Enzi Hizo: Hii ndio ilikuwa Mbeya bwana

Enzi Hizo: Hii ndio ilikuwa Mbeya bwana

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa kiswele....engine nyuma, Dar - Mbeya faster, mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya ukweli, usisahau MV Saratoga, tunyande bus service, zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa kama watano hivi, wachafuuu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. Kiwanja ngoma hapa soka lilipigwa buana timu yangu ya mtaa snow white chini ya key, kina baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry kichaa alikuwa na alergy na watu weupe akikuotea atakukimbiza na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa kama makao makuu ya vichaa walikuwa kibao.

6. Pale Bomani palikuwa na mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna, nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

7. Kipindi hicho Disco lilikuwa mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa wasape na Sugu - 2 proud, Hip hop ilinoga buana.

8. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi wa sinema pale opposite na ofisi za posta Town movie la Hatya lilifunika sana enzi zile.

9. Miaka ile buana mvua ilikuwa inapiga kama gharika, sometimes ilikuwa inamwaga barafu kama ulaya, mlima loleza ulikuwa ukifunikwa na theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina shake.

10. Siku ya jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa, mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale mifugo, nyuma ya kanisa la Roman, mkisha maliza kuogesha mnaanza kugombanisha mbwa, mbwa wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na wa kienyeji iliaminika wana nguvu balaa.

11. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali, watoto walikuwa wanatoka maeneo tofauti ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi, man'gan'ga, mafyulizi, mapohora, mapera nk.

12. Mwanjelwa enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii mitumba viwango, raba kali, msela ukitupia vya doksi umemaliza.

13. Enzi zile ukisoma sisimba na Azimio unafunika. Shule ya international ilikuwa umoja primary school. Waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa.
Hivi usafiri wa mjini, soko matola, mwanjerwa, uyole, iyunga na mbalizi bado unaitwa mzunguko?
 
Namba 1 hapo....Mimi nishakutana naye physical nakumbuka alijuwa na garage hapo soweto na alikuwa anatumia range enzi hzo...
Wakati msela mm nlikuwa napiga Mishe ya utingo----kwenye chai maharage ambayo ilikuwa inamilikiwa na mhandisi mmmja wa ndege alikuwa anafanya kazi Libya baada kuwekewa kizuizi na umoja wa mataifa aliamuakkrudi tz na alikuwa anaishi mbeya alintoa dar kwenda mbeya wakati huo nlikuwa chaliiii Mdg sana .....
2.nakumbuka mbeya kwenda beach Sisi tulijiwa tnakwenda mtoni ....unapitaaa bkok t ....eland hotel mbele kulikiwa na mto watu weknd kama wako coco....
3.shule za wajanja na watemi zilikiwa sangu na meta......nishaleteana nao sana kwenye chai maharage.......coaster Saratoga dereva yule aliwakanyaga sana mabint wanafunzi nakumbka....

Mleta uzi umenikumbisha mbali sana khsu mbeya........

Ova
unaitwa Mto nzovwe au kwa kayoyo
 
Kwa airport ya zamani namkumbuka Malafyale, alikuwa mlokole hivi biashara yake ilikuwa kuchoma mahindi pale kwenye geti la chuo cha uhasibu baadae akili zikafyatuka, bila kumsahau mzee Athman, huyu mzee alikuwa mganga asili yake ni songea alikuwa na watoto wengi kwa upande wa kiume mwanae mkubwa alikuwa IDD na wa kike Rukia. Sasa mkute mzee Athman kambeba mkewe kipenzi mama Rukia kwenye baiskeli yake ya foot brake utampenda kwa machejo. Kipindi hicho na masela wangu akiwemo Karama Nyirawila tunashinda kwenye fensi ya Mwaisango Bar & guest house (opposite) na nyumba ya kina Karama kucheza kamari ya vishikizo vya nguo almaarufu vindeti. Xmas au mwaka mpya tunapanda mafegi hadi soko matola kwenda kula maandazi na soda ndio ilikuwa hitimisho ya matembezi yetu.
Miss sana zamani!
Mkuu jitambulishe tu...Maana hao wote nawafahamu aiseee.......
 
Tukuyu stars - mabingwa Tanzania bara 1986
Kevin Haule, Hussein Zito, Karabi Mrisho, Godwin Aswile, Ally Kimwaga, Danford Ngesi, Mbwana Makata,Athuman Juma,
Fadhili Hembe, Richard Lumumba, Yusuf Kamba, Selemani Matthewa, John Alex, Daniel Chundu, Aston Pardon.
 
Njelii maskani kitambo, docksi, shule ya msingi mamga na sinde zote nimezigusa, kipindi hicho mitihani kila jumamosi mpaka unapenda, kula chipsi kwa sandima makunguru kabla soko halijabomolewa. Now Mbeya imebadilika cause kipindi hicho kuna sehemu hupiti for no reason. Remember kipindi hicho uwanja ngoma ilikua shida, uchawi mpirani umetapakaa. MTU anadaka jiwe. Si tunaona mpira kumbe style za shaolin soccer. Mbeya city, tumekua watu wazima sasa life goes on. Iyunga kitambo loleza sweeters.
 
Wale ndo walikuwa wababe. Sio hawa wa siku hizi akiwika wiki tu kwishney. Tulikuwa tunawaogopa mpaka wadogo zake pale kiwira ukikorofishana naye anakutishia "we hujui mimi mdogo wake Jombi eeeeh?" aaaah unagwaya hata akikupiga hurudishii[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hahaha kweli

Ova
 
Ukifika Sokomatola palikuwa na George's Rombo Bar ya Mzee George jirani na ilipokuwa Friends Corner Bar, hapo ilikuwa nyamachoma ya Mbuzi balaa!!!
 
Alinaali,Uswahilini matola,Ndapo,Nashangaa gari,Air japanis,Shazias,Vamponji,Lupata,Kipoke,Daaa Mbeya bwana kitambo sanaa
 
Back
Top Bottom