ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Kuna shida Gani, Sasa hivi suala la kuongea Kingereza limezidi kuwa kubwa kadiri siku zinavyozidi kusogea, Sasa hivi yani watanzania wengi Wana elimu ya form four au six , Ila wengi hawajui Kingereza, na hao wachache wanaojitahidi au tumasema wanakijua asilimia kubwa zaidi ya 98 ukiwasikiliza wanaongea Broken English japo anaeleweka lakini broken si sana mfano waziri wa elimu Prof. Ndalichako, hata Lissu ana kizungu kizuri lakini anachapia akiongea muda mrefu, mama Samia anaupiga mwingi kwasababu anasoma, katika kusoma ni rahisi kuliko free style.
Wakenya wanafanyaje, na hizi aibu zetu tunaziweka wapi, sababu hata Mwalimu wa lugha Dr. Lwaitama anachapia Kingereza.
Wanaosoma shule za English Medium ni wachache mno 0.0x , wengi ni mashule ya Serikali ambapo hata walimu hawajui Kingereza, Somo la English linafundishwa kwa kiswahili , yaani wanafundishwa cha kujibia mtihani.
Ukienda You tube , Mtanzania akaongea Kingereza atapata comments mbaya sana, Kuna wakati Hadi wanasema Lissu anawahutubia mabeberu siyo watanzania.
Angalau Mkapa alikuwa anakipiga chenyewe