1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie mimi ni "Jombi"
2. Kulikuwa na basi zinaitwa kiswele....engine nyuma, Dar - Mbeya faster, mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya ukweli, usisahau MV Saratoga, tunyande bus service, zainabus
3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa kama watano hivi, wachafuuu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.
4. Kiwanja ngoma hapa soka lilipigwa buana timu yangu ya mtaa snow white chini ya key, kina baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya flames.
5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry kichaa alikuwa na alergy na watu weupe akikuotea atakukimbiza na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa kama makao makuu ya vichaa walikuwa kibao.
6. Pale Bomani palikuwa na mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna, nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.
7. Kipindi hicho Disco lilikuwa mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa wasape na Sugu - 2 proud, Hip hop ilinoga buana.
8. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi wa sinema pale opposite na ofisi za posta Town movie la Hatya lilifunika sana enzi zile.
9. Miaka ile buana mvua ilikuwa inapiga kama gharika, sometimes ilikuwa inamwaga barafu kama ulaya, mlima loleza ulikuwa ukifunikwa na theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina shake.
10. Siku ya jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa, mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale mifugo, nyuma ya kanisa la Roman, mkisha maliza kuogesha mnaanza kugombanisha mbwa, mbwa wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na wa kienyeji iliaminika wana nguvu balaa.
11. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali, watoto walikuwa wanatoka maeneo tofauti ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi, man'gan'ga, mafyulizi, mapohora, mapera nk.
12. Mwanjelwa enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii mitumba viwango, raba kali, msela ukitupia vya doksi umemaliza.
13. Enzi zile ukisoma sisimba na Azimio unafunika. Shule ya international ilikuwa umoja primary school. Waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa.