Elimu Yetu Ya Tanzania

Elimu Yetu Ya Tanzania

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
1,278
Reaction score
1,556
Wakuu Ila Mfumo wa nchii hii wa kutumia kiingereza kama Lugha ya kufundishia Mashuleni Kwa Maana ya Shule Ya Msingi Na Secondary umepitwa na wakati.
......
Ni sawa na kama uko Arusha unataka kwenda Moshi mjini so unaelekea Babati then Kondoa halafu Singida then unapanda hadi Mwanza unashuka Tabora.
......
Halafu Unaingia Simiyu unatokea West Kilimanjaro unashuka hadi Rombo Mashati unaenda Tanga unachukua boti hadi Zanzibar afu unaingia Dar then Chalinze.
.....
Then Unashuka Wami unaingia Segera, Korogwe, Mombo, Same, Mwanga, Njia Panda, Unakula njia ya Uchira, Kiboroloni, Majengo, Unaingia njia ya Round about ya Kcmc afu ndo uingie mjini.
.....
Wakati ni suala la kuwasha gari unaingia tengeru then Usa, Katiti, King'ori, Kia, Boma, Sadala, Machine Tools, Unakula Njia Ya Mnadani, Mferejini, Maili 6, Memorial, Chagbay then umefika mjini.
.......
Mfumo tulio nao unafanya elimu iwe ngumu mara dufu. Kwanza mtu atumie nguvu nyingi kuelewa lugha afu ndo aje aelewe alichofundishwa.
.......
Ndo maana ubunifu wenye Jukumu la Kusimamia Elimu ya Nchi Hii sjui Tuseme ni mdogo sana, Muda wa kubadilika na kutumia Kiswahili ni SASA!
.......
Samahani Wakuu Hizo Njia Nilizozitaja Zito Ziko Kaskani Mwa Tz.
 
Serikali imeua mfumo wa elimu tangu uhuru.unakuta PHD au profesa hajui kiingereza hii ni hatari.unakuta profesa anatamka neno la kiingereza kama anaongea kiswahii .serikali iache ushamba itumie lugha ya kiingereza kutoka nursery hadi chuo kikuu.watoto wote wa viongozi wanasoma shule za international school.mbona hawawapeleki watoto wao shule za kayumba?
 
Kwa vile Lugha yetu ya taifa ni Kiswahili, hakuna haja sana ya kusoma masomo kwa Lugha ya Kiswahili kwa maana tayar kumbe Kiswahili tunakifaham.

Inabid tu masomo yafundishwe kwa Lugha za kigeni kama ambavyo tunatumia lugha ya Kiingereza. Baadaye tutaongeza na Kichina kabsa.
 
Mahakama ndo sizielewi hukumu ya Msolapagasi Mwakisapile inapitishwa kwa kiswahili ila inaandikwa kwa kingereza
 
Back
Top Bottom