Empower ni matapeli?

PSPA Pure'12 udsm

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
829
443
Nilituma CV yangu kwa Empower. Kwa wasiowajua Empower, ni recruitment Agency hapa Dar es salaam.Ofisi zao zipo msasani tower opposite na CCBRT.

Kwanza kabisa ni lazima nikiri kwamba wimbi la ukosefu wa ajira ni kubwa sana na linazidi kuongezeka kila siku. Kwa kanuni za kijasiliamali, linapotokea tatizo hapo ndipo zilipo fursa za kibishara. Nadhani hawa Empower nao wanafata kanuni hii. Baada ya kuona tatizo la ajira zinazidi kukua na kuongezeka Tanzania, limeibuka wimbi kubwa la watu na Wakala kibao la Ajira. Leo hii hata wafanyakazi wa majumbani wanapatikana kupitia madalali. Nikisema madali namaanisha watu binafsi na wakala, kampuni au blogs mbalimbali zilizojiweka katikati ya mfanyakazi na mwajiri.

Empower baada ya kuona fursa hii, wakaanzisha mfumo wa kila anaetuma CV katika Tovuti yao wanamuita kwenye usaili. wanaita Screening Interview. Na wanatoza 10,000 kwa kila anafika kwenye huo usaili.

Kama nilivoeleza pale juu, wimbi ni kubwa sana la ukosefu wa ajira. Kwahiyo Empower wana uhakika wa kupata wasailiwa wasiopungua 50. Hii ina maana kwamba wanaingiza si chini ya laki tano kwa siku (500,000). Kwa faida ya wasiojua hesabu yaani watu 50*10,000 kwa kila mtu. 50*10,000=500,000. Hili linaweza kuwa kadirio la chini kabisa.Tozo ya 10,000 wanaita ada ya usajiri katika kanzu data yao (Database Registration fee).

Ilibidi niulize kuhusu usaili wao, ambao kimsingi hauna tija yoyote na wala hauhusiani na kazi. Kwani unapotuma CV na wanapokuita kunakua hakuna nafasi na wanakupigia simu mara nafasi inapotokea kutoka kwa mteja wao ambaye ni makampuni yanayokua na nafasi z kazi kwa muda huo. kwa mujibu wa masaili wangu anasema usaili wao ni kwajili ya kujua mawili matatu kuhusu wewe na ni aina gani ya kazi unayotaka. Lakini kimsingi unapotuma CV unakua umeshaainisha wasifu wako, uzoefu na ujuzi wako wa kazi unayoomba.

Yatasemwa memgi hapa kuhusu huu utaratibu wa kutoza 10,000 kama utetezi, lakini ukweli unabaki pale ple, huu ni wizi na utapeli. Hakuna Guarantee ya kupata kazi. Na ukiangalia hali ya kifedha ya watafuta ajira wengi, sio uungwana kuwabebesha mzigo huu tena.

Pili, kila siku wanapokea mvua za CV pale. Lakini inaweza kuisha hata wiki 3 hawajatangaza ajira mpya kwenye tovuti yao. Hii ina maana wanaendelea kupokea pesa za watu bure ilihali wanajua kabisa hawana uwezo wa kuwakutanisha na waajiri wa idadi ile ile. Hapa Empower wanataka kula 10,000 za watoto wa masikini wasiokua na nyuma wala mbele kwa ahadi hewa ya ajira.

Tatu, kwanini isifike kipindi wakasitisha kupokea CV kwanza ili wafanyie kazi zile ambazo zimeshawafikia kwanza ili kuwatendea haki waliolipia awali? Kwa hali ya kawaida kabisa sidhani kwamba Empower wana wateja kwa maana ya waajiri zaidi ya 50. Na hata kama watakua nao, haiwezekani wakawa wanatangaza nafasi za kazi kila siku. Kama hii ndo hali halisi, kwanini wao wanapokea fedha za watu kila leo?

Hapo staki kuongelea ile tabia ya asili ya kupendeleana. Kwa wale wasomi wa Organization Theory au saikolojia watanielewa (Bias is inherent). Popote pale, upendeleo upo ila upo upendeleo wa ki-professional. Yaani mwenye sifa ya ziada ndio anapewa nafasi. Sasa katika mazingira yetu haya ya kitanzania hebu tuambiane ukweli. Mtumishi wa Empower pale zitokee nafasi sehem nzuri alafu achomoe CV ya Kitilami kilondomoni kutoka lyamko huko dabaga wakati huo mdogo wake anazurula na bahasha ya kaki posta kule hana kazi. Hii kama haijawahi kutokea hapo Empower mtaniwia radhi. Ila kwa uelewa wangu haya mambo ni ya kawaida sana.

Mwisho kabisa, naomba tusaidiane kujibu maswali la UHALALI wao kisheria. Nakumbuka mwaka jana aliyekua Waziri wa ajira Mh.Gaudensia Kabaka alizisimamisha kufanya kazi wakala zote za ajira. Sasa je, ziliruhusiwa tena lini? Na kama zimeruhusiwa, ni halali kutoza ada kama hizi? Na je lile tatizo la kujilipa nusu ya mshahara wa mfanyakazi limeisha?
Baada ya hapo tutakuwa na nafasi nzuri kujibu lile swali msingi la ama Empower ni matapeli au si matapeli.

PSPA Pure'2012 udsm.
 
Me pia napenda kufahamishwa kuwa zile ajira za NMB zilizotoka hivi karibuni ni za kweli.. Maana sasa naanza kuogopa.
 
Ah kumbe ujumbe umefika mahara pake. Sasa hawa dawa yao ni zamoto tu. Kwani hivi wanalipia kodi hiyo tozo:(:(:(:(
 
Hali ni mbaya kiuchumi katika nchi hii ya wadanganyika maana kila mtu anatumia profesheni yake kutapeli Masikini.
 
imekuwa taabu kabisa


mimi sasa najiingiza kwenye kilimo kidogo kidogo bora niwe na kabustani kangu ka mboga najua kila siku ntangiza pesa ajira hakuna.............
 
Nataka kuapply sasa hizi.
Naomba mnisaidie wanaposema CV yangu iwe scanned and signed, sijajua wanataka signature ya nani? Ukweli nmeona kazi za NMB za northern, nmekuwa interested kuapply. Naomba msaada wenu ili nitimize masharti yao.
 
Naomba mnisaidie wanaposema CV yangu iwe scanned and signed, sijajua wanataka signature ya nani? Ukweli nmeona kazi za NMB za northern, nmekuwa interested kuapply. Naomba msaada wenu ili nitimize masharti yao.
print your CV Then Sign on it , after Sign then Scan it .
 
Hio 10k ni uamuzi wako kuilipa au kutolipa, acha malalamishi yasiokuwa na msingi, maana hujashikwa mkono kutoa hio pesa, hivi ni lini watanzania hasa wasomi wa BA na m'a PhD mtaamka, hapo unakuta hao jamaa ni form 6 drop out. Kwani huoni kabisa job hakuna bado unajipeleka kwa kichinjio, Tanzania ya viwanda #
 
Hio 10k ni uamuzi wako kuilipa au kutolipa, acha malalamishi yasiokuwa na msingi, maana hujashikwa mkono kutoa hio pesa, hivi ni lini watanzania hasa wasomi wa BA na m'a PhD mtaamka, hapo unakuta hao jamaa ni form 6 drop out. Kwani huoni kabisa job hakuna bado unajipeleka kwa kichinjio, Tanzania ya viwanda #
Wee toka uzaliwe hujawai kuibiwa?
 
Back
Top Bottom