Endapo CHADEMA itakufa, haya ndio yatalikumba Taifa...

Endapo CHADEMA itakufa, haya ndio yatalikumba Taifa...

UVCCM mbona mnachagua wanaume wanamke?
 
CDM ikifa bado vinaweza kubaki vyama vingine vya upinzani lakini uwezekano mkubwa ni kwamba vitakuwa ni vyama pandikizi na kama vitakuwa vya upinzani wa kweli havitakuwa na nguvu, Kumbuka cdm ilikuwepo kabla ya 1995 hivyo kukijenga chama kingine kifikie hapo kilipofikia cdm si kazi ndogo.

Nakumbuka NCCR Mageuzi - ilikuwa na nguvu sana lakini ikafanyiwa kitu - iko wapi sasa; ilikuwepo CUF yenye nguvu 1995 na ikasemekana kushinda Zanzibar! Unayaona yanayoendelea.

Kwa wale tulioishi ndani ya mfumo wa chama kimoja tupo ambao hatupendi kurudi ndani ya mfumo huo tena. Nadhani hata ndani ya CCM yawezekana kuna watu hawapendi urudi mfumo wa chama kimoja.

Wakati Nyerere anajenga hoja ya vyama vingi alisema chama kimoja kina tabia ya kujisahau. Kikijisahau kwa sasa ambako hakuna tena miiko ya uongozi - hakika itakuwa balaa.

Hawa wanaoutosa upinzani kwa hoja ya kumuunga mkono rais nadhani hawako sahihi sana, mbona mimi namuunga mkono huku niliko?
 
Kiukweli nilichojifunza kwa upande wa siasa kama unaifatilia ni unapoteza muda kwa kweli,, kwa mana siwezi kuamini wewe umeamuwa kuwa mpinzani na umeamuwa kupambana kuona kuwa yale unayoyapinga ni sahii wewe kuwa mpinzani alafu inatokea gafla unapewa pesa unahamia kwa wale uliokuwa unawapinga kitokana na kiasi cha pesa, au kwa kuona njaa imekuwa kali na kuanza kutia huruma
 
Back
Top Bottom