Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Nkasi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charles Makongoro Nyerere ametembelea Wilaya ya Nkasi tarehe 10 Julai 2023, kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo.

Mhe. Makongoro amekagua kazi za ujenzi wa miundombinu ya Elimu Msingi katika vijiji vya Ntalamila, Kirando na Mtakuja chini ya mradi wa BOOST. Aidha amekagua ujenzi wa Bweni na Vyumba vitatu vya Madarasa kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Kate.

Mhe. Makongoro amepata nafasi ya kutembelea na kukagua mradi wa maji wenye thamani ya Tsh Milioni 743 unaotekelezwa katika kijiji cha Masolo.

Mhe. Makongoro amefika Kituo cha Afya Kate chenye thamani ya Tsh Milioni 500. Amekagua ujenzi wa Jengo la Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Nkasi.

Mhe. Makongoro amewaelekeza Wakurugenzi wote wa Halmashauri Mkoa wa Rukwa kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo ili kutimiza azma ya Serikali ya kuboresha huduma. Aidha ametoa maelekezo kwa TAKUKURU kuchukua hatua kwa haraka ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa rai na maelekezo yake kwa Halmashauri zote za Rukwa kuingiza katika Mipango na bajeti zao mpango wa ujenzi wa nyumba za watumishi ili kuboresha mazingira ya kazi na kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa Mkoa unaovutia kwa watumishi kufanya kazi.View attachment 2692131View attachment 2692133View attachment 2692134View attachment 2692136View attachment 2692132View attachment 2692135View attachment 2692137View attachment 2692138
IMG-20230718-WA0037.jpg
IMG-20230718-WA0042.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom