Enzi za Mwalimu - Tupia yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za Mwalimu - Tupia yako

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rubi, Oct 2, 2012.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Tupia yako unayokumbuka enzi za Mwalimu

  enzi za mwalimu


  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Rubi , enzi za mwalimu kuna mambo mengi sana. Nakumbuka juu ya maduka ya kaya. Kununua bidhaa kwa foleni. Bidhaa zenyewe adimu, hivyo ikipatikana lazima itunzwe na itumiwe kwa uangalifu. Nakumbuka siku moja wakati nikiwa mdogo baba yangu alinikuta nalamba sukari ambayo alisota sana mpaka kuipata. Nilichapwa viboko ambavyo navikumbuka mpaka leo, miaka mingi ikiwa imepita.
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  enzi za mwalimu
  wananchi tulikuwa 15m tulisoma kutibiwa bureee na kupewa chakula hasa nyakati za matatizo kama ya njaa bureeee na serikali ilikuwa haina hata muwekezaji mmoja.
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pia kalamu, rula na madaftari 12 tulikuwa tunagawiwa shule siku mnapofungua shule pamoja na mikebe.

  Na bado kulikuwa kuna zawadi za washindi wanaofanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.
  - kulikuwa na ngoma za shule, mchakamchaka, gwaride la shule, somo la sayansikimu tulikuwa tunafanya kwa vitendo yaaani tunapika na kula shule.

  - Tulikuwa tunakaguliwa nguo za ndani kila alhamisi kwa shuleni kwetu hasa darasa la kwanza mpaka la nne au la tano. enzi za mwalimu raha.
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Enzi za mwalimu ukisikia Mwalimu (Rais) anakuja kwenye mkoa wenu siku hiyo ni kujipanga barabarani kuimba na kupiga makofi kila anapopita maana kazi zote zinasimama kwa muda mpaka apite.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mimi nakumbuka daftari likiisha teacher anakusignia unaenda kuchukua daftari lingine!
  Zile zama achana nazo kabisa
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wafanyakazi walifanya kazi kwa moyo na kwa bidii,pia askari alikua ni mtu tayari mda wote mkakamavu zaidi
   
 8. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pia Watanzania tulikuwa tunapendana sana na kuaminiana kiasi kwamba ilikuwa sio shida kumkaribisha mtu aliyepotea kulala nyumbani kwako bila tatizo mpaka atakapompata mwenyeji wake.

  Siku hizi mtu usiyemjua sio rahisi kumkaribisha nyumbani kwako maana si salama tena.
   
 9. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Enzi za mwalimu....Tulikua tunasimuliana kuwa askari wa kenya anaogopwa na raia kama ukoma huku kwetu ni askari ni ndugu,rafiki na msaada wa karibu ukipata shida. Siku hizi dah ulimwengu umepinduka kichwa chini miguu juu.
   
Loading...