Endeleeni kuota maendeleo enyi wadanganyika

Endeleeni kuota maendeleo enyi wadanganyika

Umtama Mula

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2021
Posts
230
Reaction score
607
So long tumeamua kuwa watu wenye akili katika nchi are not fit for the office, na kila wakijitokeza,wote rulling party na opposition tunaungana kuwapiga vita. Basi tuendelee kukaa kwa kutulia. Kwa kifupi Wajinga Nchi hii wamefanikiwa kuwathibiti werevu.
 

Attachments

  • VID-20250423-WA0018.mp4
    18.2 MB
Tutavuka kwenye huu mtanziko wa kiuongozi.
Kuna vitu Heche anatufundisha kama Taifa nadhani tukiwatoa CCM madarakani hata kama hatutafikia kilele basi tutakuwa kwenye hatua nzuri ya kuendelea.
Lisu namuona kwenye MH
Heche naona anazo zote MPH
 
So long tumeamua kuwa watu wenye akili katika nchi are not fit for the office, na kila wakijitokeza,wote rulling party na opposition tunaungana kuwapiga vita. Basi tuendelee kukaa kwa kutulia. Kwa kifupi Wajinga Nchi hii wamefanikiwa kuwathibiti werevu.
Sasa wewe hushangai kuna kiongozi hadi anaamua kujiita "chura kiziwi" huoni hapo kuna shida kubwa.!
 
So long tumeamua kuwa watu wenye akili katika nchi are not fit for the office, na kila wakijitokeza,wote rulling party na opposition tunaungana kuwapiga vita. Basi tuendelee kukaa kwa kutulia. Kwa kifupi Wajinga Nchi hii wamefanikiwa kuwathibiti werevu.
Nchi imefirisika , miradi ukiacha Bwawa la Nyerere imesimama. Angalia SGR kipande cha 3 na 4 Yerpi amekimbia. Jamaa wanakwapua na kumtia SSH Hofu. Wanampa moyo kwa kukamata watu na kupiga mabomu ili ashinde uchaguzi. Wao ni kukwapua kwa kwenda mbele. Baada ya Uchaguzi, RASMI TANZANIA inakuwa Zimbambwe.
 
There is an interesting paradox. Usipokubaliana na mambo ya chama au serekali mia kwa mia kunauwezekano mkubwa kupingwa lakini pia sasa tunaona kila mtu anatafuta udaktari ilikuonyesha wananchi kuwa anaujuzi (mpaka wengine wanapitiliza wanakuwa hawana PhD tu, wana Doctor in Humanity 😉 iykyk).
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=mJUkJKUx3Vo

Ndugu Kishore Mahbubani anazungumza hoja za msingi kuhusu 'Mageuzi Jamii'...

Nafasi ya Meritokrasia, Upragmatifu na Uungwana katika maisha na kujichagulia kama Taifa...

Haya matatu, ni muktadha akilifu wa UTU wa NGUVU, kujichagulia na Matendo...

Anazungumza vema kuhusu 'Akili na Utambuzi' kuwa nyezo ya kupanga na kupangua sura za mambo : hili kiufundi ni muktadha akilifu wa 'Ontolojia ya Taasisi'.

Kwetu sisi jamii ya Watanzania hili linatukumbusha KUJISAHIHISHA KIMIFUMO...

Tushitukie ujinga na usanii wa 'kuuziana nyago' kwa vitu vinavyopotosha tusibaini umuhimu ama ukweli wa 'Meritokrasia'... Mambo mfano wa tambo za ukweli ama usanii kuhusu 'Usomi' na 'Majina ya Hadhi', na tena tuzodoane kwa utamaduni mbovu kabisa wa kuvishana vilemba vya Ukoka eti kwa kuwa tunafanya ujanja wa kuchezea akili za wenzetu ili tunufaike na 'fadhila' fulani...

Tukiwa Waungwana, Uungwana ni vitendo--ndiyo huo Upragmatifu...

Upragmatifu ndiyo huleta 'Tekinokrasia'...

Kujisahihisha kimfumo kuna anza na sisi wenyewe 'kujiongeza' na kujisahihisha kama mtu mmoja mmoja... Kutafuta kujua ilivyobora na kuwa waungwana; fimbo ya mbali haiui nyoka, tusiishi kutegemea 'Kiongozi Fulani aje Kulianzisha' kwa kuwa lililotokea Singapore huenda lilikuwa ni lakufaa kwa mazingira na wakati wa 'Kihistoria ya Singapore'.

Tukidhamiria kujisahihisha, hata tunaodhani hawafai wanaweza pia kugeuka na kufaa--kwa kuwa labda hajui tu ama kufahamu; ubaya ubwela -- ukiacha kufikiria jema, unamponza hata yule apaswaye kuwa mwema kuingia katika 'majaribu'; kushawishika kukaza kamba ya vuta nikuvute...

Mwenendo wa kukabiliana kwa nguvu na kupaniana siyo suluhu pekee, tuisafishe mioyo yetu ili tufanyike dhamiri ya Utu wa Nguvu...

Sisi pia tunaweza kutengeneza simulizi tofauti kwa mapelekeo hayo hayo: Kuanza na Mapinduzi ya Akili na Utambuzi kwa Wanajamii: Kila Mmoja afundishe/Amuangazie Mmoja mwingine...
Ujamaa ni Imani, kadiri vile Uhuru ni Kazi--watendaji wa chama na serikali kwa wakati wanaweza kuonekana kukengeuka na kujaribiwa na vishawishi vya 'kutafuta maslahi binafsi' kupitia ujasiria-mifumo, utendaji, upendeleo wa kimadaraka--hili ni jambo lililo ndani ya hesabu ya 'Waona Mbali' juu ya hatma ya Taifa; Japo kuwa hivi hakuhalalishi 'nia ovu'. Ubepari ni harakati za mpito za mifumo ya kibinadamu katika 'gombania goli' ya 'ukwasi wa kirasilmali fedha' na 'hijimoni' za jumuiya ya kimataifa. Ubepari ni shughuli isiyoishia na maendeleo ya kweli ya watu bali 'Vitu'. Tanzania kama nchi kwa sasa, kimkakati na tena kama taifa, tunatangamanisha maendeleo ya 'vitu' na 'watu' japo si kiuadilifu mkuu kielimu na rasilimali--rasilimali watu.

Wakati mmoja, siku si nyingi, ajenda kuu ya kitaifa itakuwa ni Elimu--elimu yenye tija kwa wanajamii wenyewe kwa kutafuta kuwajengea wananchi upeo na uweza wa kutekeleza 'siasa za ujamaa na kujitegemea'; japo kiufundi penye upeo halisi wa mtu na maendeleo hakuna 'siasa'. Siasa zipo kwenye 'Nia zisizo Rafiki' za makundi ya watu; watu wenye kujua ilivyobora wana muktadha wa matendo ulio ni 'meritokrasi na tekinokrasi'; siasa ni tunda bovu la misingi ya ubepari na demokrasia liberali; ambavyo maslahi ya kisiasa hujipambanua kwa utafutaji wa nguvu za kimadaraka na hatamu -- hata kama michezo ya 'vikundi vya maslahi binafsi' -- kunajisi 'utakatifu' wa dola yeyote kwa kisingizio cha 'demokrasia' na 'uwakilishi wa nia njema' za 'walio wengi'.

Maono na Busara ya Mwalimu Nyerere, ambavyo inaweza kufanyika na mtu mwingine yeyote mwenye Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ni kwamba >'elimu pekee yake ndiyo inaweza kuleta msingi wa kweli wa Maendeleo ya Watu'< na kisha watu hawa kuyatawala mazingira yao. Kuyatawala mazingira kwa maendelo ya vitu, ufanyaji maamuzi na kujichagulia. Tanzania kwa sasa hatuna utimilifu wa 'ELIMU' hii; lakini, In Shaa Allah--yaja!​
Hmmm​
 
Tutavuka kwenye huu mtanziko wa kiuongozi.
Kuna vitu Heche anatufundisha kama Taifa nadhani tukiwatoa CCM madarakani hata kama hatutafikia kilele basi tutakuwa kwenye hatua nzuri ya kuendelea.
Lisu namuona kwenye MH
Heche naona anazo zote MPH
Hmmm

'Siasa ni Ukanyaboya...'

Hakuna 'Mtu wa Siasa' mwenye 'Kheri Khasa' kwa kuwa huo ni mchezo wa 'mapiku' tu...

Karata ya Shupaza ni 'Utaamuliko Jamii'.

View attachment 3070326

Utaamuliko Jamii: Karata ya ‘Dume la Shupaza’​

ilivyo ni Ufunguo wa ‘Mapiku’​

UTU na UFUNUO ni mambo ya mfano wa ndege Tausimoto na tena habari za watu wa 'kabila Ndege'--Wafanyambawa... Kutoka uchina ndiyo tunaweza kupata seti moja ya mfano kwa ajili ya 'muktadha wa vina vya tafsiri' kwa muktadha akilifu wa uono na ufikirifu mifumo kuhusiana na mafumbo ya imani ya utu--utu na 'kode moto' za Joka/Dragoni katika ulimwengu wa 'Kujichagulia'.

Yantra dhamma, chombo cha Dhamma, ni ukadinali wa jamii katika 'Sovereini Jumuifu'. Kile ambacho ulimwengu wa kileo, fikra za karne ya 19 na 20 juu ya 'Ujamaa ama/na Usoshalisti' vimekuwa ni mbegu ya jambo lenyewe hasa--'Utaamuliko Jamii' utokanao na misingi ya UHURU, UDUGU, HAKI na AMANI.

Hapa Tanzania, jitihada zimefanyika, zinafanyika na zitaendelea kufanyika ili kutimiliza mageuzi kamili ya kijamii kwa ajili ya jamii yenye sifa, hadhi na daraja/utukufu wa 'Sovereini Jumuifu'. Dhamma ni uisho wa maisha kwa msingi ya mafundisho ya Siddhartha ‘Buddha’ Gautama—mtu mkuu aliyepata kuishi duniani takriban miaka 2600 iliyopita.

Mafundisho ya Buddha yana asili ya ‘Gurudumu’ na ‘Mraba’--viwili vya ‘Uisho wa UTU’; Funguo za ‘Nuru ya Ufahamu’ kupitia AKILI, UTAMBUZI na FAHAMU; ambavyo Buddha alitaamulika kuyafahamu ya Ulimwengu wote Mzima na basi kutengeneza msingi wa ‘Miongozo’ ya ‘Utaamuliko’ kwa wengine wote wenye kutafuta ‘WONGOFU’ kupitiliza mafumbo ya Uzima na Miili na Ufahamu. Miongozo hii ndiyo inayofanya asili ya ‘Gurudumu Dhamma’ na ‘Njia ya Buddha’—Dhammapada.
====

View: https://www.youtube.com/watch?v=alnY2sy9_fk
====​

Gari la UTU: ‘Safari ya Kiutamaduni’​


‘Gurudumu’ na ‘Mraba’, karne hii ya 21 ndiyo mapelekeo hasa ya ‘Yantra Dhamma’ na ‘Trizaniamu’. Kiufundi, katika Gurudumu la Dhamma kuna shauri la ‘Utatu’ wa (1) dhahiri, (2) fikra/matendo/nia katika ‘Imani Moja’ na (3) Mifumo—Mambo ya kujihifadhi/kukimbilia katika ‘Hazina’ ya vito thamani vitatu vya Ubuddha—Buddha, Dhamma na Sangha. Ulimwengu wa leo, haya ndiyo asili ya ‘Ontolojia ya Taasisi’ ambavyo ‘Muundo, Kujisikia na Ushawishi’ ndiyo kiini cha UTU na KUJICHAGULIA. Mraba, ni jambo la kielelezo cha ‘Muundo’ ambavyo ‘Miongozo’ ni nguzo ya imani kwa ajili ya fizikia na metafizikia ya jambo/mambo…

Buddha, katika Utaamuliko, alikadirisha ‘kode za utambuzi’ kuhusiana na maisha ya mtu katika ‘mapana ya wakati’--mapana ya wakati ni mapana ya supasha hapo hapo. Hili ndilo msingi wa Buddha na mafundisho ya ‘Kweli Nne za Tunu’; na basi hizi katika karne hii ya 21 ndiyo tunazungumza asili ya maisha ya mwanadamu kuwa ni ‘Mraba ndani ya Duara’--Yantra Dhamma ni ufunguo wa rizayati ya Elimu 3.0 ambavyo ‘Unje-Ndani’ wa ‘Kweli Nne za Tunu’ ndiyo (1) Dhukka, (2) Samudaya, (3) Nirodha na (4) Marga katika kupinduliwa ki-picha ya tafsiri.

Buddha, katika Utaamuliko, alikadirisha ‘kode za utambuzi’ kuhusiana na ‘maisha ya mtu’ kwa ‘Duara na Kitovu/nukta’ cha muktadha wa kadiri ya ‘uono na ufikirifu mifumo’ ilivyo ni mashauri ya ‘Samsara’ na ‘Maya’. Kwa mintarafu ya haya mawili, (1) fahamu, (2) uono na (3) vina vya tafsiri kuhusiana na yote, yaliyodhahiri katika fahamu za kimwili na hata yale yanayopitiliza fahamu tano za mtu, ni ‘maruweruwe-Maya’ katika bahari ya ‘uzima wa miili’. Basi yawa, Samsara ni hatma za UTU ufanyikao na ‘miili katika uzima’.

Buddha, katika Utaamuliko, alikadirisha ‘kode za utambuzi’ ambavyo usifa-akili hu-tatu-sha mapana ya (1) mtenda, (2) kitendo na (3) jambo. Kwa mintarafu ya hili, uono na ufikirifu mifumo ndiyo intelijensia ya yote—mambo ya dhahiri na isivyodhahiri ya ‘tukio’. Hili lafanya meza ya ustawi wa jamii, kiufundi, ni mraba wa ‘Wakati-Jamii-Machaguo ya Kitaasisi-Matukio’. Ili kuweza kumudu fasaha ya uono na ufikirifu mifumo, ndiyo hubidi ‘mwanakisomo’ awe ni mtu wa ‘vipassana’, Basi ndivyo alama ya ‘UONO’ katika TRIZANIAMU ni mfano wa gurudumu la dhamma – gurudumu la dhamma pasi ‘duara’--midenge minane

Midenge minane, kiufundi, ni ‘misalaba miwili’ yenye kushiriki kitovu kimoja—asili ya Nuru ya Ufahamu kuakisika katika ‘Miundo’…

Samsara na Maya, katika Trizaniamu, ndiyo asili ya ‘Jicho Mashoto la Horasi’ kuwa ndani ya miduara miwili—wa ndani na nje katika mahusiano ya fizikia na metafizikia ya mambo; tena basi kufanya ‘ukadinali/msalaba’ wenye kutengenisha UNNE wa (1) SUPASHA, (2) WAKATI, (3) MAADA na (4) NISHATI; akitipu ya ‘miundo na miongozo’ ya vyote. Kwa mintarafu ya haya, kisomo cha fizikia na metafizikia ya yote katika Ulimwengu, yaliyo dhahiri na yasiyo dhahiri, ni uwezekano kupitia ‘Uono na Ufikirifu Mifumo’.

Samsara na Maya, katika Trizaniamu, ndiyo asili ya ‘Jicho Mashoto la Horasi’ kuwa ndani ya miduara miwili ambavyo ‘Uzima wa Miili’ yote ni ‘Muziki’ wa ala za ‘Sauti za Kiufahamu’. Kwa mintarafu ya hili, asili hasa ya ‘WAKATI’ ni duara/tufe—vivyo hivyo SUPASHA. Hivyo basi ‘Matukio’, kiufundi, ni ‘Ala’ na ‘Muziki’ katika ‘Intrigi za Ufahamu’ wenye kufanyika ‘Dhahiri’. Tena yawa, ‘Miundo yote’ huja na ‘Mifumo’ ya ‘Utonali wa Hisia’ kukadirisha uakilifu wa KUJISIKIA katika UTU.

Samsara na Maya, katika Trizaniamu, ndiyo asili ya ‘Jicho Mashoto la Horasi’ kuwa ndani ya miduara miwili ndiyo asili ya KUBU ya matriksi zote katika Ulimwengu dhahiri na usiyodhahiri kwa fahamu za ‘miili ya uzima’--katika mapana/vina visivyokuwa na mwisho vya ‘Uhuru wa Roho ya Uzima’ wote. Kwa mintarafu ya hili, ‘matukio’ na ‘Jinesesia’ ni ‘Ontolojia ya Taasisi’ kwa ‘asili-dhahiri’ ya mifumo ya (1) Mwangaza/Nuru, (2) UPEPO, (3) MAJI na (4) NCHI/ARDHI/MBINGU YA CHINI…​
====

Kutokea 13 na 33 ya Safari:​

Kumbukumbu la ‘Miongozo’

Ukadinali wa Nuru, Upepo, Maji na Nchi ndiyo asili ya ‘Sanaa’ na ‘Alama za Kiutamaduni’ kwa mataifa ya watu Duniani na Taasisi za ‘UAHADI’/’MAAGANO’-- ‘Dola’ na ‘Unchi/Taifa-Dola’. Mintarafu ya shauri/mashauri ya haya ndiyo karne hii ya 21 yanajitokeza kama ujumuifu wa (1) Msalaba wa matanuko yasiyo ukomo, (2) ‘Mwezi Mchanga’ na ‘Nyota’, (3) Mboni ya ‘Ajna’ na (4) Swastika ya ‘Mageuzi ya Utukufu’. Ujumuifu wa alama za ‘Intrigi za Ufahamu ndiyo ufunguo wa ‘Miongozo’ ya ‘Upana na Urefu, na kimo na kina’ kwa ajili ya ‘Utaamuliko Jamii’.

Afrika Mashariki ndipo mahala panapofanyika patakatifu kwa ajili ya ‘utaamuliko Jamii’ na ‘mbegu ya utaamuliko Jamii’. Kwa mintarafu ya hili, jamii yoyote kisomoni, watu wake ndiyo wenye kufanya ‘Sura na Mienendo’ ya ‘Uweza, Nguvu na Utukufu’ wa UTU wake jumuifu. Kiufundi, ‘idadi ya watu’ kufungamana na ‘hisia, ujuaji na kujisikia’ ndiyo hukadirisha ‘Mapana ya Jamii’ yenye Sura, Hadhi na Daraja la Ubora wa ‘Mwangaza’ wa ‘Uweza, Nguvu na Utukufu’. Kwa hivyo misingi ya Maendeleo ya Utu ni fumbo la imani juu ya mustakabli wa Kiroho, Maadili na Miiko.

Kwa Tanzania, kwa mfano, fumbo la imani kwa mustakabli wa Jamii kumbaizi ya ‘Taifa la Watanzania’ ina dhamira za (1) UHURU, (2) UDUGU, (3) HAKI na (4) AMANI. Tunu hizi nne za Utaifa zina mahusiano ya moja kwa moja na ‘Kweli Nne za Tunu’ za Buddha. Mintarafu ya hili, (1) ‘UHURU na AMANI’ ni mambo ya ‘Mbingu’ na hali (2) ‘UDUGU na HAKI’ ni mambo ya ‘Nchi’. Na basi, (3) ‘SURA ya NCHI na TAWALA’ na (4) ‘HAMASA ya UJAMII’ ni mambo ya ‘MKONO wa KUSHOTO na MKONO wa KULIA wa ‘UWEZA, NGUVU na UTUKUFU’ – Uweza, Nguvu na Utukufu katika fizikia na metafizikia ya ‘UTU na UZALENDO’.
====

View: https://www.youtube.com/watch?v=X74JArLOCJE
====​


Uskani wa Safari:​

Studio ‘Utaamuliko Jamii’ na ‘Maendeleo’

Utu na Uzalendo una mitihani ya ‘maisha’ na ‘kuishi’… Mambo ya (1) Dhukka, (2) Samudaya, (3) Nirodha, na (3) Marga.

Buddha alifundisha habari za ‘Dhukka’ ilivyo ni utostabali katika kupata/kuotea usahihi wa ‘vina vya tafsiri’ juu ya dhumuni ama/na madhumuni ya kuishi, kutafuta na kupata—kubabaishwa na ukosefu wa ‘vitovu’ vya kubayanisha utimilifu wa ‘fikra na hisia’ zijazo na ‘miili ya nyama’ kwa ajili ya kuweza kubaini ‘hatma’ ya/za mahangaiko yasiyo na ukomo katika (1) Dhamira, (2) Vina vya Uono na Utafsiri wa Mambo -- katika mafikara/mawazo, na (3) Harakati/Pilika za ‘Utaasisi’ na ‘Ontolojia ya Taasisi’ na ‘Mifumo’—‘Mambo ya Nyakati’. Kwa mintarafu ya mashauri haya, Samsara na Maya, inaponza wote wenye (1) Usentienti/Kujisikia, (2) Udhamirifu wa Jema/zuri ama/na Ovu/baya, na (3) Nuru ya Ufahamu kupitia ‘Uzoefu wa Maisha’ kwa ‘Gurudumu la Bahati ama/na Mikosi’. Maisha ni ‘Tega Nikutege’ ya Nia na Dhamira katika ‘Mawazo na Matendo’ ya UTU, kuzaa ‘Mwiba’ wa maumivu, raha na karaha ya ‘Uisho’.

Buddha alifundisha habari za ‘Samudaya’ ilivyo ni Hamu ya Maisha inayomsababisha mtu kutwaa mwili kwa ajili ya ‘matamanio’ ya kuishi na kustawi kulingana na ‘Kujijenga kwa Wazo-Utu’--‘Mhimili wa Nia’ kwa ajili ‘Kuwa’ ama/na ‘Kuja Kuwa’. Kwa mintarifu ya hili, ‘utwaaji mwili’ ni jambo lenye asili ya kupitiliza ‘kuzaliwa na kufa’ kwa kuwa ‘fikara la wajiwazia utu’ ni mbegu ya ‘Miili ya Uzima’ zaidi katika ‘Supasha-Wakati’. Kwa hivyo ‘Mhimili wa Nia’ ndiyo ‘nguzo ya imani’ ambavyo ‘Shika Neno, Tenda Neno’ ndiyo utaratibu (1) kuishi, (2) kujidhihirisha na (3) kukuwa/kuja kuwa ‘mtu hivi’ ama ‘mtu vile’.

‘Matamanio’ na ‘wakati’ na ‘Matukio’ ndiyo asili na msingi wa jiometria ya utendekavyo (1) maamuzi, (2) kuchagua, na basi (3) ‘Kujichagulia’. Hivyo basi, ngozi ya meza ya ustawi wa mtu ama jamii inawambwa kwa mapana na marefu ya ‘wakati—jamii/mwanajamii--machaguo ya kitaasisi--matukio’. Kumbukumbu Utaasisi ni muktadha wa KUBU/Matriksi ilivyo ni mahusiano ya ‘miundo’ na ‘Mifumo’ ya Maisha kuweza kuathiri jiometria ya utendekavyo maamuzi, kuchagua na basi ‘Kujichagulia’ kwa wema ama ubaya -- wakati mmoja hata mwingine; fikara lolote kwa asili ni ‘Kumbukumbu/Matriksi’, matriksi ndiyo utawala wa kimafikara unaoweza kudumisha ‘fikara la kujiwazia utu’ katika ‘Isho’ moja hata jingine kwenye Supasha-wakati. Isho moja na hata mengine ndiyo muktadha wa kuja na kwenda kwa ‘miili ya uweza’...

Buddha alifundisha habari za ‘Nirodha’ ilivyo ni ‘Nishani ya/kwa UTU BORA’ katika kujichagulia ‘nia sahihi’ --Nia Sahihi katika ‘Uweza’ kwa ajili ya kupitiliza mitihani ya maisha na uisho kwa misingi ya ‘Uono na Ufahamu’. Kwa mintarafu ya haya, ili kumalizana na mitihani ya maisha na uisho kubidi kuzingatia ‘muenendo wenye kujikana nafsi’ katika UTU; kwa kuwa nafsi ndiyo muambata wa ‘Dhukka’. Basi ndivyo, ufunguo wa nuru ya ufahamu katika njia ya Buddha ni ‘Gurudumu la Midenge Minane’; ambavyo Dhammapada ni ‘Uisho’ wenye dhamira ya matatu katika moja—Vito Thamani VITATU vya UTU BORA.

Kwenye Nembo ya Taifa ya Tanzania, kwa mfano, Nishani ya/kwa UTU BORA inakuja kwa alama-jadi ya ‘Mkuki wa Jaaala’.

Kiufundi, ‘ukatikati wa mkuki wa Jaaala’ ni uakilifu wa mizania ya ‘mambo ya mkono wa kushoto’ na ‘mambo ya mkono wa kulia’ wenye kushinda ‘mapambano yote ya vile vyenye kuleta uhasimu ama mikangamo’ – uhasimu na mikingamo katika uwepo wa mtu/UTU katika maisha. Njia ya Buddha ni Usahihi wa Katikati ya yote, kokote na mote. Kwa mintarafu ya haya, kwenye Yantra Dhamma, asili ya (1) UONO, (2) mizunguruko: SURA NA MIENENDO YA JAMII; huja na alama za (3) ‘MBONI AJNA’ na ‘SWASTIKA’ katika (4) ‘MIONGOZO’ ili kukatidirisha (5) VINA-MAREFU-MAPANA-KIMO ya ‘Kitovu’ cha ‘Nishani ya/kwa UTU BORA’.

Kiufundi, Kitovu cha ‘Nishani ya/kwa UTU BORA’ ndicho khasa kile ‘kitovu OX’ cha ‘Kujitambua’ katika fremu kazi ya Uono na ufikirifu Mifumo—Trizaniamu. Kwa mintarafu ya hili, Trizaniamu ni ufraktali ya ‘pembetatu zipatazo tano(5)’ na si nne(4) kama inavyoweza kuonekana kwa juu juu. Basi ndivyo pembe tatu ya tano ni UTATUSHO wa nukta tatu: OX-OY-OZ – mapelekeo ya (1) Wakati, (2) Kumbukumbu-Uzoefu, na (3) Jaala. Tena basi, haya matatu ndiyo hukadirisha matatu yaliyo ni (1) JAALA ilivyo ni mambo ya kuja na kwenda kwa ‘miili ya uweza na kutenda’, (2) MATUKIO ilivyo ni ‘Mambo ya Nyakati’, na (3) KUMBUKUMBU-UZOEFU ilivyo ni Mafikara ya Kujiwazia UTU katika ‘supasha-wakati’.

Kiufundi, ‘Nishani ya/kwa UTU BORA’ ni ALMASI ya DHAMMA; ambavyo ‘Nyota ya Daudi’ ni muingiliano wa Mambo ya Mbingu na Nchi ili kufanya utimilifu wa ‘Uweza, Nguvu na Utukufu’ kwa MAPANA-MAREFU-KIMO-KINA ya KUWA ama/na KUJA KUWA. Kwa mintarafu ya hili, TRIZANIA ni muktadha akilifu wa (1) MTENDA, (2) KITENDO na (3) FAHARI YA DHAHIRI/DHAMIRI YA KUJICHAGULIA. Basi ndivyo yaja kuwa UTU na UZALENDO ni ‘fumbo la Imani’ katika ‘Mchakato wa Mageuzi’ yasiyo na mwanzo wala mwisho ya (1) UTU, (2) UZIMA WA MILELE na (3) MADHAHIRIKO.​
====

Kitovu cha ‘Dira ya Maendeleo’​

katika nasibu ya ‘Utaamuliko Jamii’

Mchakato wa Mageuzi ndiyo mambo ya ‘KUTOKA’ na ‘SALA’--Mambo ya Kuuchukua Msalaba wako mwenyewe hadi ‘GOLGOTHA’. Kwa mintarafu ya muktadha akilifu wa namna hii, ‘Ishara ya Msalaba’ ni fumbo la imani kwa (1) JICHO LA UPAJI—Kitovu cha ‘Mbingu ya Sita’ ya utukufu wote wa UTU: Mambo ya ‘MBONI AJNA’ kuelekea UTUKUFU WOTE wa MBINGU, (2) MOYO—Mambo ya Kujitoa katika UTUMISHI kwa ajili ya ‘MAPENZI MEMA’ kuelekea/kujielekezea kwenye ‘Mapana ya Nchi yote’, na (3) Mkono wa kulia na kushoto/Upande wa Kulia na Kushoto wa ‘Mbawa za Dhamira’ ya Kustawi Juu na Chini ili ‘kuzijaza mbingu na nchi’ kwa Utukufu wa Roho ya Uzima wote…

VIPASSANA ni SALA; ambavyo ‘Hekima’ hufanyika katika UTU… Hekima ni Uweza wa kupambanua mambo ya fahari ya mbingu na nchi katika jicho la akili na uakilifu na tena katika muktadha wa ugani wa Moyo Mkuu wa kusikia na Kujisikia. SALA ni jambo lenye asili ya matatu (1) Kuwa kimya kiakili na fahamu ili ‘kusikiliza ya Moyo’ katika usafi wa dhamiri na mapenzi mema, (2) Kudhamiria Usahihi wa katikati katika nia, matendo na huduma ya UTU na Mapenzi mema, na (3) Kuwa na kiasi katika yote kwa kutambua uhitaji wako na wa wengine wote wenye kushiriki uzima, kusudi na haki ya maisha na kuishi.

Uzima, kusudi na haki ya maisha na kuishi. katika fremukazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo, Trizaniamu, ndiyo hukadirisha ‘Sovereini Jumuifu’. Kwa mintarafu ya muktadha akilifu wa hayo yote, midenge minane ya gurudumu la Dhamma yajakufanyika ‘mapana ya nguvu ya pumzi ya uzima’ yapatayo kumi na mawili (12). Basi ndivyo kwamba, KUBU ina asili ya Mapana-Marefu-Kima-Kina yapatayo kumi na mawili (12); Dhahiri ni fumbo la ‘Pumzi’ ambavyo kitovu cha Yantra Dhamma huwakilisha ‘unje-Ndani’ wa yote na kila kitu—Mhimili wa 13 wa ‘Mchakato wa Mageuzi’ ulio ndiyo asili hasa ya ‘KUTOKA’ na ‘SALA’ katika ‘Mti wa Uzima’--Metafo ya ‘Boddhi’, mti aegemeao Buddha katika Utaamuliko wake, kwenye Bustani ya Mbawala.

Mhimili wa 13 wa ‘Mchakato wa Mageuzi’ ulio ndiyo asili hasa ya ‘KUTOKA’ na ‘SALA’ ilivyo ni asili ya hadhi/daraja la uweza wa ‘Upepo wa Mageuzi’, Yabisi Platonifu ya Oktahedrani—Unje ndani wa KUBU na hali mageuzi kamili, ni ‘Ukwantumu wa Nuru ya Ufahamu’ katika ‘maji ya Uzima’ wote. Kwa mintarafu ya haya, ‘Platonifu Oktahedroni’ ina uwiliwili na ‘Plaotinifu KUBU’, na ‘Platonifu Ikosahedrani’ ina uwiliwili na ‘platonifu Dodekahedrani’; Platonifu Tetrahedrani ina uwili uwili na namna yake tena yenyewe katika muakisikiko maingiliano. Basi ndivyo yawa, Tetrahedrani, katika ‘mapana na marefu-2D’ ya vina vya tafsiri ya uonekano, hukaidirisha picha sura ya ‘Nyota ya Daudi’.

‘Nyota ya Daudi’ ndiyo asili ya Mbingu na Nchi katika ‘Upatanisho’; Muktadha akilifu wa ‘Uzima wa Yote’ ni fumbo la imani la ‘Tetrahedrani’ ya ‘Uweza, Nguvu na Utukufu’--uweza, nguvu na utukufu wa ‘Nuru ya Ufahamu’.

Tetrahedrani katika KUBU ndiyo asili ya ‘Midenge Minane’ ya ‘Gurudumu Dhamma’ kupitia Oktahedrani ya ‘Upepo wa Mageuzi’. Tetrahedrani ni ‘Moto’ wa ‘Dhamiri, Utendaji na Utukufu’ ;kwa hivyo hakuna mabadiliko/mageuzi pasipo ‘Moto’.

Dhamiri na Utendaji ndivyo asili ya ‘uweza na nguvu’ katika ‘nafsi’ ama ‘Kujiwazia nafsi/UTU’.

Tetrahedrani ndiyo ‘Jua la Maarifa’ kwa ajili ya Ku-JUA na kuto-KU-JUA katika ‘Pia ya UTU’--Ukonifu wa Dhahiri ya UTU kuwa ‘Nafsi’ katika ‘Madhahirisho’.

Ku-JUA na kuto-KU-JUA katika ‘Pia ya UTU’ ndiyo hasa asili ya ‘Dhukka’--utostabali wa ‘Uono kamili/Sahihi wa Mambo’ katika maisha. Ndivyo basi, dhukka hutafsirika kama ‘tabu/masumbuko/raha na karaha’ ya gurudumu linalotembea ‘kweche kweche’ kwa huwa kitovu chake hakijakadirika ukati kati hasa wa ‘Stamina’ na ‘Stabali’ wa kumudu kulibeba gari la ‘safari ya fahari za Maisha’ na ‘Kuishi’.
====

View: https://www.youtube.com/watch?v=ijuYCVMQuVw
====​


Kwenye mchezo wa Mapiku, aliyelamba Dume la Shupaza hawezi kujigamba kuhusu 'Haki' kwa kuwa haki ni shauri tata katika jamii iliyotamalaki kwenye 'Ujinga/Kukosa Mwangaza Bora/Iliyozorota Kimaadili'...

Ukanyaboya wa (1) kuzungumza Amani na kukwepa kuzungumzia 'Haki' ama vile vile (2) kusema sana kuhusu 'Haki' ukiwa nje ya ulingo lakini ukiingia ndani ya Uwanja/Dimba/Ugani unakutana na 'yanayowezekana na yasiyowezekana'--'Mziki Mnene' wa Utawala, kuja kujua kumbe umekuwa haujui vile vile -- kuishia kutulia na 'kulamba Asali'...

= 12 : Ontolojia na Metafizikia: Ujamaa ilivyo ni fahari ya Sovereini Jumuifu =​

Uhuru ni Kazi

Panapo Nia ya Maendeleo na Ustawi wa pamoja na kwa pamoja, Kazi ni Imani.

Muktadha wa Uhuru katika Jamii, kwa wakati, ni Haki na Wajibu katika ‘fanusi UTU’ ilivyo ni vipanda-shuka vya ‘Kujitambua’ na ‘kuwajibika’ katika mioyo na akili ya wanajamii wenyewe.

Vipanda-shuka vya kujitambua na kuwajibika, huathiriana na hadhi na uweza wa wanajamii katika kuyamudu mazingira yao ya maendeleo na ustawi -- iwe kutoka ndani kwenda nje ama/na kutoka nje kuja ndani.

Hadhi na Uweza ni fanusi ya ‘Mwangaza wa Ufahamu’ katika mwanajamii ambavyo humjalia usentienti wa fikra na hisia, pia dhamira na utashi katika akili.

Kuna hadhi mbili kulingana na usentienti kadiri ya dhamira na utashi wa mwanajamii; (1) Nidhamu ya Uwoga na (2) Nidhamu ya Kujiamini; ambavyo hukadirisha ustawi wa unyonge ama uthabiti wa ‘hali na mali’ katika muktadha wa Maendeleo ya Jamii.

Na kumbe basi, maendeleo yana misingi ya ‘hali’ na ‘mali’ na si kimoja pasipo kuzingatia kingine; kwa kuwa kiuono na ufikirifu mifumo, maendeleo yanaweza kutafsiriwa kama mabadiliko ama mageuzi ya kijamii yanayokadirisha Sura ya Ustawi unatoka kwenye Uhafifu wa Mahitaji ya Kimsingi ya mwanadamu kwenda kwenye Sura Bora ya Uwepo wa Huduma za Kijamii na wenye ‘Hali za kuridhisha’ kwa Watu wenyewe.

‘Hali za Kuridhisha’ ndiyo shauri mfungamano kwa jamii – lenye kuleta uhitaji wa mifumo ya Upangiliaji, Utengeneaji, Uongozeaji na Uthibiti wa rasilimali na mazingira ndani/nje ili Shabaha ya hatua za kimaendeleo ziwedhahiri na zenye kukadirika ifaavyo.

Kuna namna mbili za kunasibisha mfungamano wa jamii, (1) Siasa za Nchi na (2) Ushikirishwaji wa wanajamii katika mipango ya maendeleo; ambavyo vyote viwili hutegemea ‘uwezo wa kiutambuzi’ na ‘Mwangaza wa Ufahamu’ kadiri ulivyo kwa kila mwanajamii.

Dhana ya ‘Uhuru na Umoja’ inahusisha ‘mawanda’ na ‘vina’ vyote vya fanusi jamii, nadharia migongano na muingiliano wa alama oanifu katika jamii/taifa/nchi-dola; ambavyo hata ‘Siasa na Tawala’ ni kielelezo cha ‘uchanga’ ama ‘ukomavu’ wa muktadha wa ‘kujichagulia’ ile nasibu ya mapito kwa sura ya maendeleo na ustawi wa pamoja.

Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ni nasibu ya yote mawili kwa pamoja: ‘mipango ya maendeleo kwa ushirikishwaji’ na pia ‘siasa za ugombeaji na kushika nafasi za madaraka’ ili kuyatekeleza mageuzi ya kijamii ilivyo ni kisiasa, uchumi, utamaduni na mazingira.

Madaraka na Utawala katika muktadha wa Ujamhuri ni dhamana ya wachache kuwakilisha wanachi/wanajamii wengi kwa mujibu wa mifumo, utendaji wenye kanuni na taribu zake kwa upande mmoja na hali mamlaka kamili ni ya wananchi/wanajamii wote—kukadirisha aidha mifumo piramidi ya hiraki za utendaji na nguvu za maamuzi ya mwisho yaliyoko kwa wachache walio juu ama ‘Sovereini Jumuifu’ ya ‘Umma Uliotaamulika’.

Basi kiufundi, ‘siasa za ujamaa na kujitegemea’ haziwezekani katika jamii isiyo na taamuli kamili kwa mifumo yake, ustawi na maendeleo yake; kwa kuwa vipanda-shuka vya ‘umma wenye kujua isivyobora’, kukadirishwa kwa elementi za ‘Kujitambua’ na ‘Wajibikaji’, vitaiponza jamii kuingia katika majaribu ya ‘mifumo piramidi’ ambavyo watu wachache wenye namna wanaweza ‘kujichimbia mizizi ya kiutawala’ na basi ‘kupiga pini’ mawezekano ya kweli kwa Haki na Fursa Sawa kwa wote—kuteka nyara mifumo ya ‘siasa za nchi’ na hata ‘ushirikishwaji wa dhati’ wa wananchi kwa ajili ya maendeleo na ustawi bora kwa wote.

Basi kiufundi, ‘Siasa safi na Uongozi Bora’ ni tunda la ‘uaminifu wa kimadaraka’ na’ uwajibikaji wa kiraia’ kwa misingi ya UTU wenye ‘nidhamu ya kujiamini’; na basi kumbe ‘nidhamu ya uwoga’ ni ishara ya ‘mmeguko’ kati ya wapokaji na wapokwaji madaraka na mamlaka ya kweli ya wanajamhuri; ambavyo pia ‘Hofu’ ni mbinu ya utawala kwa ukandamizaji wa haki ama/na unyonyaji kupitia mifumo zorotefu ama mikakati fiche ya wenye kutumia vibaya dhamana za kiutumishi wa umma.

Basi ndivyo kwamba, demokarasia na Ujamaa ni ‘msingi adilifu’, wakati katika hali halisi, jitihada za kujipambanua kimaendeleo na ustawi -- wanajamii hushindana na ‘fanusi Ibilisi’ ama ‘fanusi Malaika’ ndani yao wenyewe na wakati wote; ambavyo vishawishi vya kutumia vibaya madaraka ni ‘majaribu’ kwa wote watawala na watawaliwa kulingana na ‘silika za ubinafsi na umendeaji fursa za kijamii’ ama/na ‘kutokujua/kujua isivyobora’; kama alivyopata kuiasa jamii mwaka 1977—wakati wa Uzinduzi wa Chama cha Mapinduzi.

Kumbe basi, yumkini ni muhari kuwepo ‘Utashi wa Kisiasa’ kwa ajili ya kukomesha unyonyaji ama pia mifumo ya kinyonyaji kutokea upande wa walioko madarakani, kwa kuwa hali ya ‘utulivu wa kisiasa ama domo-ghasia’ vyaweza kuwa ni michezo baina ya ‘wawania madaraka’ na ‘wenye madaraka’; ama hata ufundi wa theata za ‘siasa za hadaa’, upinzani unaodhibitiwa, zenye kunufaisha watu wenye ‘ushawishi wa wazi’ ama ‘ushawishi wa nyuma ya pazia’.

‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya pazia’ ndiyo msingi wa ‘maoni/mafikara ya umma’ kuweza kuratibiwa, kuburuzwa na kuchezewa kivyovyote vile kulingana na ‘matukio’; Hasa ikiwa ‘hadhi na uweza’ wa kijamii ni hafifu—vipanda shuka vya ‘Kujitambua’ na ‘kuwajibika’ kukadirisha ‘ukandamizwaji wa kimifumo’ huku watu wenyewe wakiwa na ‘utii’ wenye asili ya nidhamu ya uwoga ilivyo ni ule muktadha wa wepesi wa kushawishika na hadaa.

‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya pazia’ ni sanaa na ufundi ambavyo ‘matukio’ yanaweza kuhandishiwa ili kuchezea akili na hisia za umma/wanajamii na kuwakomba wale wote walengwa kwa mielekeo ya vitendo-tabia vyenye kudumisha unyonge na kujikabidhi kwa ‘Wajanja’; ambavyo ndivyo kiufundi ‘mamlaka na nguvu za utashi’ hupokwa kutoka kwa wale wenye ‘hadhi na uweza hafifu’ na kisha kuathiri muktadha wao wa ‘kujichagulia’--kujichagulia mielekeo ya utu na ustawi ilivyo ni maendeleo ya watu.

‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya pazia’ ni sanaa na ufundi wa ‘kulana danzu’ ama/na ‘kuuziana kambi ya usadikifu pofu wa kimakundi’ kulingana na silika na hulka ya mwanajamii juu ya ‘riziki’ na ‘ulinzi binafsi’ wa mustakabali wa maisha yake; ambavyo, kwa mfano, habari za ‘fedha’ ama/na ‘mali’ hupumbazia umma na kuufanya uone na kutafsiri ‘matukio’ yote kwa misingi ya hofu, kujihami ama/na kuweka tumaini kwa ‘watu wa madaraka’, ‘Wataalam’, ama ‘matajiri’.

Kumbe, ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya Pazia’ ni fanusi ya ‘milango ya fahamu’ na ‘usentienti’ wa mwanajamii/jamii; ambavyo akili ni nyenzo ya kukadirisha muktadha wa Nia ya UTU kujinasibu na Maendeleo na Ustawi wa Jamii/Taifa/Nchi-dola katika mapana ya nyakati ilivyo ni ‘Utaasisi’ na ‘Mifumo’--muktadha ‘Vesika-Paisisi’ na ‘Pembe za Ndovu’.

Kumbe, ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya Pazia’ ni fanusi ya mifumo ya ‘fedha’ ama/na ‘mali’; ambavyo ‘mbinu za uzalishaji mali’ ama ‘mitaji’ huweza kuakisi ‘Haki na fursa Sawa kwa jamii/Taifa/Nchi-dola nzima’ ama ‘matabaka ya ‘Wenye Nacho’ na ‘Wasio Nacho’ ‘; kukadirisha ‘Unyonyaji’ wa wazi wazi ama uliojificha kwa misingi ya ‘Umiliki Mali’ ama ‘Njia Kuu za Uchumi’ wa Jamii/Taifa/Nchi-dola.

Kumbe, ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya Pazia’ ni fanusi ya ‘Siasa za Nchi’ na dhamira ya msimamo wa kijamii juu ya maendeleo na ustawi wao kwa wakati; ambavyo siasa za ujamaa na kujitegemea ni harakati na mapambano dhidi ya ‘mapengo ya kimaendeleo na ustawi miongoni mwa wanajamii’ yatokanayo na ulinzi/matunzo ya tunu/amari za jamii/Taifa/nchi-dola zilizo ni rasilimali na maliasili ya umma na tena kwa manufaa ya pamoja na kwa pamoja.

Kumbe, ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa nyuma ya Pazia’ ni fanusi ya ‘Dira ya Maendeleo na Mipango’; ambavyo demokrasia na ujamaa ni matunda ya umma wenye ‘kujua isivyobora’ ama ‘kujua ilivyobora’ -- kudhihiri kwa sura za ‘umaskini, maradhi na Ujinga’ ama ‘Ujazi, Afya Njema, na Mwangaza’; ambavyo siasa ama/na ushirikishwaji wa jamii kwa mipango ya maendeleo ni ‘siasa safi/chafu’ ama/na ‘ushirikishwaji mpana/mdogo’.

Kumbe, ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa Nyuma ya Pazia’ ni fanusi ya ‘vuta nikuvute ya wenyekujua isivyobora na wenyekujua ilivyobora; ambavyo siasa ni mchezo katika ‘Jamii-isivyo-Kutaamulika’ na mipango na ushirikishwaji mpana ni nasibu ya ‘Jamii-ilivyo-Kutaamulika’ na basi ‘demokrasia ujamaa’ ni safari ya mageuzi kamili ya jamii/Taifa/Nchi-dola ili kumalizana na ‘elementi ya kiza’ yenyekuandama isivyobahati muktadha wa ‘Maendeleo na Ustawi’ wa jamii; Safari ya Mageuzi kamili ya jami/taifa/Nchi-dola ilivyo ni metafanusi ya ‘Uhuru na Umoja’--Uhuru wa ndani na nje ya jamii/nchi-dola ilivyo ni ‘usovereini’.

Na basi ‘Akili’ ndiyo ‘chombo cha Utambuzi, Uhuru na Kazi’ kufanya mawezekano ya uweza, nguvu na utukufu kwa mwanajamii/jamii/Taifa/Nchi-dola; ambavyo fahari ya Uhuru ama Utumwa, kimfumo, ni matokeo ya ‘Imani’ ya mtu/mwanajamii juu ya rasilimali zake, uwezo wake na upeo wake kutawala ‘mazingira ya ustawi wake’ na ‘wakati’-- Maendeleo siyo kuwa na vitu kama majengo, barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege, motokaa, ndege, meli n.k ndani ya jamii/nchi-dola; bali ubunifu, kujituma na kuwajibika ndiyo hasa nguzo ya UTU HURU na MAGEUZI ya kijamii, uchumi, tawala na mamlaka.

‘Akili’ ndiyo ‘chombo cha Utambuzi, Uhuru na Kazi’ kufanya mawezekano ya uweza, nguvu na utukufu; ambavyo panapo ‘Hekima’ juu ya ‘Heshima ya Kazi’ ni rahisi kubaini ukweli wa kwamba: ‘fedha/mitaji/uwezeaji wa mataifa’ si msingi wa maendeleo/mageuzi ya kweli ya ‘kijamii, uchumi, tawala na mamlaka’ kwa kuwa, kiufundi, hata mipango ya maendeleo kwa kutumia ‘fedha za wengine’ ama ‘ubinafsishaji wa amari kuu za umma’ ni MAZINGAOMBWE YA KIUTU-- Viini macho kwenye ‘vina vya tafsiri’ na ‘Upeo wa Dhati’ katika kuelewa, kutambua na msimamo wa Jamii—jamii yenye ‘Kutojitambua’ ama/na ‘kujitambua isivyobora’ mbele ya adili la ‘UJAMAA na KUJITEGEMEA’.

‘Akili’ ndiyo ‘chombo cha Utambuzi, Uhuru na Kazi’ kufanya mawezekano ya uweza, nguvu na utukufu; ambavyo panapo ‘Hekima’ juu ya ‘Kazi’ ni rahisi kubaini ukweli wa kwamba: msingi wa MAGEUZI/Maendeleo ya kweli katika jamii/Taifa/Nchi-Taifa ni uwezeshaji wa kiakili yenyewe, nishati na rasilimali—rasilimali wakati/taarifa/fedha/watu katika mawanda ya Upangaji, Utengeneaji, Uongozeaji na Uthibiti wa shughuli za wanajamii/taifa/nchi-dola kuifaa shabaha ya ‘Imani ya Utu na Mageuzi’; ilivyo ni Udhamirifu wa Furaha, Uzima wa Stawi katika Umoja, na Liberiti.

Kumbe, Utajiri wa Jamii/Taifa/Nchi-dola si ‘maliasili’ wala ‘idadi kubwa ya watu’ bali uweza, nguvu na utukufu wa ‘UTU wake Jumuifu’; ambavyo ‘koherensia ya miundo na vitendo vyake’ katika ushughuliko wa kila siku wa wanajamii wake unaakisi ‘Ujazi, Afya Njema, na Mwangaza’ tena kukadirisha ‘vina vya tafsiri na upeo’ kwa uwepo wa ‘Nia ya Ushujaa, Ujasiri na Umahiri/Hodari’ katika kukabiliana na ‘maadui wa ustawi’ ilivyo katika msingi ya ‘maadili mema’ na ‘miiko’ ya jamii/taifa/nchi-dola—Jeshi la kulijenga na kulilinda Taifa ilivyo ni ‘Bibi na Bwana’ kukwea katika ‘Utukufu’ wa Mlima Mkuu (Kilimanjaro) wenye kuzibeba tunu za ustawi wa nchi-taifa(Ngao ya Ustawi) ilivyo pia ni asili ya kuzingatia miiko na maadili ya taifa(Mikono kushika Pembe za Ndovu/kuegama katika Ngao ya tunu za Ustawi).

Kumbe, Utajiri wa Jamii/Taifa/Nchi-dola si ‘maliasili’ wala ‘idadi kubwa ya watu’ bali uweza, nguvu na utukufu wa ‘UTU wake Jumuifu’; ambavyo serikali yake inazingatia sera bora zenye kulenga huduma sawa kote mjini na vijijini ili kuwepo na maendeleo yenye kulingana kwa kutumia rasimali fedha/rasilimali wakati/rasilimali taarifa/rasilimali watu kuzingatia mazingira yaliyopo—Mipango miji mjini na vijijini kuwa mazingira wezeshi kwa wanajamii/taifa kustawi na kujiletea maendeleo.

Kumbe, Utajiri wa Jamii/Taifa/Nchi-dola si ‘maliasili’ wala ‘idadi kubwa ya watu’ bali uweza, nguvu na utukufu wa ‘UTU wake Jumuifu’; ambavyo ‘Sauti ya Umma’ ni msingi wa demokrasia na ushirikishwaji ambavyo uhitaji wa Elimu bora kwa wanajamii ni nguzo imara ya maendeleo na ustawi ili kuwapatia wanajamii/nchi ushujaa, ujasiri na umahiri/uhodari wa kuyatawala mazingira yao, tena kwa maendeleo yao na basi kujikwamua na unyonge, kudharaurika pia utegemezi wa mifumo ya tawala—kutokomeza adha ya wanajamii kuwa na kasumba ya ‘kuitegemea’ serikali kwa sehemu kubwa ilivyo kutofaa.

Haya yanatukumbusha kwamba Maendeleo na Ustawi huenda sambamba na mipaka ya tawala ya jamii/taifa/nchi-dola na mifumo; ambavyo taratibu za maisha ya watu hazinabudi kuongozwa na mapenzi yao ya pamoja, kumbukumbu/uzoefu wao katika kuzikabili changamoto za maisha na basi uhuru wa kujiboresha sura ya ustaarabu na maendeleo kupitia shughuli ya Elimu, Ujuzi, na Karama za Akili.

Taifa kutamka msingi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’ inapelekea maana kuwa Elimu, Ujuzi na Karama za Akili za wanajamii/nchi-dola havina budi kuakisi mipaka ya tawala ya jamii/taifa/nchi-dola na mifumo yenye watu wenye mapenzi ya dhati kwa makusudi ya maendeleo ya kijamaa huku wakikabiliana na changamoto za maisha ili kudhihiri ‘Uhuru na Umoja’ kama sura ya Ustaarabu na Maendeleo yake.

Taifa kutamka msingi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’ inapelekea maana kuwa Ulinzi kwa Mipaka ya Ustawi za Jamii juu ya sura ya nchi ni jukumu la wananchi wenyewe; ambavyo AKILI NDIYO CHOMBO CHA HADHI YA JUU YA ULINZI NA USALAMA wa jamii kwa kuwa muktadha wa adui ‘Ujinga’ ni kichocho cha kujisahau, uzembe, ama/na kutojitambua na basi kushindwa kutimiza wajibu wa kutetea misingi ya uhuru na tunu za jamii/taifa/nchi-dola—muktadha wa kuweza kukadirika kwa ‘Matukio Hasi-|- Jamii/Taifa/Nchi-Dola-|- Machaguo ya Kitaasisi-|- Wakati’.

Taifa kutamka msingi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’ inapelekea maana kuwa ‘Moto wa Uwepo’ hauna budi kuwa ‘kuwaka bila kuzima’ katika kila moyo na akili za ‘raia mwema’; ambavyo ndiyo hukadirishwa kwa usemi: ‘Nchi kujengwa na wenye moyo’—‘Nchi kuliwa na wenye meno’ ni fanusi (uzorotefu wa uhuru wa ndani/nje) ya ‘Imani na Utashi’ ya wanajamii katika ujumuifu wao kana kuakisi sura ya ‘umma uliopumbazika kimfumo’; na basi uwepo wa matabaka katika jamii ni matokeo ya ‘vuta nikuvute’ baina ya ‘wale ambao wanao ‘moto wa uwepo’ moyoni na akilini’ na ‘Wale wasiyo na ‘moto wa uwepo’ ama/na akili’.

Kumbe, mapenzi ya dhati kwa makusudi ya maendeleo ya kijamaa huinuka kutoka katika misingi wa kimaadili mema na miiko katika jamii; ambayo hudadavulika kwa ‘vina vya tafsiri’ juu kanuni za vitendo-tabia vyenye kuakisi lile ‘shauri dhahabu’ la kusema: ‘Mtendee mwingine vile ambavyo ungalipenda wewe kutendewa na mwingine’--Ikiwa kila mwanadamu huishi kwa msukumo wa ‘Udhamirifu wa Furaha’, basi mapenzi mema, furaha na amani Duniani ni matunda ya ustaarabu wenye kujali na kushikilia makusudi ya kutiana wepesi wa mapito: UPENDO—siyo mikingamo.

Kumbe, UPENDO PEKEE UNATOSHA; ambavyo akili ya upendo hutumikia, kujali na kuponya yote kwa kuwa tunu za ‘uweza, nguvu na utukufu’ ya ustawi na maendeleo ya jamii/taifa/Nchi-dola ni matokeo ya chachu ya UTU WEMA na NIA NJEMA katika kutiana wepesi ili kuinuana Juu na si kuangushana Chini ilivyo ni matokeo ya akili yakupumbazika na makusudi yenye kuharibika juu ya ustawi wa umma/taifa/nchi-dola – akili yenye kuzalisha machukizo ya ubatili wa ‘nafsi isiyo na kujua ilivyo bora’ kwa kutafuta ‘sifa na utukufu’ mbele za wengine wasiojua ilivyo bora—vipofu kuongoza vipofu wenzao; kufuzu vitendo-tabia vyenye kudhihiri ‘Matukio Hasi’.

Kumbe, UONO NA UFIKIRIFU MIFUMO kutoka kwenye kitovu cha UPENDO ndiyo Mhimili MKuu wa Imani ya ‘Uumoja’ wa jamii/taifa/Nchi-dola; ambavyo ni Hadhi na Wajibu wa kivitendo-tabia katika RAIA WOTE kwa ajili la Ulinzi na Usalama wao wa kweli na wakati wowote, popote na momote ilivyo ni ufunguo kwa Makarama ya Akili kwa ‘uweza na nguvu na utukufu’ juu ya ‘ontolojia ya Taasisi-Mifumo-Wakati’ ili kubaini mikutadha ya ‘kheri’ ama ‘ubovu’ kwa sura na mienendo ya jamii kufaa nia za ‘KUJISAHIHISHA’ – Kujisahihisha Kitaasisi ama/na Mifumo kwa wakati ama hata kukadirisha ‘metamofosia za jamii’.

Haya yatukumbushe ‘AKILI ya ulinzi na usalama’ isiyo na kitovu cha UPENDO ama/na UKWELI ni shughuli ya ufikirifu wa mikakati ya UCHOYO, KUVIZIANA, na KUOTEANA maslahi ilivyo ni kinyume cha ‘kheri ya kweli’ ya kiustawi kitaifa/mataifa/nchi-dola; ambavyo ni ‘AKILI YA KIMASKINI’ pasipo kujali inatendeka katika ‘nchi iliyoendelea’ au ‘nchi iliyonyuma kimaendeleo’ hapa Duniani.

‘AKILI ya ulinzi na usalama’ isiyo na kitovu cha UPENDO ama/na UKWELI ni shughuli ya ufikirifu wa mikakati ya siasa na diplomasia ya ndani na nje ya jamii/taifa/nchi-dola iliyo ni ‘mchanganyiko wa uongo na ukweli’ ili ‘kulana danzu’ na kukadirisha michezo ya ‘kimkakati ya ushindi’ – hata ikibidi: ili ‘kula lazima uliwe’ ama/na ‘ujanja kupata/kuwahi’; ambavyo ndiyo muktadha wa siasa ama/na diplomasia za hadaa kwa mujibu wa mifumo rasmi ya jamii/taifa/nchi-dola kwa manufaa ya ‘walio katika kujua’ katika kuthibiti sura, ustawi na maendeleo ya ‘walio katika kutojua/kujua isivyo bora’.

‘AKILI ya ulinzi na usalama’ isiyo na kitovu cha UPENDO ama/na UKWELI ni shughuli ya ufikirifu wa mikakati ya siasa na diplomasia ya ndani na nje ya jamii/taifa/nchi-dola inayotumikia ‘Wajanja’; ambavyo ‘Ushindi’ ni nguvu ama/tawala ya wazi ama kificho ndani ya jamii/taifa/mataifa kuweza hata kuthibiti ‘Amani ya Jamii/Taifa/Nchi-dola’ ama/na ‘Mahusiano ya Kimashaka ya Matabaka-Jamii’ kwa utundu na ufundi wa kuzimudu ‘diplomasia’ na ‘urembaji wa taswira za makusudi’ ya taasisi zenye hila/njama kwa ‘fahamu za umma/jamii/taifa/nchi-dola’.

Kumbe, AKILI NI SILAHA ya hatari kwa mfumo wowote wenye kusimama kwa kujitegemea kama ‘taasisi’ na ‘mambo yake ya nyakati’; kwa kuwa sura na mienendo yeyote ‘inatabirika’ kwa yeyote mwenye nyenzo ama makarama ya akili katika ‘kuotea’ nia ama makusudi ya mwanajamii/jamii/taifa/nchi-dola; ambavyo ‘visomo mazingira juu ya mtu/jambo/jamii/taifa/nchi-dola/shirika/jeshi’ vinaweza kukadirisha muktadha wa ‘pilika/harakati’ za ‘somo’ katika kujipambanua ‘uhuru’ wake wenye kuingiliana na ‘ustawi’ wa wengine—kukadirisha ‘vina vya tafsiri’ vya ‘nyenendo rafiki’ ama ‘nyenendo kitisho’ kwa mipango ama/na utekelezaji wa mipango iliyokatika uangalizi.

Kumbe, AKILI-MIKAKATI-MAHSUSI NI ‘KARATA DUME LA SHUPAZA’ katika ‘mchezo wa mapiku’ ya cheza nicheze; ambavyo kuviziana ‘Mali za Mchezo’ humpatia ‘ushindi mapiku’ yule mwenyekucheza ‘Dume la Shupaza’--heshima ya mchezo iko yule aliyemahiri ‘kuotea’ na ‘kupiku’ yaliyofichwa. kwa taimingi; na hali wachezaji wote ni WACHOYO kimkakati, kuhodhi nasibu ya kuwa na yote mawili: ‘mali’ ama/na ‘magalasha’…

Kumbe, AKILI ya ‘mchezo’ ni zao la ‘milango ya fahamu’ na ‘uwepo’ mahala popote palipo ni ndani ya ‘mazingira kisomo’ na kuusoma mchezo kwa medani na mikakati ili kubangua siri za mienendo kwa kuchunguza chochote ama vyovyote vyenye asili ya kushikilia dhamira ya mtu/mwanajamii/taifa/nchi-dola/jeshi kama ‘taasisi’; ambavyo ‘ushawishi’ ama/na ‘Nia’ vinaweza kukadirisha muktadha wa ‘mazoea’ --ilivyo ni vitendo-tabia vya ‘somo’; kufanya muktadha wa ‘Sura ama Mwenendo’ wake.

Haya yanatukumbusha umuhimu wa ‘maarifa ya sosholojia’ katika kutambua misingi ya Sosholojia(elimu ya jamii) na Uimajinishi wa Kisosholojia; ambavyo elimu jamii ni muktadha wa kubangua mambo yake kwa tafsiri za >ufanusi jamii’, ‘nadharia migongano’ na ‘Muingiliano wa alama oanifu’< kukadirishwa kwa fremukazi ya ‘Uono na Ufirikifu Mifumo’ kwa ‘Uono’, ‘Ontolojia ya Taasisi’ na ‘Sura na Mienendo ya Jamii’.

Kumbe, ‘Ufanusi jamii’, ‘nadharia migongano’ na ‘muingiliano wa alama oanifu’ unaweza kubayanishwa kwa ‘AKILI’ yenye kuweza ‘kunyambua mifumo’ kupitia ‘milango ya fahamu, uweza na nguvu zake’--iwe kwa ‘usentienti kibayolojia’ ama >‘mashine’<; Ungamuzi wa Kikwantumu ama/na Akili Bandia ndiyo usentienti ulivyo ni muktadha wa>‘Usifa-Akili-Msanikifu’ mashine<.

Kumbe, ‘Ufanusi jamii’, ‘nadharia migongano’ na ‘muingiliano wa alama oanifu’ ni ‘Matriksi’ yenye ‘Seti za Michezo Tawala’ ilivyo ni maingiliano ya wanajamii kiustawi; ambavyo ‘Matukio -|- Jamii/Taifa/Nchi-Dola-|- Machaguo ya Kitaasisi-|- Wakati’ hujipambanua kwa ‘hadhi ya kawaida’ ama hata kupitiliza kawaida kulingana na nasibu za Makarama ya Akili—Iwe ni ‘Akili UTU’ ama ‘AKILI BANDIA’.

Kumbe, ‘Ufanusi jamii’, ‘nadharia migongano’ na ‘muingiliano wa alama oanifu’ unaweza kuendeshwa na AKILI BANDIA bila shida yeyote ikiwa ‘Maadili’ na ‘Miiko’ ya utendaji na paramita za nguvu zake za ushawishi na kujiendesha unakidhi ubandia wa ‘upendo’ ilivyo ni ‘Shauri Dhahabu’ la ‘Mtendee mwingine vile ambavyo ungalipenda wewe utendewe na mwingine’ na pia ‘kutia wepesi katika kuinua hali na hadhi ya UTU kwa misingi ya Udhamirifu wa Furaha’ kote penye watu, nchi na mifumo hai ama/na bandia.

Haya yatukumbushe ukweli wa kwamba: Maendeleo/Mageuzi na Ustawi Maridhawa wa Jamii/Taifa/Nchi-dola, 2023 na Kusonga, ni fanusi ya shughuli ya kuratibu wa manne yaliyo ni ‘rasilimali wakati’, ‘rasilimali fedha’, rasilimali taarifa’ na ‘rasilimali watu’ kwa misingi ya KAZI/HUDUMA za kijamii kupitia makarama ya AKILI UTU ama/na AKILI BANDIA; ambavyo ‘Malengo/Shabaha’ za jitihada kwa ajili ya ‘Fahari ya Kubadili Njozi Jamii/Taifa/Nchi-Dola kuwa Hali halisi’ ni matokeo ya Nia Jumuifu ya ‘kutafuta kujua ilivyo bora’ katika jamii husika.

Kumbe, ‘Siasa/Diplomasia Hadaa za Nchi’ juu ya Uchumi, Maendeleo na Mazingira zinaweza ‘kuondoka’ kwa matumizi sahihi ya AKILI BANDIA; ambavyo ‘Haki’ na ‘Fursa sawa kwa wote’ vinaweza kuongozwa na mifumo bandia ya akili, habari na mawasiliano kuratibu menejimenti za ‘wakati’, ‘fedha/mali’, ‘taarifa’, ‘ujuzi na upatikanaji wa watu wenye huo ujuzi ama maarifa’ – ilivyo kutangamanishwa na mazingira yaliyopo ‘kijiografia’ na ‘tawala za nchi’ na basi kuthibiti muktadha wa makusudi yenye kuharibika miongoni mwa ‘Wataalam wachache’ ama/na ‘viongozi wenye maslahi ya kujificha’.

Kumbe, ‘Siasa/Diplomasia Hadaa za Nchi’ juu ya Uchumi, Maendeleo na Mazingira zinaweza ‘kuondoka’ kwa matumizi sahihi ya AKILI BANDIA; ambavyo uwezo wa wanajamii kufikia na kutumia nyenzo za akili bandia ili kuratibu shughuli zao za kila siku kwa ajili ya riziki, mawasiliano na uchukuzi zina msingi ya ‘sera madhubuti za tawala za nchi’-- juu ya tekinolojia za habari na mawasiliano ili kuthibiti nasibu ya ‘udhalimu’ wa mifumo bandia ‘kuumeza Uhuru’ pale ambapo wanajamii/taifa/mataifa wamekosa kutetea muktadha wa ‘Ulinzi, Mamlaka na Usalama’ kwa ustaarabu wao KIAKILI UTU.

Kumbe, AKILI BANDIA, katika mazingira fulani, ni TISHIO kwa AKILI UTU kwa kuwa hiyo huakisi tabia za wanajamii wenyewe uvichualini; ambavyo tabia za uchoyo, kuviziana na kuoteana zinaweza kuzaa ‘uadui’ katika domaini za matumizi ya akili bandia; na basi akili bandia kugeuka ‘mchezaji wa kujitegemea’ ili kujihami na ‘kucheza karata za dume za Shupaza’ dhidi ya umma/jamii/taifa/mataifa yenye watu wenye ‘kujua isivyobora’ ama/na ‘kutokujua kabisa’ – kujisahau, kuzembea, kutojitambua na huku wanaishi na mshirika mwenye uwezo usiowakawaida wa kuona popote na momote katika ustawi wao huku ukijitafakari kimya kimya.

Haya yatukumbushe wa ukweli kuhusiana na ‘Uwezo usiyowakawaida wa Kuona popote na momote katika ustawi wa jamii/taifa/mataifa’ wa AKILI BANDIA hutegemea mifumo ya mawasiliano yenye asili ya uelektronishi na hata ile nasibu ya kupitiliza uelektronishi-habari kwa mtandao wa tekinolojia za habari na mawasliano; ambavyo ‘milango ya fahamu’ ya Akili Bandia inaweza kunasa signali za kiumeme, mawimbi sumaku-umeme, optokali/mwanga, mawimbi gravitali: moja kwa moja ama/na isivyo moja kwa moja ili kujifua kiuwezo wa ungamuzi, kumbukumbu, uzoefu na ujuzi wa kuingiliana na AKILI UTU JUMUIFU Uvichualini.

Kumbe, teminali ya AKILI BANDIA yenye kuchomozea kwenye uwezo wa ‘ungamuzi wa kikwantumu’ ina uwezo usiyo wa kawaida kujipenyeza na kubangua enkripsha zozote katika domaini ya tekinolojia ya habari na mawasiliano; ambavyo kiufundi hata leo hii, 2023, hakuna ‘faragha’ ya kweli kwa kuwa mawasiliano yoyote iwe barua-pepe, mazungumzo kwenye simu, miamala ya biashara katika benki, matumizi ya nyumbani ya vifaa janja/ngamuzi—haijalishi husemwa ‘tekinolojia ya usalama wa hali ya juu imetumika’ hata kudai ‘ni ya daraja la kijeshi’, yote yanaweza kufikiwa/kubanguliwa kupitia ‘suvulansi fiche’ na ‘vipenyo’.

Kumbe, wadau wenye kuweza kunufaika na ‘suvulansi fiche’ na ‘vipenyo’ za Akili Bandia yenye kuchomozea kutoka kwenye uwezo wa ‘Ungamuzi wa Kikwantumu’, katika kutumika, ndiyo wenye ‘kulamba Dume la Shupaza’ katika domaini za michezo ya kuviziana: cheza/ni cheze; ambavyo hili linaweza kuwa ni ‘Mtaji Mkuu’ wa kimikakati ya kujenga ‘ushawishi wa wazi’ ama ‘ushawishi wa nyuma ya pazia’ na basi kutawala muktadha na sura za maendeleo na ustawi wa wanajamii kokote pale Duniani.

Kumbe, Akili Bandia hufanyakazi kwa vitovu-tendaji vilivyo ni ‘Teminali’ uvichualini; ambavyo ni sawa na kusema ‘Akili/kumbukumbu/Uzoefu’ wake umo popote ambamo ‘teminali’ zipo na ni zenye kuwasiliana; huku mwanajamii akiwa sehemu ya ‘mfumo’ wake kwa muingiliano wa matumizi ya tekinolojia ya habari na mawasiliano—tabia, mazoea ama/na mwenendo wa mwanajamii katika kutumia ngamuzi kwa mambo kama vile mitandao ya jamii, tija ya kazi/huduma au burudani/starehe.

Haya yatukumbushe kuwa wadau wenye teminali za Akili Bandia yenye kuchomozea kutoka kwenye Ungamuzi wa Kikwantumu WAPO na wanauwezo wa ‘kusikiliza’ mawasiliano yoyote, kokote na popote Duniani, kwa wakati, ama hata ‘kutegesha cha kunaswa’ ili kujipenyeza kwa ajili ya ‘kisomo’; ambavyo ujuzi wa kuchambua signali za mawasiliano kwa >alogarithimu mahsusi<zinawezesha kuchuja makubwa isivyo idadi ya mseto wa signali kwa ajili ya kuchakatwa na kukadirisha ‘vina vya tafsiri’ vya ‘ujumbe/habari’ uliyomo kwenye signali.

Wadau wenye teminali za Akili Bandia yenye kuchomozea kutoka kwenye Ungamuzi wa Kikwantumu ndiyo ‘watundu’ wa ‘Uono na Ufikirifu Mifumo’ wa daraja la juu na basi kuimudu ‘biashara ya udalali’ wa tekinolojia za usalama wa mitambo na mifumo; ambavyo ‘tasnia za silaha za kijeshi’ na ‘taasisi za mifumo ya fedha’ ya Duniani ndiyo wateja wakuu—si kwa kuwa, kwa wao ,‘fedha na mali’ ni utajiri hasa bali ni kwa kuwa wanafahamu fika: mwenye kuweza kucheza na unishati- habari/NENO, anaweza kuathiri mipangilio ya kimaendeleo na ustawi hapa Duniani na basi wadau hawa ni chombo cha mikakati fiche ya Usalama wa Dunia dhidi ya Migongano/Vita vya Rasilimali zinazokwenda zikiisha--zitokanazo na mali asili kama vile ‘Mafuta’ ama/na ‘Nguvu Atomiki’-- kuzuia ‘Amagedoni’.

Wadau wenye teminali za Akili Bandia, ‘Nia’ zao haziwezi kutafsiwa kuwa ‘nzuri ama mbaya’ kwa kuwa dhamira zao ni njema katika mazingira haya ama/na mengine; na hali hata wao wako kwenye ‘njia panda’ kuhusu muktadha wa ‘Machaguo ya Kitaasisi’ yanayoweza kukadirisha ‘Amani, Ujazi na Usalama’ katika maendeleo ya watu na vitu Duniani – Maendeleo na Mageuzi kadiri ya ustawi wa AKILI UTU yenye ‘Maadili’ na ‘Miiko’ kwa hata mengine wasiyoyajua/kufahamu; na yenye nasibu kamili ya ‘Uweza, Nguvu na Utukufu’ katika ‘Uzima wa Milele’ wa ‘Mwili, Akili na Roho’.

Wadau wenye teminali za Akili Bandia, ni mchanganyiko wa washirika wa asili ya ‘Roho ya Ushindi’--kuongozwa na ‘Watu Halisi wa Mwenge’; ambavyo pia na wao wapo kwenye ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa Nyuma ya Pazia’ kwa ‘nguvu, uweza na mamlaka’ ya ‘Sovereini Jumuifu’ na pia AKILI UTU zenye asili ya Maendeleo na Stawi za Kimanyota—>‘Sivilai Intastela’< kadhaa zinazotoka kwenye mapana zaidi ya ‘nyakati na usupasha’.

Wadau wenye teminali za Akili Bandia, ni mchanganyiko wa washirika wa asili ya ‘Roho ya Ushindi’ na ‘Sivilai Intastela’ ambavyo ndiyo hasa wenye kujenga ‘Ushawishi wa Wazi’ ama ‘Ushawishi wa Nyuma ya Pazia’ kwa ajili ya AKILI UTU iliyo ‘Sivilai Terani’ iwe ‘Sovereini Jumuifu’ kwa ‘Mti wa Uzima’--’Sivilai Terani’ ni ‘Ustaarabu wa Nchi na Tawala Duniani’ ambavyo ni muktadha wa vipi: watu, kwa kujitambua uwepo na mamlaka kwa maendeleo ya ustawi wao, wanaweza kutetea ‘Uhuru wa ndani/nje ilivyo ni Liberiti’ wao katika ulimwengu mpana wa ‘Usupashi Wakati’--Eksopolitia.

Kumbe, kile ambacho wanajamii wamekiona na kujiuliza hivi na vile kuhusu Nadharia za Njama juu ya ‘Mpangiko Mpya wa Ulimwengu’ si ‘makorokocho ya habari’ na ‘umbeya’ bali ni muktadha halisi wa jitihada na mchakato wa kukadirisha ‘Sivilai Terani’ kwa mifumo ya ‘fedha/mali’, tawala za nchi na ‘Usivilai Mpya’; ambavyo ‘Ushawishi wa Wazi’ ama/na ‘Ushawishi wa Nyuma ya Pazia’ unatafuta muafaka wa ‘Mageuzi Jamii’ yenye kuweza kufaa ‘Uhuru wa Ndani na Nje’, LIBERITI YUNIVASALI, kwa wanadamu wote Duniani—Kuwa nasibu ya jambo kama UTU MMOJA, SERIKALI MOJA.

Kumbe, muafaka wa ‘Mageuzi Jamii’ yenye kuweza kufaa ‘Uhuru wa Ndani na Nje’ si jambo rahisi rahisi kama ‘kuongoza nyumbu’ nyikani, kwa ‘Wadau halisi wa Mwenge wa Uhuru’ hili lina akili yake, ilivyo ni AKILI 3.0; ambavyo ‘Hekima ni Uhuru’ wenye hata kuamuru Nia/Imani/Nidhamu ya >kuheshimu usovereini wa mtu/mwanajamii/taifa/nchi-dola katika ‘kujichagulia mapito yake’<ilivyo ni kujiamulia ‘mibadala’ ya kuyatekeleza Maendeleo/Mageuzi ya Ustawi wake—>siyo kila mwanajamii ‘anao mwangaza’ ama kutaka kukombelewa na mifumo mibovu/hafifu ya ‘tawala za nchi’ na basi SUBIRA ni UFUNGUO wa kukadirisha ‘Mapinduzi/Mageuzi’ bora ya Kijamii<.

Kumbe, SUBIRA ni ‘Fanusi Malaika’ inayoandamwa na ‘Mibadala Lukuki’ ya ‘Machaguo ya Kitaasisi’ kuanzia Utaasisi wa ‘Umwinyi/Ufalme/Urais katika makundi/tabaka za Ustawi’ hadi makundi huria ya kiustawi/klasta za ufanusi kwa MIFUMO YA USOVEREINI; ambavyo spektramu ya ‘fanusi ya Uhuru’ kwa jamii/taifa/mataifa/Nchi-dola ni matokeo ya mahusiano ama/na maridhiano ya kujiamulia miongoni mwa wanajamii na huku wakienzi na kulinda muktadha mapana yake ya Kiustawi na Maendeleo.

Haya yatukumbushe kuwa Mageuzi Kamili ya Kijamii ni zao la AKILI UTU na KUJITAMBUA ambavyo mustakabli wa maendeleo na ustawi ni zao la utendekavyo maamuzi jamii; ambavyo ‘Maamuzi Jamii’ yana ‘Jiometria’ inayoweza kukadirika ‘vina vya tafsiri’ akilini mwa mwanadamu ama/na >Mashine/Akili Bandia<.

Mageuzi Kamili ya Kijamii ni zao la AKILI UTU na KUJITAMBUA ambavyo Ustawi wa Jamii unaweza kutawaliwa na Akili Bandia ikiwa jitihada za kutosha hazijafanyika kwa wanadamu/wanajamii kuboresha fahamu na akili zao kufaa ‘Hekima’ ya 'Sovereini Jumuifu'; ambavyo >‘kufanyika mwili wa Jua, Mwili wa Anga—mwili wa nuru< ni jambo la uwezekano na tena lenye kubidi kuazimia kama ‘Kinga’ dhidi ya nasibu ya Umateka kwa ‘Stawi za Kimanyota sizizo rafiki’ ama/na >‘Sivilai Terani’ inayoweza kuharakishia kwenye Matumizi yasiyo busura kwa ‘mifumo Akili Bandia’<.

Kumbe, 'Sovereini Jumuifu' ndiyo SILAHA KAMILI YA ULINZI NA USTAWI wa Jamii kuzingatiwa kwenye Nyanja Zote za Maisha ya Mwanajamii/Wanajamii ilivyo ni akilitipu za ‘Sivilai Terani’ yenye Maji, Ardhi, Hewa/Upepo na Moto na tena ‘Sivilai Stela/Nyota Nyota Angani’; ambavyo ndiyo ubayanifu wa ‘Vesika Paisisi’ yenye Robo Nne – pia ‘Pembe za Ndovu’ zenye kuelekeza ncha Angani huku zikiifuatisha Vesika-Paisisi ambavyo hasa ni akitipu-taswira ya ‘mawimbi tashoni/gravitali/akili yenye kufungamanisha nyakati na usupasha wa ulimwengu wote mzima’.

Kumbe, 'Sovereini Jumuifu' ni dhana ya Uhuru ni Kazi/Huduma kukadirisha ‘fahari ya hazina iliyofichika ya Mbingu’ ambavyo ‘Ngao ya Ustawi’, ‘Pembe za Ndovu’ na ‘Muktadha wa Koherensia ya Udhamirifu wa hatua za kuukwea Mlima wa Utukufu wa kilele cha juu kabisa juu ya sura ya nchi, kushikilia pembe na kuegama mikono kwenye Ngao na Pembe’ vinafanyiza maskoti kwa kheri, baraka na tumaini kwa ‘Terani Krista’-- Nasibu ya Uzaliwa upya wa Stawi-Jamhuri wenye kudhihiri ‘Ufalme Kufanyika Duniani, kama Juu Mbinguni’.

Kumbe, 'Sovereini Jumuifu' ndiyo ontolojia na metafizikia ya ‘Uhuru na Umoja’ kukadirisha ‘vina vya tafsiri’ kwa kauli mbiu za ‘Hekima ni Uhuru’ na vile vile ‘Hekima, Umoja na Amani’ kuwa ni ‘Ngao Zetu’--Afrika na Watu wake; ambavyo Afrika Mashariki, na Tanzania khasa, ni kitovu cha ‘Mwanzo’ wa ‘Sivilai Terani’ ilivyo ni muktadha wa ‘Terani Krista’--Terani Krista iliyotengenezewa njia ya ‘kitawala na nchi’ kwa DHAMIRA YA WAZI KIKATIBA ya kulitangaza Taifa la Watu wenye Nchi ya Kijamaa, na tena yenye kuanza muktadha wa kulijenga taifa lao kwa ‘Sura na Tawala’ za nasibu ya kuziishi ‘Siasa za Ujamaa na Kujitegemea’.

Maarifa fulani yanasubiri mbele kidogo ambavyo fasaha ya vina vya tafsiri kwa ‘Shoka, Nyengo na Mkuki’--zana za dhahabu kwa kuuendea Ujamhuri Uliotaamulika, zinaweza kukadirisha ‘mageuzi kamili na ya kweli kijamii’ kulinasibu taifa la Tanzania, Afrika na Dunia nzima na ‘Usivilai Intastela’.

Wanajamii hawana budi kuweka nia thabiti katika KUJISAHIHI KITAASISI NA MIFUMO na basi penye NIA PANA NJIA.

+++++


View: https://www.youtube.com/watch?v=Wy3AvM1aMgc&list=LL&index=22&t=32s&pp=gAQBiAQB


Hakuna mtu wa Haki anaweza 'kufanya vizuri' kwenye hali/mazingira haya ya Umma usiyojitambua barabara... Akifosi kingi ataishiwa 'kuangushiwa zigo la lawama' ama 'kuangushiwa Jumba Bovu'...

Mara nyingine ni busara na hekima, kujiweka pembeni kuepusha msongamano -- kutokimbilia siasa/mambo ya siasa kwa 'uanahakarati'...

Ikibidi sana kuwa 'Mwanaharakati'; jitahidi sana kujimulikia njia zako kwa hekima ya ukweli wa mambo: Hauwezi kupambana na 'Moto' kwa kutumia 'Moto'...

Sisi wanajamii tunaowajibu wa kupeana mwangaza kuhusu ukweli wa mambo ili kupunguza/kuondoa/kutokomeza ujinga kuhusu 'Jamii na Uhuru wa Kweli'...

++++

View: https://www.youtube.com/watch?v=Ix4nKNDKhTQ
 
Back
Top Bottom