Endelea kupumzika kwa amani Ngwea

barcelonista

Senior Member
Apr 26, 2021
158
146
ENDELEA KUPUMZIKA KWA AMANI COWBAMA.

Na Xavi Hernandez Alcantara

Wao walipewa wakina Tupac Shakur,Notorious,Eminem lakini sisi tulipewa wewe wao waliongezewa wakina Jay Z,T.I na wengine wengi lakini sisi tulipewa wewe mmoja uliekuwa na ubongo wa Albert Einstein kwenye kichwa chako wewe ulikuwa maana halisi ya kipaji kwenye muziki.

Wakati Mfalme wa Pop Michael Jackson akiiacha Dunia na Album gumzo ile ya Thriller ya miaka ya 1982 wewe uliondoka na ukatuachia Album yako ya A.K.A MIMI Album ambayo hakukuwa na mtu ambaye angeweza kusogeza nyimbo mbele zaidi ya kuifanya ijirudie.

Kipaji chako kilikuwa kikubwa sana ulifahamu kila kitu kuhusu muziki ukaiteka Nchi kwa namna ambayo ulifanya mziki wako kwa namna ambavyo ulitengeneza nyimbo kali ziliozoeleweka,Uandishi wako haukuwa wakawaida.

Kwa sasa umelala na hauwezi kuamka ni miaka 8 sasa imepita lakini kile ulichokitengeneza bado hakiishi utamu Mungu alitugea zawadi kubwa lazima tumshukuru kwa hilo,Nilikusifu kabla ya kifo chako leo nasema tena

Uliposhika Maiki ya P.Funky ulijua namna ya kutengeneza hits kali tukashindwa kujua ipi tamu zaidi ni She Got Gwan,Ghetto Langu au Mikasi. Endelea kupumzika kwa amani bahati mbaya platform za muziki hazikuwa kama sasa.

Uligusa sehemu zote za burudani akatuambia kuhusu mapenzi kupitia CNN,Mapenzi Gani. Baadae ukatupeleka Kimya Kimya ukiwa na jamaa yako JayMo huku mtaani ukatuletea Nipeni Dili. Kiufupi ulikuwa mwana muziki uliyekuwa na kipaji kikubwa sana.

Namna ambavyo ulikuwa na uwezo wa kuichezea beat na kuinyanyasa ni pale tuliposikiliza CNN. Maisha ya mtanzania ni chini ya dollar moja wewe ukatugea hit kali ukisema MASIKINI WENZANGU.

Ukatufanya tushindwe kukuchoka,ukatufanya tushindwe kukuzoe kwa namna ambavyo ulikuwa hatari. Uliburudisha na Ulitoa Elimu mikono yako ilijua kuandika na Ubongo wako ulikuwa unafikiria mbali sana.

Hakuna mwanadamu tena kama wewe ambaye aliweza kuimba sana,ambaye aliweza kurap sana hakuna mwanadamu anaeweza kufanya Freestyle kama zako. Freestyle ni wewe na ulivyokufa uliondoka nazo. Tulipewa Godzilla lakini alikufuata mapema huko uliko.

Bongo Records ipo na P.Funky Majani yupo ile Maiki uliyokuwa unaitumia kuachia ngoma kali ndiyo hiyo anaitumia bwana mdogo Rapcha. Sijui niandike nini ili wajue namaanisha nini hawa watoto wa leo Doh"

Wakati wengi wakiendelea kufurahi na ngoma zako kali kama CNN,Ghetto Langu,She Got Gwan,Mikasi,Dakika 1,Nipe Dili,Speed 120. Kuna hii moja inaitwa MASIKINI WENZANGU inabaki kuwa nyimbo yangu bora kutoka kwako. Kama ulivyotuambia ukifa pengo lako halizibiki. REST IN PEACE GWEA. COWBAMA.

images (2).jpeg
 
Kwenye G weka H kwenye E weka T
na kwenye T weka O...ni GHETO,
Masela kwa maduu...

Dah rest in peace ka wiiizeeee

Nipo hapa nasikiliza mdundo wako wa weekeeend baaabyyy!!!
 
MASIKINI WEZANGU......

hii itabaki milele na milele
Aliandika
Alichora
Alifikiria mbali sana
Na akauvaa utanzania vyema ....

wachache wanaishi wengi wetu tunasindikiza

Weka mgomo baridi hlf uijue serikali
Then muulize ulimboka umuhimu wa madaktari
 
emoji444.png
Kwenye G weka H kwenye E weka T
na kwenye T weka O...ni GHETO,
Masela kwa maduu...
emoji445.png


Dah rest in peace ka wiiizeeee

Nipo hapa nasikiliza mdundo wako wa weekeeend baaabyyy!!!
hatari mzee🔥🔥🔥🔥
MASIKINI WEZANGU......

hii itabaki milele na milele
Aliandika
Alichora
Alifikiria mbali sana
Na akauvaa utanzania vyema ....

wachache wanaishi wengi wetu tunasindikiza

Weka mgomo baridi hlf uijue serikali
Then muulize ulimboka umuhimu wa madaktari
Wachache ndio wanaishi wengi wetu maescot,twiga wanapanda bila hata ya paspot..

Dah,🔥🔥🔥 sema imebaki kama underra
ated song
 
Umempamba sana ila wala hakuwa na maajabu hayo nyimbo zake ziliendana na umri wako ndio maana unemuona kama mtu hatari ila wa kawaida tu.
 
Mimi na watoto wangu mpaaka wajukuu huyu Mwamba atabaki kuwa nembo yangu.Dakika moja huu wimbo mpaka leo sijui ni ubongo wa Namna gani ulitumika kuandaa haya mashairi.Ngwea ni msanii bora sana
Dk moja ni bonge la wimbo. Ktk nyimbi zake zoote huu ndo my favour kwa kweli
 
Mademu wangu wote mimi ninawazimia,
nipeni namba zenu wote nitawapigia...

hii nyimbo itabaki nyimbo bora kutoka kwake, apumzike kwa amani.

pia kuna sikiliza, weekend
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom