Enyi waume ishini na wake zenu kwa akili

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Pengine usipokuwa makini huwezi kujua iwapo ninyi wawili (Mke na Mume) ni mwili mmoja.

Mke ana kazi nzuri na mume nae mungu kamjali. wote mna msahhara ambao unalingana kama si kukaribia. (Asante Mungu), mwisho wa mwezi umefika, japo mlipanga mwanzoni mwa mwezi mambo ya kufanya, mwenzio anakueleza kuwa yeye mshahara wake tayari ana deni kwa fundi nguo (ni sare ya harusi ya mdogo wa rafiki yake), anadaiwa saloon, anadaiwa michango ya send off ya rafiki yake (hiyo huwezi kumlipia, hamkupanga) na amemtumia mama nyumbani kiasi na amepanga kutoa sadaka Fungu la Kumi. Umekwishaaa....

Unastuka, "ehee vipi mbona hatuambizani kabla?"

Anakujibu: "lakini kama mimi singekuwa na kazi usingenilisha, usingenivisha, usingeninywesha??..we kiacha wenzio watanigharimia!!!"

mh. unatafakari , mwezi uliopita mliingia kwenye malumbano, mlileta msichana wa kazi wa kwanza akasema amfai, anajeuri,anamjibu hovyo, akamleta mwingine, akaka siku mbili akasema sio msafi, mwingine alikaa wiki anasema hajui kusoma atawaharibu watoto, akaleta mwingine "Mzimbabwe" ambae mshahara wake ni mkubwa sana lakini hakuhusisha mpaka wakati wa kumlipa.

Anakuambia: " Leo Dada anadai mshahara wake..,

Ulipouliza: " kwani ngapi??",

Anajibu " Huyu ni laki na nusu tu ni Mzimbabwe na mchapakazi mzuri, nimempenda"..

Unashtuka ..."mh. mbona wapo wengi wa hamsini kwa nini hivyo?"

Anajibu: "hao wa hamsini ndio wakorofi!!, mimi siwezi labda ukae nao wewe"

Tunalipaje?? imekula kwako hiyo...

Pango la Nyumba Tshs. 250,000 (kwa mwezi)

Umeme 50,000 (kwa mwezi)
Mafuta ya gari 20,000 (kwa siku)
Hela ya chakula 20,000 ( kwa siku)
Bili ya Maji 30,000 (kwa mwezi)
Gesi 58,000 (mtungi kwa mwezi)
Bado hujala ofisini, hujanywa, hujatoa michango kwenye shughuli za kijamii nk. ONgeza na 150, 000 ya binti wa kazi za ndani!!! Kudadadeki! + Ada ya watoto wawili 880, 0000 (kwa term).

Toa kwenye Mshahara wako ambao hauzidi Tshs. 700,000 kwa mwezi (take home).Jumlisha majukumu ya familia ya pande zote mbili (yako na Mkeo) + Vidonga vya tumbo + ka Presha kwa mbali!!

Ikifikia hapo tambua Wewe Mume ni kichwa cha nyumba, ishi na Mkeo kwa Akili. Msigombane, mpatane, chukua nafasi yako, timiza wajibu wako, acha maisha yaende mbele...ukipata wasaa mkanyane..
 
mmh, iko kazi... si afadhali uoe housewife tu ujue moja kuliko huyo 'mfanyakazi' ambaye kipato chake hakina mchango wowote ndani ya nyumba
 
20000 ya chakula nyumbani kila siku?
Hiyo familia ni ya wazembe!!!

Ngapi, hapo ndio kiwango Lizzy!! kwa bei ya nyama kilo 5500, samaki 6500,ndizi tattu 500, fungu la mchicha fungu 300-500, maharagwe 2200, unga kilo 1200, mchele kilo 2300, maji ya kunywa 1500 (1.5 litre), mkate 1200- 1500, sukari 2200, majani ya chai, nk nk...Hujahesabu idadi ya wakaazi
 
mmh, iko kazi... si afadhali uone housewife tu ujue moja kuliko huyo 'mfanyakazi' ambaye kipato chake hakina mchango wowote ndani ya nyumba

Kama mnapata hadi za bajeti ya kwenda kuhonga nyumba ndogo na kuweka heshima bar kupitiliza.........kwanini msifanyiwe hivyo??
 
ukichanganya na deni la mahari, na mkwe anakuulizia kila inapofika tarehe za mwisho wa mwezi aaahhhh usingizi haushuki kabisaaa
 
it serves nothing kukomoana... kuna umuhimu wa akina mama nao kuonyesha a sense of responsibility ndani ya familia

Ndio visa vyenyewe hivyo, na kichwa cha nyuma ukifa mwelekeo kwa muda unakuwa KWISHNE>.. wanajipanga upya!!
 
it serves nothing kukomoana... kuna umuhimu wa akina mama nao kuonyesha a sense of responsibility ndani ya familia

Mie sijakataa akina mama kuwa resiponsible na familia zao, ila kuna wanaume wengine wanadeserve kabisaa kutokana na mambo kama hayo hapo, na vilevile wengine mnawazoesha wenyewe!!
 
Ngapi, hapo ndio kiwango Lizzy!! kwa bei ya nyama kilo 5500, samaki 6500,ndizi tattu 500, fungu la mchicha fungu 300-500, maharagwe 2200, unga kilo 1200, mchele kilo 2300, maji ya kunywa 1500 (1.5 litre), mkate 1200- 1500, sukari 2200, majani ya chai, nk nk...Hujahesabu idadi ya wakaazi

Ngoswe hapa nilipo kuna watu wazima watano na watoto wawili wadogo wadogo.

Matumizi. . .
Nyama kg 1- 5500 (inatumika mara mbili kwasababu kuna mboga nyingine . . .maharage/mboga za majani na hamna anaenyosha kupunjika vinyago).
Mchele kg 1 - 2300 (mlo mmoja na kiporo cha watoto kinabaki. . hapo kila mtu anajipakulia na kuongeza wakitaka hivyo hamna kusema labda watu hawashibi).
Mboga za majani 1000 (zinalika mara mbili)
Matunda ya 1000 (parachichi/ndizi/embe. . .mchana na jioni)
Mafuta ya kupikia 500 milo yote
Nyanya za 500
Carrot, hoho, bamia 500
Unga wa ugali kg 1 - 1800

Mpaka hapo imetumika 12,600 tena kwa kununua vitu kila siku which we don't do. Kitu kinachonunuliwa siku husika ni nyanya pekee. Kwa maana hiyo hatuwezi kutumia zaidi ya sh. 10000 kwa milo yote pamoja na chai.

Waambie wanunue vitu vya jumla (mchele, unga, mafuta, maharage, vitunguu vinakaa sana, viazi, carrot, nyanya ni kiasi cha kuchagua ambazo hazijaiva sana n.k).
 
Lizzy haya mwengine tunaambiwa, hela ya kula kiasi kadhaaa...ukipiga hesabu wewe mwenyewe una kula 10,000 kwa siku, unafikiria watu watano haitoshi hta 15,000.
May be kuna panga linatembea hapo, ukiacha kwa mama (mwanamke) anampa msichana wa kazi (mwanamke mwenzie) aweke mipango ya menyu ya siku.

Ndio maaana tunaambiwa "tuishi na wake zetu kwa akili", (wana akili zaidi yetu) na kwa upane wao wanaambiwa "watupende" kama Kristo alivyolipenda kanisa.
 
Sasa huko ni kukomoana. Vile vitu visivyoharibika ni vizuri vikanunuliwa kwa jumla. . .yani kwa siku mtu akiacha 10000 nyumbani ibaki chenji si chini ya sh. 3000.

Mie ningekua hao wamama wanaochiwa 20 000 kila siku mbona ningesha-save kamtaji ka kishkaji. 10000 kila siku. . kwa wiki 70 000. Mwezi mzima naweka walau 250 000. Siku mwenzangu akiniambia mambo hayaeleweki namwambia usijali kuna kapesa nimekaficha sehemu. . mwenyewe atashagaa.

Ila hiyo ni kama hamuishi maisha ya kukomoana.
 
daah iyo kali, ila wapo pia wanaume pasua kichwa maana anataka alelewe na mkewe wakat na yeye kazi na mshahara mzur anapata ila kuonga anajua
 
Unaweza ukaishi nao kwa akili na wakakutia changa la macho vile vile heehehe hawa viumbe wanazaliwa na phd zao sisi mpaka tuende shule

Sasa jifanyeni kubisha muone nitakavyowalipua
 
Sasa huko ni kukomoana. Vile vitu visivyoharibika ni vizuri vikanunuliwa kwa jumla. . .yani kwa siku mtu akiacha 10000 nyumbani ibaki chenji si chini ya sh. 3000.

Mie ningekua hao wamama wanaochiwa 20 000 kila siku mbona ningesha-save kamtaji ka kishkaji. 10000 kila siku. . kwa wiki 70 000. Mwezi mzima naweka walau 250 000. Siku mwenzangu akiniambia mambo hayaeleweki namwambia usijali kuna kapesa nimekaficha sehemu. . mwenyewe atashagaa.

Ila hiyo ni kama hamuishi maisha ya kukomoana.

Watanzania wachache sana wanaoishi maisha halisi, wengi ni maumivu yenye kuhitaji msaada. Hata kama una msahara wa 1M take home kama si fisadi, masiha ni magumu sana. Ukipiga hesabu kama kila siku unaacha hela ya kula nyumbani 10,000 kwa mwezi inakuwa 300,000 + 20,000 ya mafuta kwa siku = 600,000 kwa mwezi + 5,000 ya chakula yako kwa siku = 150,000 kwa mwezi + 5,000 vocha = 150,000 kwa mwezi,
 
Sasa na wewe. . . kama mtu pesa yake yenyewe ya kulenga kwa manati gari ya kazi gani? Si apande daladala/boda au hata bajaj?

Maana kama mtu atatumia zaidi ya nusu ya mshahara (600 000/1000 000) kwenye kununua mafuta tuu, basi hatumii akili. Yani mpaka hapo yeye hajatumia akili ku-minimize cost ila yeye anaweza taka mke nyumbani afanye hivyo. . .aiseee hiyo hapana.

Kama ni akili ya kupanga matumizi yapaswa muwe nayo wote au mfundishane, otherwise hamna la maana mtakalokaa mfanye.
 
hayo matumizi yako yako juu sana, wanawake wanapaswa kusaidia pia lakini wanaume ndio wahusika wakuu. mnafikiri mlivyoitwa vicha ni urembo? mnapaswa kuwakilisha, msipowajibika kwenye familia zenu mtawajibika kwenye nyumba ndogo? siku nzote furaha ya mke na watoto huleta baraka kwa baba.
 
Back
Top Bottom