Endelezeni kwenu- Pinda

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Nyie wana JF endelezeni kwenu na sio kujichimbia Ulaya na Dar tu kwi kwi kwi!!!!
Waziri Mkuu ashawishi wazawa wa Rukwa kuwekeza kwao

Na Peter Edson

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewataka wakazi wa mkoa wa Rukwa waishio katika jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine kurudi katika mkoa wao na kuwekeza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na wakazi wa mkoa huo wanaoishi Dar es Salaam katika mkutano wa kujadili mpango mkakati unaoweza kutatua kero zinazoukabili mkoa huo, Pinda alisema ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi, wazawa wa Rukwa hawana budi kurudi katika mkoa kuwekeza.

揝ina maana ya ninyi kurudi kule na kuacha shughuli zenu hapa ila nasema sisi tunaokaa mbali na mkoa wetu, hatuna budi kurudi nyumbani kuwekeza miradi ya maendeleo kwa lengo la kuufanya mkoa wetu uwe na hadhi,攁lisema Pinda.

Alisema wazaliwa wa mkoa wa Rukwa, wana uwezo mkubwa wa kushughulikia matatizo ya mkoa huo ilimradi waongeze umoja na mshikamano.

揗koa wa Rukwa uko nyuma kimaendeleo, wawekezaji wengi wanashindwa kuwekeza kwa sababu za kijiografia na kuwepo kwa miundombinu mibovu. Ili kuwavutia, tunatakiwa kuwa mfano, turudi kuwekeza kwetu,攁lisema Pinda

Alisema pamoja na kuchelewa kwa maendeleo katika mkoa huo, jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa kuanzia sasa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu na kuipa elimu kipaombele.

Mbunge wa Kwela Crisant Mzindakaya aliwaeleza wazawa wa mkoa huo kuwa wakifanya mchezo wageni watauvamia na kuwekeza miradi yao.

揘yumbani ni nyumbani tu, ni vema tukarudi na kufanya maendeleo kwetu, siku zinazokuja tutashindwa kupata ardhi kabisa kwa kuwa wenzetu wamegundua vivutio na fursa zilizopo wanazichangamkia kwelikweli," alisema.
 
Asije akawa anajianda kutumia kauli hiyo kuanza kusukumia kila kitu kwao na kusahau kuwa yeye ni waziri Mkuu wa Tanzania
 
Asije akawa anajianda kutumia kauli hiyo kuanza kusukumia kila kitu kwao na kusahau kuwa yeye ni waziri Mkuu wa Tanzania

Mkuu Mpita Njia,

Cha kumuuliza ni yeye kafanya nini huko kabla ya kuwa PM? Kusema rahisi lakini kutenda kazi kweli.

Mimi ni mwumini wa kusogeza maendeleo mpaka kule wilayani kwahiyo nakubaliana naye juu ya wito huu.

Kule Rukwa wanasema ukitaka kurudi lazima upitie bagamoyo kwanza, vinginevyo mchana ni binadamu na usiku unakuwa punda mbeba mizigo. Ni ujinga tu uliozidi kikomo, wanatisha watu kwa uchawi mchwara ambao haupo!
 
[quote
Mbunge wa Kwela Crisant Mzindakaya aliwaeleza wazawa wa mkoa huo kuwa wakifanya mchezo wageni watauvamia na kuwekeza miradi yao.
[/quote]

Hizi kelele za uzawa wa kimikoa ni hatari. Wao ''wakivamia'' Dar es Salaam ni sawa, kwao hawataki 'tuvamie''! Sielewi
 
Dar haina wenyewe, ni yetu wote, huko mikoani ndiko kuna wenyewe. Neno uzawa naona linaanza kutumika vibaya. Mtanzania yoyote ana haki ya kuishi popote pale anapotaka.

Sisi kule kwetu Kyela tunatimua Wakinga eti sio wazawa, ni ubaguzi mtupu!
 
Dar ina wenyewe. Kilichofanya watu kuhamia dar ni kutafuta economic means. Na huko kwa mnakoita kwa wenyewe, watu wanashindwa kuhamia, kurudi au kujenga ni kwa sababu hakuna chachu za kuendesha engine za maendeleo. Zikiwepo basi watu watahamia na watajenga tu.

Na kilicho sababisha sehemu nyingi kutokuwa na chachu za maendeleo ni kuanza kujenga ofisi za chama kwanza.
 
Yap, naona sasa viongozi wetu wanalewa... ni aibu kubwa kwa wazirri mkuu kuwaambia wananchi waendeleze makwao..ikwa namna yoyote ile itatafsirika vibaya sana..Sasa naanza kuamini pengine madaraka wengi wamechukua bila kuwa na sifa zinazostahili..
 
Bob umeendeleza kwenu. Kwetu mi narudi kutambika na kupalilia makaburi tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom