ENGINE YA TOYOTA LANDCRUISER AINA YA 1HZ INAHITAJIKA!!!..

Mawio

Member
Nov 25, 2008
54
95
Wakuu, salaam!!!..

Ninahitaji Landcruiser 1Hz Series iwe katika hali nzuri.

Mwenye nayo ani-cheki inbox au kwa namba hii +255788246790

Bajeti/Pesa niliyonayo mkononi ni Millioni mbili na nusu (2,500,000/=) Pesa za Ki-Tanzania.

Shukrani.
 
maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,210
2,000
Wakati mwingine najisikia hasira lakini na gundua ni ujinga.

Fanya utafiti wa awali kabla ya kupost kitu.

Engine za magari zina bei zake na zinajulikana.

Hivi ukisema unataka engine ya 1 HZ kwa 2.5m uko sawa kweli?

Jiulize ya Rav 4 itauzwa bei gani?

Hata ya wizi huwezi pata.
 
Mkuu Maringeni!!!..

Huna haja ya kupata hasira Kaka, hili dogo moja tu linakutia hasira Mkuu?!! Mbona kuna mengi ambayo ukitaka kukabiliana nayo kwa namna hii utabaki kitandani unaugulia maumivu ya hasira wala usitoke nje!!!..

Taratibu tu Mkuu, bahati mbaya sana (kama utapenda kuiita hivyo) Mwenyezi Mungu kaijaza dunia hii na viumbe wa kila aina; wafupi, warefu, wanene, wembamba, weupe, weusi n.k, pia uwezo wetu wa kuona, kufikiri, kusikia, kupanga, kuamua n.k hutofautiana pia, hilo linakwenda mbali zaidi hata kufikia namna tunavyoweza pata taarifa (kwa maana ya uwepo wa taarifa husika, teknolojia ya usambazaji, gharama za kuifikia taarifa husika n.k).

Utofauti wetu ndio tunu yetu (na hii inakwenda mbali kabisa mpaka kwenye utofauti wetu wa rangi za ngozi, jinsia, mahali mtu alipotoka, imani zetu, mitizamo na itikadi za kisiasa, tamaduni n.k) na ndio hutufanya tuione dunia hii katika mwanga tofauti kila mmoja wetu, tuna mengi mno yanayotutofautisha kama binadamu tukiyaangalia kwa upande mmoja tu itatuwia vigumu sana kuielewa hii dunia. Hebu tutambue na tushukuru mizania na kani ya uwiano wa uwepo wetu na yote yatokanayo na hilo.

Hongera kwa kuwa na taarifa (kwa kiwango ulichonacho) kuhusu magari na vifaa vyake, kwa bahati mbaya sana Binadamu hatukuwahi wala hatutaweza kuwa sawa kila wakati au wakati wote, ningeshukuru sana kama ungeweza kuweka bandiko la bei za magari yote, kwa miundo yake yote, matoleo yake yote, vifaa vyake vyote kwa hali zake zote ili kukwepa kughafirishwa na mbumbumbu watarajiwa kama mimi.

Kwa sasa ninachojua tu ni kuwa ninahitaji engine ya Landcruiser 1Hz, na pesa niliyonayo kwa minajili ya engine hio ni millioni mbili na nusu (2,500,000/=) pesa za Ki-Tanzania na nina imani kuna mtu mmoja, sehemu flani atakuwa na uhitaji wa pesa hiyo dhidi ya engine hio ninayoitafuta.

Mkuu Maringeni, sitaki kufikiria uwepo wetu na ushiriki wetu enzi za "BARTER TRADE" ya wahenga, Daaaah ingebidi nivae "BODY SHIELD" Kabisa, Daaaaaaah...LOL :):)!!!..

Kuna kabandiko haka kanaweza kushusha hasira zetu pia..

Kwa sasa nikutakie jioni njema sana, na mafanikio katika kuufunga mwaka 2018 na kuelekea 2019.

Jioni njema Mkuu..

¬Mawio :):)!!!...
 
Attachments

Mubby777

JF-Expert Member
Oct 17, 2018
223
1,000

Kwa hili jibu la kistaarabu jamaa alikuja na hasira zake za umaskini atakuwa msata anakimbilia morogoro
 
Mawio

Member
Nov 25, 2008
54
95
Kwa hili jibu la kistaarabu jamaa alikuja na hasira zake za umaskini atakuwa msata anakimbilia morogoro
Mkuu Mubby777!!!..

Salaam.

Tumuombee Amani ndugu yetu Maringeni, hatujui ni nini kimemkumba mpaka akawa na hasira nyingi na za ghafla sana kwa jana.

Nategemea kesho itakuwa siku nzuri kuliko jana kwa kila mmoja wetu.

Amani iwe kwenu nyote Wakuu..

Shukrani sana.

¬Mawio :):)!!!..
 
Mawio

Member
Nov 25, 2008
54
95
Nimewahi ninua 1HZ kwa ajili ya coaster kwa 1.5M.
Mkuu Tabutupu.

Salaam.

Biashara ni makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji na mara nyingi huongozwa na utashi wa muuzaji kuuza mali/huduma yake na mnunuzi kuwa tayari kununua mali/huduma inayouzwa na muuzaji kwa viwango vitakavyokubaliwa na pande mbili hizi kuu, likiishafikiwa hilo basi taratibu nyingine za kisheria na mengineyo hufuata na mchakato wa kufanya biashara kukamilika.

Bado ninasubiri kwa hamu hii kanuni ya Mkuu Maringeni ya "COOKIE CUTTER MODEL" & "ONE SIZE FITS ALL"!!! ikiambatana na kanuni (ndogo au kubwa), taratibu na miongozo yake na mie ninufaike nayo.

Tofauti na hapo nitaendelea kuamini katika utaratibu-tangulizi hapo juu.

Niwatakie Amani, Afya, Mafanikio na Maendeleo kupitia jukwaa hili tukufu ninyi nyote bila kumsahau ndugu yangu Mkuu Maringeni.

Shukrani,

¬Mawio :l :l ...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom