WATINDI mashetani,
Tena mapunguani,
Wana kasoro kichwani,
Naam tundu rasini,
Wanazua tafrani,
Nchi yakosa amani.
Wa kumuogopa nani?
Yehova ama shetani?
Waloizua tafrani,
Mbinguni na duniani,
Watu hawaelewani,
Asama upunguani.
Kinga yangu Rahmani,
Mola wa mashetani,
Mlezi wangu Manani,
Mola wa waumini,
Hivi kaumbwa na nani?
Ibilisi maluuni.
Vilivyopo duniani,
Muumba wake Manani,
Hata huno ushetani,
Muumba wake Manani,
WATINDI mashetani,
Kiboko yao Manani.
Tahadhari ni thamani,
Ni lazima si utani,
Palipo kosa amani,
Na subira nafsini,
Tuishipo nakamani,
Tahadhari kibindoni.
Njano5.
0784845394