Enyi wake wa wanasiasa za mageuzi, washikeni mikono waume zenu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wanawake wa sasa katika mataifa ya kiafrika, wanawakataza waume zao wasiingie kwenye harakati za kisiasa za upinzani.., mbaya zaidi wanatoa sababu za ajabu kabisaa, eti.., watabaki wajane waume zao wakiuwawa kwenye mapambano hayo na harakati za kisiasa...., miaka hii ni tofauti sana na wanawake wa zama zile.., hayati mzee Karume aliwahi kumueleza mkewe, kwamba, kama atakutwa na mauti katika mapinduzi ya kumuondoa Sultani katika ardhi ya Zanzibar, basi mkewe aishi kwa furaha na amani kwa sababu mumewe ni shujaa.., na akamtaka asomeshe watoto wao (endapo atakutwa na mauti)...

Unaweza kuwa mjane hata bila mumeo kujihusisha na harakati za kisiasa, wapo wanawake wengi waliobaki wajane kwa sababu waume zao walikutwa na mauti katika ajali, magonjwa, ugomvi, vifo vya ghafla etc... Kuwa mjane hakutokani na mumeo kujihusisha na siasa za mageuzi...Naomba niwakumbushe kitu hapa... (nitaandika historia fupi ya wake wa wanasiasa walioachwa wajane.. Lakini hadi leo majina yao yanaendelea kuishi milele)..

Pauline Lumumba aliyekuwa mke wa mwanamapinduzi wa Zaire (sasa DR Congo) Patrice Emery Lumumba.., alishuhudia kukamatwa kwa mumewe mjini Ilebo jimboni Kassai-Occidental kabla ya kuuliwa kwake jimboni Katanga Januari 17, 1961. Alichofanikiwa kubaki nacho Pauline ni Barua ya Lumumba kwa mkewe ambayo aliita “risala yangu ya mwisho kwa Pauline”..

Kwenye risala hiyo, Emery Patrice Lumumba alisema hahofii maisha yake mwenyewe, ikiwa itahitajika kumwaga damu yake ili wakongo wapate uhuru wa kweli, kamwe hawezi kusita... Pauline Lumumba alishuhudia mumewe akikamatwa, lakini hakuwahi kuona maiti ya mumewe, hadi na yeye mauti yanamkuta.. Mwili wa mumewe unatajwa kuchomwa na tindikali na kuyeyuka baada ya kuchomwa visu na kuachwa dakika 20 asikilize maumivu..

Mke wa mwanamapinduzi wa Burkina Faso, Thomas Isidore Nöel Sankara anaitwa, Mariam Sankara,... Thomas Sankara alikuwa Rais wa Burkina Faso (zamani Upper Volta) kuanzia 4 August 1983 kabla ya kuuwawa 15 October 1987.. Sankara aliuwawa mwaka 1987 katika mapinduzi ya kijeshi ambayo yanatajwa kuratibiwa na rafiki yake Blaise Compaore.. Wakati Sankara anafariki, alimuacha mkewe mjane na watoto wawili (Phillipe na August)...

Wakati baba yao anafariki Phillipe alikuwa na miaka 7, August alikuwa na miaka 5... Baada ya kifo cha mumewe aliamua kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa, Mariam Sankara ameishi uhamishoni tangu mwaka 1987 hadi 2007 aliporuhusiwa kurudi Burkina Faso... Mariam alirejea nchini kwake, Burkina Faso na kushinikiza kesi ya mumewe ianzs kusikilizwa upya, na mahakama ilitoa amri, kaburi la Sankara lifukuliwe ili kufanya uchunguzi kubaini kama mwili ule ulipigwa risasi...

Kwa miaka takribani 27, Winnie Madikizela-Mandela aliishi bila uwepo wa mumewe (Nelson Madiba Mandela) katika maisha yake, mumewe wakati anafungwa jela kwa makosa ya uchochezi.. (Mandela alifungwa mwaka 1963 na kuachiwa huru mwaka 1990)..,alimuacha Winnie na watoto wawili (1) mkononi (Zenani na Zindzi) .., Winnie hakukata tamaa, aliendelea na mapambano ya kisiasa dhidi ya ubaguzi wa rangi..

Wakati huo Mandela akiwa gereza liko kisiwani linaitwa 'Robben Island'... Winnie anaaminika kuwa mmoja kati ya wanawake jasiri kuwahi kutokea Ulimwenguni.., historia ya Afrika Kusini inamtaja Winnie kuwa mama wa taifa hilo, aliwahi kufungwa jela akiwaacha watoto wake uraiani... Akiwapigania wananchi wa Afrika ya kusini.. Winnie Mandela na Nelson Mandela walikamilisha rasmi talaka yao machi 19, 1996.. Pia Winnie Mandela amewahi kufungwa jela miezi 18 kwa kosa la uchochezi mwaka 1969...

Graça Machel, ambaye ni mjane wa Nelson Mandela na pia Rais wa zamani wa Mozambique, Samora Machel,.. Mwaka 1975 baada ya Mozambique kupata uhuru, aliteuliwa kuwa waziri wa elimu na utamaduni wa taifa hilo, na baadae kuolewa na Samora Machel..,

Samora Machel mwaka 1950 akiwa anafanya kazi ya uuguzi katika kisiwa cha Inhaca alikutana na Sorita Tchaiakomo wakaanzisha mahusiano na kupata watoto wanaitwa Joscélina, Idelson na Olívia.. Mwaka 1963 kabla Machel hajaindoka Msumbiji na kujiunga na FRELIMO, alianzisha mahusiano na Irene Buque ambaye walipata mtoto anaitwa Ornila... Pamoja na kuzaa nao hawakuweza kuwaoa Tchaiakomo au Buque.

Mwaka 1969,Tunduru Tanzania, Samora Machel alimuoa Josina Abiatar Muthemba.. Akiwa msituni na jeshi la FRELIMO akiusaka uhuru wa Msumbiji. Novemba mwaka huo, walimpata mtoto wao anaitwa Samora (Samito).. Josina alifariki mwaka 1971 kwa ugonjwa wa kansa., miezi mitatu baada ya uhuru (1975) Samora Machel alimuoa Graça Simbine maarufu kama Graça Machel.. Walipata watoto wawili Josina na Malengane..

Mwaka 1986, Samora machel alifariki katika ajali ya ndege nchini Afrika kusini.. Graça Machel ndiye mwanamke pekee ambaye ametumikia nafasi ya 'first lady' kwenye mataifa mawili tofauti.., Mozambique 1975-1986 na Afrika ya Kusini 1998-1999..., Graça Machel aliishi na mumewe kwa miaka 11 pekee...

Fathia Nkrumah.., mke wa Rais wa kwanza wa Ghana huru Osagyefo Kwame Nkrumah.. Fathia alizaliwa katika wilaya ya Zeitoun katika nchi ya Misri.., kabla ya kuolewa na Nkurumah, alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi inaitwa Notre Dame des Apôtres huki Zeitoun.. Aliacha kazi ya ualimu na kuanza kufanya kazi benki, huko alikutana na Nkurumah.., ingawa mama yake alikataa kwa sababu Fathia alikuwa mwarabu wa Misri na Nkurumah mweusi wa Ghana..,

lakini mchana wa siku ya mwaka mpya (1957-1958) walifunga ndoa.. Mwaka 1966, mapinduzi ya kijeshi yaliyoendeshwa na wanajeshi katika nchi ya Ghana yanahusishwa na mkono wa majasusi wa CIA., waliwakamata na kuwaua wanachama wa chama cha kisiasa cha Nkurumah kiliitwa Convention Peoples Party (CPP).., wengine wakiwepo Nkurumah walikimbia nchi na kuanza kuishi uhamishoni.. Alikimbilia Guinea Conakry.. Ambako alipewa hifadhi na Rais wa nchi hiyo Ahmed Sekou Toure..

Huko alipewa heshima ya kipekee kama Rais wa nchi hiyo.. Nkurumah alifariki kwa ugonjwa wa kansa mwaka 1972 akiwa na miaka 62... Hadi anakwenda kuishi uhamishoni Nkurumah alimuachia mkewe watoto watatu, Gamal (1959), Samiah (1960) na Sekou (1963).., hivyo ameishi uhamishoni.., mkewe akiwa pekee yake kwa miaka 6....

Aleida March (mke wa Ernesto Che Guevara).., huyu aliachwa na watoto wawili mkononi wakati mumewe akikutwa na mauti Oktoba 9, 1967 (akiwa na miaka 39) huko La Higuera, Vallegrande, Bolivia..

Betty Dean Sanders maarufu kama Betty Shabazz, alikuwa mke wa Malcom X.., mpigania haki za watu weusi na usawa na pia mwanaharakati... Alifariki Februari 21, 1965 (akiwa na miaka 39) Manhattan, New York, U.S.A.., hadi anafariki, alikuwa amepata watoto 6.. (Qubilah Shabazz, Ilyasah Shabazz, Attallah Shabazz, Malikah Shabazz, Gamilah Lumumba Shabazz, Malaak Shabazz)

Rais wa 35 wa Marekani, John Fitzgerald "Jack" Kennedy.., alifariki November 1963 huko Dallas, Texas, United States.. Alikuwa amemuoa Jacqueline Kennedy Onassis, John F Kennedy alikuwa Rais wa Marekani tangu mwaka 1961 hadi mwaka 1963.. Jacqueline aliachiwa watoto wanne (Caroline Kennedy, John F. Kennedy Jr., Patrick Bouvier Kennedy, Arabella Kennedy)

Martin Luther King Jr., alikuwa muhuburi wa injili wa dhehebu la Marekani la Baptist, moja kati ya waanzilishi wa vuguvugu la kudai na kupigania haki za wamarekani weusi.., aliuwawa kwa kupigwa risasi Aprili 4, 1968, huko Memphis, Tennessee, United States.. Alikuwa amemuoa Coretta Scott King, wakapata watoto wanne., (Martin Luther King III, Dexter Scott King, Bernice King, Yolanda King).., hivyo mwaka 1968 wakati wa kifo cha Martin, alimuacha Coretta akiwa mjane...

Mifano inatosha kwa leo
 
Rais si mtu wa kuchezewa na kutukanwa ovyo...hao wanawake wanajua nguvu ya rais.... anauwezo hata wa kuagiza kichwa chako kikaletwa kwenye sahani ndani ya saa moja..na hiko kichwa kinaweza hata kuchukuliwa wakati umelala na mkewako kitandani..
 
Walau leo nlitegemea hata ungethamini mchango wa mke wa katibu mkuu wa zamani Dr. W Slaa na kutuelezea jinsi alivyoingia front line...Lakini mmeishia kumtukana
1470306214286.jpg
 
Rais si mtu wa kuchezewa na kutukanwa ovyo...hao wanawake wanajua nguvu ya rais.... anauwezo hata wa kuagiza kichwa chako kikaletwa kwenye sahani ndani ya saa moja..na hiko kichwa kinaweza hata kuchukuliwa wakati umelala na mkewako kitandani..
Hebu naomba sehemu tusi lilipotoka kwenye hiyo post?
 
Walau leo nlitegemea hata ungethamini mchango wa mke wa katibu mkuu wa zamani Dr. W Slaa na kutuelezea jinsi alivyoingia front line...Lakini mmeishia kumtukana
View attachment 375935
Huyo aliingia front lakini aliishia kutukanwa na makamanda baada ya chama kupata direction mpya..wake wa makamanda washaurini vyema waume zenu msije kuashia kama huyu..
 
Huyo aliingia front lakini aliishia kutukanwa na makamanda baada ya chama kupata direction mpya..wake wa makamanda washaurini vyema waume zenu msije kuashia kama huyu..
Tafautisha kutukanwa na kukimbia... kweli vijana wa Lumumba mkiambiwa akili zenu ni nusu kijiko msichukie ndio size yenu hiyo
 
Rais si mtu wa kuchezewa na kutukanwa ovyo...hao wanawake wanajua nguvu ya rais.... anauwezo hata wa kuagiza kichwa chako kikaletwa kwenye sahani ndani ya saa moja..na hiko kichwa kinaweza hata kuchukuliwa wakati umelala na mkewako kitandani..

Baada ya kuletewa kichwa wewe unaishi milele?
 
Huyu mama mlikua mnamfungulia thread humu kila uchwao na kumtusi, records speaks from themselves, watu wabaya sanau nyie.
Ndio maana nimekwambia mchukueni huko ccm atawafa sana nyie maana nyie si watu wa namna hiyo mnawapenda sana
 
Miaka ya kuanzia 1960 mpka miaka ya 1990 dunia ilikuwa inapitia katika kipindi cha transition katika kuelekea democracy hii tuliokuwa nayo sasa hv kati ya miaka hiyo vikundi vingi na watu walijitokeza kudai madai mbalimbali ikiwamo haki zao ,uhuru wao,mageuzi ya kimfumo na kisiasa vitu vingi vilifanyika ikiwamo mapinduzi na violence za aina mbalimbali zilifanyika ktk nchi nyingi duniani na zote hizo ziliongozwa na watu waliojiita wanaharakati si wanasiasa coz siasa na harakati haviendani.

siasa mlengo wake ni maridhiano ndo maana cku zote siasa huwa inafanywa hadharani tofauti na harakati ambazo unaweza kuzifanyia popote hata msituni tunapozungumzia siasa ni lazima pawepo na mtawala na watawaliwa na siasa nyingi hufanyika kipindi cha kampeni baada ya hapo siasa uamia sehemu husika ambayo ni bunge au katika mabalaza ambayo yapo kisheria ni kenya na tanzania pekee ambapo uchaguzi ukimalizika siasa bado zinafanywa
nje ya mifumo wa kibunge au kibalaza

sasa leo kinachfanywa na chadema kilishafanywa na watu miaka kati ya1960-1990 na kwa lugha yepesi ni harakati na si siasa pia wanatakiwa kujua ya kwamba siasa za dunia cku hizi zimebadilika sana ni wapi katika dunia hii wanafanya siasa kama wanazofanya chadema ?? ukisikia maandamano basi ujue ni chama cha wafanyakazi au wanaharakati na pia cku zote njia yeyote ya kuvunja amani hutumiwa na watu walioshindwa kufanya siasa na kuhamia uanaharakati
 
Back
Top Bottom