Tunapoelekea kufikisha miaka 50 tangu Uhuru wa Nchi hii, hebu tukumbushane matukio/jambo/suala/picha/kituko/vimbwanga iwe katika nyanja ya Burudani, Starehe, Michezo, kijamii ambayo kwa akili ya kawaida ni Nadra kuyaona yakifanyika sasa hivi katika Dunia ya sasa ya Utandawazi.
Ngoja Nichokoze: Enzi hizo nakumbuka kuna watu walikuwa wanarekodi katika mikanda(Tape) mechi za Simba na Yanga zilizokuwa zinarushwa Live na Redio Tanzania(RTD), nadhani kwa lengo la kuziuza, au kukumbushia kusikiliza.
Enzi hizo za watangazaji mpira kama Abuubakar Lyongo, Sued Mwinyi....n.k
Kwa akili ya kawaida, sidhani kama kuna anayefanya hivyo sasa hivi...