Sikumbuki kitu.
Umeona eeh? Hasa wakati ule yule jamaa anaitwa Saleh Jabir alipotoa ile OPP ya kiswahili the Naught by nature wakatoa Hip Hop ree sijui hata sikumbuki jina lakeYaani wewe ulikuwa mtoto wakati ngoma ya OPP iko kwenye chati? Daaah ama kweli sasa wengine tumeanza kuzeeka lol.
Utakumbuka nini wakati ulikuwa bado kwenye diapers!:embarassed2:
Ningekumbuka hata kua kwenye diapers. . .
Haaa we si tulikuwa tunacheza wote KOMBOLELAAAAA! Yaani umesahau?
Ntachezaje kombolela na wazee mimi?
Au wewe ndo ulikua like fataki la mtaani kwetu? Maana lilikua linapenda kweli kukimbiza vibinti migombani.
Acha hizo wewe...hakuna mtu mzima anayekumbuka wakati akiwa kwenye diapers.
Na wewe migombani ulikuwa unatafuta nini?
Nlikua nachuma kahawa na kutungua maembe. . .
Chautundu wewe kumbe
Dah kama we enzi hizo ulikuwa kibinti basi we ndio mzee halafu nakumbuka ulikuwa unapenda kuniomba nikusindikize ukitumwa.......hahahhaaa we nae bhana eti ulikuwa unaogopa kuvuka kale ka mto ka pale njianiNtachezaje kombolela na wazee mimi?
Au wewe ndo ulikua like fataki la mtaani kwetu? Maana lilikua linapenda kweli kukimbiza vibinti migombani.
Dah kama we enzi hizo ulikuwa kibinti basi we ndio mzee halafu nakumbuka ulikuwa unapenda kuniomba nikusindikize ukitumwa.......hahahhaaa we nae bhana eti ulikuwa unaogopa kuvuka kale ka mto ka pale njiani
Mbona hata sikua mtundu?
Watundu ni wale waliokua wanakimbizwa na Jr hapo.
Dah unakumbuka zile nyimbo mlizokuwa mnaimba wakati mnavuta kokoro?Mimi niliyekulia kijijini wakati mwengine sitaki kukumbuka life ilivyokuwa tafu huku kijijini kwetu. ratiba ilikuwa kuamka saa kumi na moja alfajiri kwenda kutegua nyavu za samaki ziwani, sas ana kale kaubaridi ka asubuhi, ukitoka hapo na manyavu yako pamoja na samaki wako waliopatikana ni kwenda shambani mpaka saa tisa ndo upate ugali wako wa mhogo na sato fresh ama san! Kale kalikuwa kajela aisee japo kamenifundisha maisha