Kuzungumza na kuelewa Kiingereza kunategemea sana na ufahamu wa matumizi ya maneno. Mimi kilichonifanya niwe fluent katika lugha ya Kiingereza ni kusoma vitabu vingi na magazeti mengi. Nimesoma series yote (novels) ya James Hardley Chase (zaidi ya vitabu 90), Novels nyingi sana za African writers, cartoons series nyingi (kama vile Tintin, Asterix, Andy Cap, X-men, nk.). Pia watoto wangu walipokuwa wadogo tulikuwa tunaangalia pamoja cartoon zao kwenye runinga. Nilisikiliza sana taarifa za habari na audio books za Kiingereza.
Kusoma vitabu na majarida ya Kiingereza ni njia moja nzuri sana ya kukuza msamiati wako na pia kuona maneno yanavyotumiwa. (Chagua vitabu unavyovipenda kama vile vya hadithi). Njia hii itakusaidia kuweza kuzungumza, kuandika, na kuielewa hii lugha ya Kiingereza.
Tatizo tulilokuwa nalo siku hizi ni kuwa watu hawasomi vitabu au magazeti kwa sababu kila wakati uko mbele ya runinga kwa habari na burudani.
Nitajaribu kushiriki kwenye huu mjadala na naomba msinichukie kwa sababu nitakuwa nawakosoa watu mabandiko yao ya Kiswahili na Kiingereza. Na ili tuwe kwenye ngazi moja, atakaeona kosa langu lolote la matumizi ya Kiingereza au Kiswahili hapa basi naomba anisahihishe haraka sana. Lakini ili tujifunze vizuri, punguzeni kejeli na ngebe. Utani wa kawaida sio mbaya.