Eng Stella Manyanya: CHADEMA Wanahusika na mgomo wa madaktari; amfananisha Ulimboka na Hitler

Hivi huyu mama ana akili kweli?Nahisi nyanya zimejaa kichwani, tena zimeanza kuoza
 
nimemsikia vizuri sana huyu mama akiihusisha chadema na tukio la Dr kupigwa, nilicho kinote hapa ni jinsi wabunge wa ccm wanavyoshabikia nakufurahishwa kupigwa vibaya na kuumizwa kwa Dr ulimboka Kwa kweli hili ni jambo ambalo sikutegemea kuliona kwa mbunge yeyote hasa ukizingatia anaonekana na wananchi wake!
Huyu Stella matomato analipwa milioni kumi plus marupurupu ya bure toka kwa kodi ya watanzania wanaouwawa kinyama kama Dr. Ulimboka. Akiangalia hizo hela zinampa kichaa ndiyo maana ameamua kushangilia kwa hali na mali aliyotendewa mtetezi wa wanyonge wa taifa hili. Pia kwa kuikashifu Chadema inayoendeshwa kwa nguvu ya wananchi ametukashifu sisi wote. Jamani hili ni taifa dhaifu linaloongozwa na kiongozi DHAIFU. Aliwapa ubunge Manyanya na wengine anaoweza kuwafikia kirahisi na kutimiza haja zake ambazo anazijua yeye mwenyewe. Watanzania tunavuna matunda Dhaifu na hivyo nchi inaelekea kuwa Dhaifu on a daily basis. Mungu ibariki Tanzania na manyanya yake yote.
 
hayo yalisemwa LEO bungeni na Eng huyo mwanasiasa akidai kwamba watu waliomteka Uli walivaa magwanda ya Chadema,hivyo kuuhusisha utekaji na tukio zima la Dr Ulimboka na CHADEMA
Mama anachanganyikiwa huyo! Hafanyi lolote huko 'Nyasa - Mbinga"
 
Romance:

sitta_mdee.jpg

 
Huyu si mwanzo alikuwa kati ya waliokuwa wanajiita wapambanaji wa ufisadi kwenye tume ya mwakyembe!
 
Huo ndio ukweli hakuna uongo hata chembe hapo, ukweli Leo umewauma sana sana cdm, niliisha wahi sema cdm ni kikundi cha wahuni, si mmeona sasa mnataka kumuua ulimboka
Ulimboka amesema na amenukuliwa na vyombo vya habari kwamba alikamatwa na askari waliokuwa wanataka aseme ni nani anayewachochea wagome. Sasa unaposema ni chadema una maana kwamab Chadema wana polisi wao? Mnyika amewaambia bungeni kwamba mtangaze mbele ya bunge kwamba polisi ni mali ya chadema halafu muone cha moto.
 
ndi tatizo la kuwa mchumia tumbo! Nampenda sana "manyanya" kwani anaimarisha chama
 
Licha ya kusema waliomteka dr ulimboka ni chadema, Huyu mama analeta ukabila kwenye hii nchi. Pale aliposema anataka madaktari wafanye kazi walikotokea. Huyu maza swaga zake vipi?
 
Nadhani huyu mama ana matatizo ya akili make hata katika simple reasoning haiwezekani Chadema wachochee mgomo na hao waliochochea mgomo wamteke Dr. Ulimboka haiingii akilini. Pengine angesomeka iwapo dr. Ulimboka alikuwa anazuia mgomo ihali CDM wanashinikiza madaktari wagome. Jamani wabunge CCM let's grow up and mature.

Hata mimi ndo hapo nashindwa kuelewa huyu mama alimaanisha nini.Wanaochochea mgomo tena wamteke Dr.Uli???Kweli nimeamini ukiwa CCM akili inakuwa haifanyi kazi.Tutafika tu ngoja waendelee kuropoka
 
Mama anachanganyikiwa huyo! Hafanyi lolote huko 'Nyasa - Mbinga"

naona wewe ndio unachanganyikiwa na kuchanganya mambo vibaya sana kuliko mama,kwa taarifa tu ni kwamba hayuko huko nyasa sijui mbinga,yuko sumbawanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom