Enyi wanawake!!!

M.E.M.A

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
1,373
Reaction score
472
Hili tangazo la CRDB, mama anamwambia mwanae akavae kwanza suruali, '..tena ile ninayoipenda..'.
Natafakari: Mama is so concerned kijana wake 'atatokelezeaje', pili she even has her 'favourite' Son's trousers. Imagine the son marrying a woman who can't match the Son's mother concerns about him, isn't it sufficient to conclude that the marriage would likely 'feel' inadequate to the Son somehow? Isn't that an avenue for 'restlessness', 'inner hunger' that leads to 'extra marital' affairs - a son's self quest for something he is accustomed to having all his life but don't have now'?

Nimekumbuka mtu mmoja kwenye semina moja..alisema "kijana wa kiume mwanamke wa kwanza kukutana naye maishani ni mama yake. Anajifunza upendo wa mwanamke kupitia kwa mama yake, na quality na picha ya mwanamke maishani mwake huwa na reference kwa mama". Naamini ni sahihi kabisa..maana nimewahi kusikia kijana akisema..'mimi nikiwa mkubwa nataka nimuoe mama'!!? Sasa tatizo litakuwa pale atakapopata mismatch ya mama yake kwa kweli ndoa italack something.

Mwisho..sehemu kubwa ya mama wakwe hawaivi na wakwe zao (wake) kwa kuwa mama anaona mwanae anakuwa mistreated.

Haya wadada/wanawake humu, mnazijua favourites za wanaume zenu? Kama hamzijui basi cheating itaendelea hadi mtu apate mahali ambapo kuna chembechembe za 'mama'.

"Mimi namuomba Mungu anipatie mke mwenye quality za mama yangu."
 
unaweza kuwa sawa kwa upande fulani hasa upande wa wanaume kupenda wake zoa kuwa na sifa za mama zao hasa kama zinavutia kwani the same thing applies to watoto wa kike,ila hapo kwenye nyekundu hapo mkuu ndipo ulipoingia chaka,nikianza na nyekundu ya kwanza,


'restlessness', 'inner hunger' that leads to 'extra marital' affairs
hiki ni kisingizio tu cha kuwa na extra marital affairs,kwani uchumba maanake nini?huo ndio wakati wa kijana kujua ikiwa mke wake ana sifa kama za mama au la,ukiona hana na ungependa awe nazo basi unamtafuta aliye na sifa hizo uzitakazo,lakini kuoa tu na kuamua kuwa na intruders in your marriage ni tatizo lako we mwenyewe binafsi.


Haya wadada/wanawake humu, mnazijua favourites za wanaume zenu? Kama hamzijui basi cheating itaendelea hadi mtu apate mahali ambapo kuna chembechembe za 'mama'. hapa pia huo si ukweli kwamba men are cheating kwa sababu wake zao hawana characters za mama zao,wengine wake zao wana characters nzuri zaidi ya mama zao lakini ndo hivo bado atacheat tu,so hiyo ni tabia ya mtu tu.

Na pia je kama mama alikuwa mcharuko sana bado mume atataka mke awe na sifa kama za mama?
 
i wish that very much but i dont see kama my wife is an image of my mother, Maybe she is, that's why i cant see!

[MENTION]CC;Heaven on Earth,Preta,LadyFuraha[/MENTION]
 
Katika hilo tangazo, je uliweza kung'amua umri wa kijana wa kiume ni upi?

Maana kuna umri ambao binti au kijana huwa chini ya uangalizi wa mzazi (mama) kwani huo ndio wajibu wa mama kwa wakti huo...

Suala la kuchaguliwa nguo katika umri huo si la kushangaza kwa kuwa mtoto anakuwa hajapevuka akili ya kufanya maamuzi binafsi yaliyo sahihi...

Ukiweza kutoa jibu la swali pale juu, nadhani ndipo nitajua kuwa hoja yako ina mashiko au lah!!!
 
Mimi najua kila jambo lina faida na hasara, mimi ningependa kweli mke wangu awe kama mama yangu karibia vitu vingi sana, hiii ni pamoja na muonekano mpaka upole wake! lakini nisingependa awe kama mimi kwa baadhi ya mambo! huo ni mfano wangu! lakini wapo watu mkuu angependa mke wake bora awe na tabia zake kuliko mama yake kwa namna mama yake alivyo! hivyo unapooa mke haji kumlidhisha mama yako ila wewe xo ni vema mkiamua kuwa pamoja basi mwambie mwenzio kuwa nini unapenda na nini hupendi naye afanye hivyo ili! kama unaona mashariti yake magumu asikushawishi kwa kusema basi hilo ntavumilia upendo kuna wakati unachuja xo at that level uvumilivu huwa hakuna mtu anatafuta weakness tu better kuwa smart mapema kwa kila analotamka toka kinywani mwake maana alinenalo mtu ndilo awazalo na analo waza ndilo atendalo!
 

Mkuu unganisha point moja na nyingine. Mwanamke wa kwanza mtoto wa kiume kukutana naye ni mama yake mzazi. Kwamba ni mcharuko au yupoje yupoje bado ni mama yake na ana mazuri yake.

Kuhusu cheating..hebu niambie kuna cheating inayofanyika bila visingizio au justifications. ?
 

Ulipokuwa unakojoa kitandani ulipewa karipio liwe viboko au vinginevyo..na mpaka leo unafahamu kukojoa kitandani sio staha.

Hata biblia inasema "mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee". Ninachotaka kusema ni kwamba kile ulichofundishwa au jinsi ulivyokuwa treated kina impact endelevu katika maisha ya mtu. Wewe hapo leo ukiambiwa "baby hili shati silipendi, vua vaa lile pale"....unavua tena huku unachekacheka, je tuseme hujapevuka akili???
 
mkuu kuna mama wengine wana gubu mpaka mtoto mwenyewe anakubali kuwa jamani mi mwenzenu mama yangu acheni tu naomba wife asiwe hivi jamani,si wote wanaowish wake zao wawe as their mamas inategemea na mazuri ya mama yake,na hata kama kila moja ana mazuri yake lakini bado mabaya ni mabaya na mazuri ni mazuri tu so hata kama ni mama au baba au whoever kama ana mabaya utayaona na mazuri utayaona tu.

yeah chaeating zote hazikosi visingizio so naona na wewe kisingizio chako ni searching for a woman with characters like your mama au siyo mkuu?
 

Ukitaka kujua mapenzi ya mama kwa mtoto wake yapoje..mtafute kichaa mwenye mtoto kisha jaribu kumnyang'anya mtoto wake.

Mkuu pamoja na kwamba mke haji kumridhisha mama, bali wewe.., subiri itokee mama na huyo mke hawaivi uone maisha yako yatakavyokuwa 'matamu' kama shubiri.
 
MWANAUME AKIPATA MKE MWENYE SIFA HIZI MBILI

1. Anampenda Mungu, anamcha Mungu, anakupenda, kukujali na kukuheshimu
2. Anaelewana na mama yako

....basi wewe kazana kutafuta maisha, matatizo ya ndoa kwisha kazi. Labda uwe una yako mengineyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…