Endapo video & audio zitatumika kwa Sugu, basi Mnyeti ajiadae

Hahaha ILANI inayotumika inavipengele, kipengele cha kesi ya sugu kina ruhusu audio.
 
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana. Taifa limegawanyika kabisa
 
Kiberiti ni kifaa kinachofanya haki kutendeka. Tunaheshimu sheria lakini sio wajinga. Kuporwa haki na kumuachia Mungu huo ni ujinga wakati kiberiti kipo.

Aisee, nimepigwa butwaa :eek::eek::eek: lakini baadae kidogo nikacheka :D:D:D aste - aste kwa comment yako hii!!

Wakati huohuo ninakuunga mkono mkuu kwani ni kweli haki haiji kwenye kisahani kama cake ya harusi bali wakati mwingine lazima kwanza :mad::mad::mad::mad: upige moto kwa njiti ya kiberiti msitu na manyasi sawasawa tu na mkulima wa miwa anapotaka kuvuna miwa yake ili kufukuza simba, mbweha na mifisi manyoka ili upite salama kwenda uendako ama mkulima avune miwa yake salama!!
 
Kuna kila dalili ya kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kuja kuwa kesi ya mfano kwa vizazi na vizazi vijavyo.
Sabasaba za msingi zipo nyingi ila nitaweka chache nitakazozikumbuka na nyingine mtanisaidia:-
  1. Kesi ya Sugu inaendeshwa kwa mtindo wa haraka ambapo itasikilizwa mfululizo, tofauti kabisa na kesi zingine za aina hiyo zilizopo mahakamani kwa sasa naweza kusema safari hii polisi wamejiandaa vizuri na ushahidi wanao mkononi hawahitaji kupoteza muda kazi nzuri .
  2. Kuna watu wa mlengo fulani wa kisiasa wanapiga mbiu kuwaandaa watu kisaikolojia kuwa makosa ya Sugu ni makubwa na anastahili kufungwa.
  3. Ni hivi majuzi tu TAKUKURU, Ilitupilia mbali ushahidi wa picha na sauti uliotolewa dhidi ya mtuhumiwa mmoja wa rushwa, kwa sababu wanazozifahamu wao, sipingi uamuzi huo kwa kuwa ni muhimu ushahidi kama huo kabla ya kukubalika mahakamani kwanza ni lazima upitie kwa wataalam wa Sauti, picha, na ishara kwa maana ya kwamba mtaalamu wa sauti afanye uchaguzi na kuthibitisha pasi na shaka kuwa sauti inayosikika ni ya mtuhumiwa na si vinginevyo, hali kadhalika wataalamu wa picha na ishara waithibitishie mahakama pasi na shaka kuwa picha na ishara zinazoonekana zinaendana na sauti inayosikika na kwamba hakuna uhariri wowote uliofanyika.
  4. Sugu hakutahadharishwa na polisi kuwa wanamrekodi na kuwa maneno atakayoyaongea yatatumika kama ushahidi mahakamani dhidi yake, hivyo basi kuweza kumpa nafasi mlalamikiwa kuthibitisha maneno yaliyorekodiwa kuwa ndio maneno halisi aliyo yatamka baada tu ya recording kukamilika. Kwa sababu hiyo ni vigumu sana kwa polisi kuutoa ushahidi huu bila kupitia kwa wataalamu nilio wataja ili waweze kuthibitisha pasi na shaka. Kwa uamuzi uliotolewa jana kukubaliwa kwa ushahidi huu bila kupitia kwa wataalamu husika ndio ninachosema mahakama itaweka historia kwani hapatakuwa tena na umuhimu wa wataalamu kuthibitisha ushahidi kitaalamu mfano Madaktari, alama za vidole, maabara nk.
  5. Matumizi ya ushahidi huo wa polisi mahakamani yataamua pia ushahidi wa wabunge wa Arumeru na Arusha dhidi ya Mnyeti kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili. Kwani mazingira ya ushahidi ulivyo patikana katika kesi hizi yanafanana.
  6. Mashaka ya Mbowe, na kujitoa kwa mawakili wa mtuhumiwa wakilalamikia mwenendo wa kesi usioridhisha, hakimu kumnyima dhamana mlalamikiwa richa ya kuwa anastahili pili hakimu kukataa kujitoa katika shauri hilo richa ya kuombwa kufanya hivyo tatu kuukubali ushahidi ulio rekodiwa bila kwanza kupitia taratibu zinazokubalika hii imeifanya mahakama kujiweka kwenye mizani dhidi ya raia.
Kwa vyovyote vile kesi hii imeiweka mahakama kwenye mizani, itahukumu lakini pia ijue itahukumiwa. Isije kuwa maneno ya jaji mkuu pia yalilenga kutuandaa kisaikolojia.
Mkuu mahakama ni tawi la ccm kwa maana jaji mkuu na majaji wanachaguliwa na mwenyekiti wa ccm
 
siasa bila kutumia matusi jukwani inawezekana, siasa za matusi hazina tija katika taifa letu,
 
Wajiandae kupokea Video zinazoonyesha Viriba vya Miili ilikuwa inaokotwa Baharini,

Tuone watakataa? Kama waliweza kupokea wa Sauti wasubiri wa Video na Sauti, maana Hiyo Miili ilikuwa inaokotwa na Polisi na kutuambaia wanaendelea na Uchinguzi kujua Miili inatokea Wapi, na Wazuri akisema Miili mingine ni yawakimbizi.
Wakshapokea watamfunga nani!bahari au sulfeti
 
Back
Top Bottom