Mwembebasha
JF-Expert Member
- Dec 27, 2013
- 1,424
- 406
Yaani nimejaribu kuvuta picha ya hili tukio nimecheka mpaka mbavu zinauma!!!Nakumbuka kuna mlinzi aliwahi ona bundi akajua simba basi akaja kutangaza kua kuna simba alikua ni mmasai .Mimi nilikua napenda kutoroka kwenda kijijini na washkaji siku moja niliwauliza wana zengo kua huku kuna simba wakasema ni bundi wakubwa tu.Basi ulipita kama mwezi siku moja nilikua natoka prepo ile mida ya saa za wasongo kama saa nane usiku hivi nilikua nakimbia kwa korido kuna jamaa akatokea mbele yangu alikua anaenda kunawa uso ili akasome akaniuliza unakimbia nini?Nikajibu simba!Aisee yule jamaa alitupa maji na kukimbilia domitory na kuanza kulia simbaaaaaaa!Shule nzima ilikimbizana yule mlinzi ndio usiseme!Basi madom yetu yalikua na kenchi yaani watu walininginia kama popo ili simba aiwangate!Kuja kuja kama wameuzwa walikua wame umia vibaya aisee members wa mkandawile mpo hapa???
Kwa wale waliosoma tanga tech kwa kamanda TETI the headmaster,mi nilisoma advance pale nikiishi bweni la TWIGA.Nakumbuka zile siku za wali a.k.a punje a.k.a chakula cha binadamu tulikuwa tunajiandaa kama unakwenda vitani,unapiga raba,jeans na t-shirt then unajipanga kwa foleni.Mgawaji anapokugawia,huangalii sahani,unamuangalia usoni kwa jazba yaani shari tupu.
Nakumbukuka niko sec Siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na Ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.
siku moja tosamaganga tuko bwaloni kaja jamaa mmoja fm4 amechelewa msosi ameukosa basi kaja kwenye meza yetu kachukua msosi wangu kaweka kwenye sahani yake then kasepa mi kumfuatilia kanizaba kibao. nlilala na njaa siku ile hata sisahau
ahahahahah....enzi hizo Tabora boyz..kulikuwa na chemba moja katika bweni la mkwawa inaitwa university..mle tulikuwa tunalala pipo kama kumi na moja hivi tukiwemo viongozi..mke wa headmasta jina la utan nyumelo alikuwa na tabia ya kuja kutuamsha asubuh na mapema mabwenini..siku hiyo kaja kakuta pipo zote zimelala naked chemban coz tulipanga tumkomoe...ahahah yule mama eti akasema wala hatishiki coz keshaona kubwa zaidi ya zetu..mwee..but atleast alipunguza kuja akawa anaishia bweni kuu...vituko vya mesini hasa siku za nyali aka ubwabwa we acha tu..
Umenikumbusha vyoo vya nje maarufu kama Half Mile, hivyo vyoo vipo umbali wa zaidi ya mita mia mbili. Kufanyiwa usafi kwake ni mpaka mwanafunzi akamatwe na kosa ndio akafanye usafi, sasa pata picha ya harufu ya mchanganyiko wa maharage yasiyo na viungo + bondo jeusi harufu ikoje...
Wale Alumna wa Tosamaganga High School watakumbuka ile staili tuliyokuwa tunatumia kwenda kulenga shabaha pindi ikitokea maji yamekatika kwenye vyoo vya ndani vya kuvuta.
Unavua shati na suruali mbali unabakiza bukta au chupi tu ndiyo unaingia Half mile vinginevyo ukirudi darasani watu watakukimbia kwa harufu.