Ems ni njia y uhakika, ya haraka na salama,
Kwa malipo ya shilingi elf 15 utapewa risiti ya uthibitisho wa malipo na tracking number itayokuwezesha kujua barua yako imefika wapi, barua za kawaida huzina tracking number
Ni njia ya haraka sana, kwa Mimi ambae nipo mbeya gari la ems linaondokaga na barua za ems saa tano asubuhi na linafikisha barua dar es salaam siku hiyo hiyo, kwa barua za kawaida zinaweza kuchukua mwezi au zaidi
Barua inapofika tu itapelekwa kwenye ofisi husika uliyoiandikia barua kwa njia ya pikipiki za ems, ni tofauti ni barua za kawaida inabidi ofisi uliyoandikia barua ikafuate barua posta
Ni hayo tu, kupata kazi inabidi ujitume kwenye utafutaji na uombaji, Ems ni Huduma effective