Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,131
Nimekumbuka jambo, siku moja jeshi la polisi walikuja Ruvu JKT kuwasaili vijana ili wawaajiri. Vijana walijitokeza kama tu kujaribu zari lao huku wengine wakijisemea kuna la kesho na keshokutwa. Kuna vijana madoja wakubwa wa shamba ile siku walijipeleka shamba wenyewe ili tu wasifanye usaili wa Polisi.
Kule zamani kijana ukitokea mtaani unasema ikitokea kazi yoyote utakuwa tayari kufanya cha ajabu ukimaliza tu six week unaanza kuchagua kazi. Kazi kama ya Upolisi, Zimamoto na Magereza walikuwa wanaenda watu wenye vyeti vya kuungaunga, wenye miili yenye excuse au vijana wanaokaribia kumaliza mikataba yao ya miaka 2.
Siku hizi dunia iko kasi, hata mgambo wa Jiji wakienda Ruvu JKT kuhitaji nguvu kazi vijana watapigana vikumbo kugombea hizo nafasi.