Nimekuona mitaa fulani halafu ukasepa baada ya kuona nondo zilivyopigiliwa. Habari za masiku malenga wangu.
Mie sioni tatizo pia mtu kufowadi e mail zake ila tatizo linakuja kwenye contents za hiyo e mail. Kama ikiwa kuna maneno yasiyofaa au picha chafu za kutengeneza mie sikuungi mkono. Fahamu kumfanyia mtu jambo ovu unatakiwa ufikirie je akifanyiwa mtu wako baba yako, mjomba wako, dada yako, mama yako au wewe utajisikiaje?
Ukiona hutafurahia basi na huyo muhusika mnaemjadili hapa kwa majina mengi mengi mengi yakiwa ya kuchukiza hatapenda pia. Sidhani kuna mtu anapendwa aitwe kwa majina ya ajabu ajabu yenye kila hila za kejeli na dharau. Sisi waislam tumeusiwa tuitane majina mazuri ndio maana ni nadra sana kukuta majina ya ajabu ajabu kwa waislam ila wachache wakibantu haswahaswa.