ushawahi kucheza mchezo wa "Yanga yanga nipe kucha nyeupe"?
 
Ha ha ha hizo zote zinahusika sana ila hiyo 15 ndo imenikumbusha hasira yangu ya mwaka 197....nilipokuwa darasa la kwanza nilinyolewa msalaba wakati nywele zangu zilikuwa ndefu nikasusa kusuka mpaka leo nanyoa kipara
 
hahaaaa daddy... nishawahi sema nilikuwa mesahau kidogo... afu pia tukiona kunguru wengi wamekusanyika angani tunaanza kuimba "mvua njoo katalina njoo"!!!!!

hehehe....wale kunguru wenye vizibao, umenikumbusha mbali kweli ikifika jioni unakimbia kwenda kuogeshwa
 
....au kutoka nje na mfupa wa paja la kuku na chembechembe za ubwabwa kifuani.

Kuwaringishia wenzenu kuwa leo kwenu mmeuchapa ubweche.

kwa mwendo huu, we utakua kila ulipopewa soda unaiongezea maji kidogo ili iwe nyingi...
 
Ndege ikiwa inapita angani unakimbia kuchukua sindano na kuinyoshea ukiwa na imani kuwa kwa kufanya hivyo itadondoka
 
hizo zote nimezipitia....ila hapo kwenye blue....ni pageni...

We Preta kweli!? mie zote nimepitia ukiongezea na kununuliwa nguo mwezi wa tano unazitunza hadi xmas, kuongeza maji kwenye soda ili isiishe, kuanika juani battery za radio ili zipate nguvu
 
Last edited by a moderator:
•Ukiona albino unatemea mate kifuani kwa kuamini usipofanya hivyo mama yako naye atazaa zeru zeru
•Kutomsogelea mtu aliyedondokwa kwa ugonjwa wa kifafa kwa kuamini kwamba akij@mb@ na kuvuta ile harufu na wewe unapata kumbe lengo ni kumpa hewa ya kutosha ili awahi kuzinduka
 
Back
Top Bottom