English medium nouma jamani, nifanyeje nijue kingereza?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,357
6,896
Katika harakati za kutafuta ajira nimepata kazi ya kufundisha English Medium, kwa kuwa siwezi kuongea kingireza nikachagua kufundisha Maths na ICT, sasa bwana ikaja ikafika siku ya kushika zamu za wiki, katika kutoa taratibu hapo paredi aisee natetemeka hadi mdomo kwani hakipandi kabisa kile nilichokremu ndio hicho.

Yani siwezi kuongea zaidi ya dakika 2 hadi wanafunzi wananishangaa kwanza ninavyo kibrokeni, kumbuka wale watoto ni wakali na wanaenda kunisemea hadi kwa bosi japokua analifahamu hilo lakini kavunga kwa ninachokifundisha kinaeleweka. Ila sasa hawa watoto wananishangaa hadi nasikia aibu huku nikijaribu kujikakamua lakini zero hadi jasho la mgongoni linanitiririka.

Jamani naombeni msaada kwa anayejua njia inayomwezesha mtu kuongea kingereza yani nimejaribu lakini basi tu.
 
Dah pole mkuu.. Jitahidi uwe marafiki na hao hao watoto kwanza na muda mwingi ongea nao kingereza hata kama ni broken. Wakikucheka wewe ndo unajifunza kwa haraka nakwambia ndani ya mwaka tu utaomba kufundisha somo la kiingereza.:rolleyes:
 
Haaaaa nimecheka kweli hadi machozi mweee kazi hizi Pole sana mkuu.

Hao hao wanafunzi wako ndo watumie vizuri kama walimu wako, jishushe kuwa na urafiki nao kwa madarasa tofauti jichanganye na ongea nao ngeli muda wote baadabya Mwezi mmoja tu utakuwa mbali ukiwa serious.
Pia omba msaada kwa walimu wenzio hasa wale wa lower classes utaongea soon , wanajua mbinu za kumfanya hata mtoto aliyehamia kutoka Swahili medium muongea Kiingereza ndani ya wiki tu .

Kifupi kuwa kiherehere na jiwekee malengo ni kazi rahisi kama kuchana karatasi tu mkuu.
 
Yan we endelea kumuhonga boss wako km unavyofanya wala hao wanafunzi wasikutishe utajua taratibu kwa kusoma vitabu vyao
 
ulifauluje mkuu au una vyeti feki?
Kawaida sana kwa wasomi kutokea shule za swahili medium a.k.a kayumba wengi kiingereza hakipandi Elimu Chuo Kikuu halali kabisa, wanakariri kiingereza badala ya kuelewa lugha . Hata walimu wa sekondari wengi wanavunjavunja tu mkuu so usishangae wachache sana wanaweza kutoa hata tangazo kwa ufasaha bila kuchanganya na kiswahili haaaaa
 
Back
Top Bottom