Elimu yetu Tanzania: Mbona International Schools hazina 'Holiday Package' kama shule nyingine?

Mfumo wetu ni kwamba wanaopasua A hawaendi ualimu wanaofeli ndiyo wanakuwa walimj, Magufuli aliwaita vilaza pale UDOM.

kaka haya mambo kukariri ni vibaya sana, na inasikitisha mno, wangapi na hizo A wapo kwenye kada za ualimu, mabadiliko ya sera ya mwaka 1974 ya Azimio la Musoma lilitaka kuondoa uhaba ya Walimu kwa kuwa wakati huo mpaka 2008 nchi ilikumbwa na hio changamoto (mpaka sasa) ndio mana SI WALIOFELI ila WOTE waliweza kusomea ualimu na ndio mana vigezo vya kwenda kusomea havikuwa vigumu sana,

Ualimu kuonekana kuwa kada ya failures ni kwa sababu ya mkakati huo, na sijui kwanini watu hawataki kuelewa, vingine hutokana na chuki ya mtu tuu, na si kwamba haelewi kinachoendelea,

Mambo yanabadilika kaka, hii ni taaluma, sijui kama unafahamu vigezo vya kusomea ualimu na udaktari kwa sasa.

Btw; mimi ni Mwalimu.
 
Mkuu maisha hayana holiday...kila aliefanikiwa hamalizi kazi zake zote ofisini.japo unaona kama hawana...ukichunguza wana (projects and assignments)....
Usizoeshe wanao kuwa kuna muda ambao mambo yote muhimu yanawekwa pose ili ale bata kwanza.....
Nina uhakika kuwa mtoto wako hasomi international school.

Shule unazolinganisha hazifanani,kwenye ufundishaji,mtaala,hadhi,sinyllabus na hata malengo ya elimu na kadhalika.kwa mfano kuna CBC ya English medium, CBC ya kiswahili,British Carriculum na Cambridge.....

Sasa wewe na Mimi watoto wetu wanasoma CBC ya kayumba alafu unataka waende na curriculum ambayo hata haitambui mitihani kama assessment ya uwezo wa mtoto.
Usikariri.

Mwalimu mkuu hapa.
Asante mwalimu mkuu mi nimekuelewa sana.
 
Hatimaye tumeeleweka. Waziri Ummy Mwalimu katangaza hakuna ruhusa mtoto kusoma wakati wa likizo.

Likizo ni muda wa mapumziko.

Hivyo walimu acheni uvivu tumieni vizuri dakika 40 au 80 za vipindi vyenu.

Holiday packages si jambo baya, lasivyo lisingekuwepo kabisa; na hilo neno tusinge kuwa nalo. Mwaka wa masomo hugawanyaa katika likizo nne, mbili fupi yaani ya March na September na Mbili ndefu yaani Juni na Disemba.

Tuna kundi la mitihani ya Mid-Term

Kuna Terminal

Na Annual.

Mtihani wa Terminal hufanyika mwezi Juni, terminal exam maana yake ni upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi kabla ya kumaliza mtaala wa somo (term assessment). Hapa ndipo Mwalimu hupaswa kutoa Holiday Package ili kupima umbali mwanafunzi amefikia nusu muhula wa kwanza.

Pia tuna mitihani ya Mid term ya mwezi September, mitihani ile ni ya kufanyia tathmini ya uelewa wa mwanafunzi nusu muhula ya pili, kisha mwezi oktoba na novemba ni kwa ajili ya kurudia maudhui ya mihula yote miwili.

Mtihani wa Annual ni mtihani wa upimaji wa mwisho wa mwaka, likizo ya mtihani huu ndipo mwalimu hapaswi kutoa Holiday Package kwa sababu hafanyi tathmini ya nusu muhula. Mtihani ule sio Assessment ni Examination (cross check) ile ni taarifa ya nini mwanafunzi ameambulia mwaka mzima, na ni taarifa kwa mzazi na Mwalimu juu ya uwezo wa mwanafunzi anayejiandaa kuingia ngazi inayofuata.
 
Hatimaye tumeeleweka. Waziri Ummy Mwalimu katangaza hakuna ruhusa mtoto kusoma wakati wa likizo.

Likizo ni muda wa mapumziko.

Hivyo walimu acheni uvivu tumieni vizuri dakika 40 au 80 za vipindi vyenu.

bro unaelewa holiday packages?? Ama ulielewa hoja yangu? Ama ume quote kuamsha thread?
 
Niliielewa. Ni hoja iliyoenda kinyume na mahitaji na haki za binadamu anayeitwa mtoto.

Nilianzisha thread makusudi nikijua likizo imekaribia na wasumbufu wa holiday package wataanza na kiukweli wameshaanza..

Lengo langu lilikuwa mamlaka ziingilie kwani muda wa mwalimu ni shuleni na dakika zake 40 au 80.

Muda wa nyumbani si wa mwalimu wala shule.

Wewe ulijikita kuonyesha hadi ratiba ya mitihani ikiwemo ya term na mid term na end of the year.

Kimsingi milikuvumili tu kwani mitihani yote hiyo ni wajibu wako wewe mwalimu katika muda wa shule.

Muda usio wa shule ni mtoto kulelewa na wengine ikiwemo mtaani na wengine.

Hivyo tumine muda wenu shuleni, tungeni hata mitihani 1000 lakini hukohuko shuleni.

Sisi muda usio wa shule ni wetu wazazi.

Kwa taarifa yako mimi mwanangu hata hizi mnazoita homework huwa sitaki kumuona nazo hspa nyumbani.

Kazi za shule amalizie huko shuleni akija nyumbani kama ni kusoma asome mambi tofauti na ya shuleni mfano, aende Library akaazime vitabu au aingie kwenye internet akajadili na wanafunzi wa nchi nyingine duniani.

Nilisoma hivyo ninawarithisha wanangu hivyo nilifaulu na wanafaulu vizuri.

Sawa.
 
Back
Top Bottom