Enzi Hizo: Hii ndio ilikuwa Mbeya bwana

Enzi Hizo: Hii ndio ilikuwa Mbeya bwana

chaUkucha

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
3,382
Reaction score
1,222
1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa kiswele....engine nyuma, Dar - Mbeya faster, mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya ukweli, usisahau MV Saratoga, tunyande bus service, zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa kama watano hivi, wachafuuu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. Kiwanja ngoma hapa soka lilipigwa buana timu yangu ya mtaa snow white chini ya key, kina baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry kichaa alikuwa na alergy na watu weupe akikuotea atakukimbiza na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa kama makao makuu ya vichaa walikuwa kibao.

6. Pale Bomani palikuwa na mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna, nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

7. Kipindi hicho Disco lilikuwa mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa wasape na Sugu - 2 proud, Hip hop ilinoga buana.

8. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi wa sinema pale opposite na ofisi za posta Town movie la Hatya lilifunika sana enzi zile.

9. Miaka ile buana mvua ilikuwa inapiga kama gharika, sometimes ilikuwa inamwaga barafu kama ulaya, mlima loleza ulikuwa ukifunikwa na theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina shake.

10. Siku ya jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa, mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale mifugo, nyuma ya kanisa la Roman, mkisha maliza kuogesha mnaanza kugombanisha mbwa, mbwa wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na wa kienyeji iliaminika wana nguvu balaa.

11. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali, watoto walikuwa wanatoka maeneo tofauti ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi, man'gan'ga, mafyulizi, mapohora, mapera nk.

12. Mwanjelwa enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii mitumba viwango, raba kali, msela ukitupia vya doksi umemaliza.

13. Enzi zile ukisoma sisimba na Azimio unafunika. Shule ya international ilikuwa umoja primary school. Waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa.
 
5cd10d1bdaca2ed723675c83a3c87451.jpg
 
Mwanjelwa kulikuwa na mbabe wa mby mtemi Daudi Masoke
 
Jombi alifariki inasemekana mpaka usalama walikuwa wanamuogopa jamaa alikuwa noma.
 
Namba 1 hapo....Mimi nishakutana naye physical nakumbuka alijuwa na garage hapo soweto na alikuwa anatumia range enzi hzo...
Wakati msela mm nlikuwa napiga Mishe ya utingo----kwenye chai maharage ambayo ilikuwa inamilikiwa na mhandisi mmmja wa ndege alikuwa anafanya kazi Libya baada kuwekewa kizuizi na umoja wa mataifa aliamuakkrudi tz na alikuwa anaishi mbeya alintoa dar kwenda mbeya wakati huo nlikuwa chaliiii Mdg sana .....
2.nakumbuka mbeya kwenda beach Sisi tulijiwa tnakwenda mtoni ....unapitaaa bkok t ....eland hotel mbele kulikiwa na mto watu weknd kama wako coco....
3.shule za wajanja na watemi zilikiwa sangu na meta......nishaleteana nao sana kwenye chai maharage.......coaster Saratoga dereva yule aliwakanyaga sana mabint wanafunzi nakumbka....

Mleta uzi umenikumbisha mbali sana khsu mbeya........

Ova
 
Kulikua na kibaka Jairo simike mtaalam baraa, bila kumsahau chande kwenye palinge utakoma. Semeni nzovwe mtoto wa kalongoti alikua balaa.ukoo wa kibo nzovwe nao wamo sijui waliishia wapi acha kina mwamajuja
 
Umemsahau kichaa mmoha aliitwa melele,timu zingine.za kiwanjangoma kama saitama,blacktown,jogoobasha,blackstar,ghana timu ya nyumbani,
 
Back
Top Bottom