Elimu yetu iwe ya mfumo wa 6+3+2+3, miaka 20 mtu kashahitimu chuo

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Amani iwe kwenu!

Kwa mfumo wetu wa sasa wa elimu mwanafunzi anaanza darasa la kwanza akiwa na miaka 7, anasoma elimu ya msingi kwa miaka 7, akifaulu anaenda sekondari kwa miaka 4, akifaulu anasoma sekondari ya juu miaka 2 na akifaulu anaenda chuo miaka 3 (au zaidi kwa baadhi ya fani). Kwa mtindo huu mtu anamaliza chuo akiwa na miaka isiyopungua 23 yaani 7+7+4+2+3. Umri huu ni mkubwa sana na ingefaa mtu huyu awe tayari anajitegemea kama mfumo wa elimu mbadala ungetumika.

Mimi napendekeza mfumo wa elimu ungekuwa hivi, mwanafunzi aanze shule akiwa na miaka 6 (hii inawezekana maana imeshazoeleka hasa mijini) sasa iwe ni sera ya nchi bila kujali jinsi ya mtoto. Halafu elimu ya msingi iwe miaka 6 tu hapa itabidi darasa la sita lasasa livunjwe masomo yanayofundishwa darasa la tano, sita na saba yaanzie darasa la nne, tano na kufika mwaka wa sita yawe yamefundishwa yote.

Wanafunzi wanafaulu elimu ya msingi kwa walau wastani Wa C waende sekondari ambako watasoma kwa miaka 3 (kama QT wanasoma elimu ya sekondary katika mazingira ya nyumbani kwa miaka 2 na wanafaulu basi wanafunzi wa shule wanaweza kufaulu vizuri tu wakisoma sekondary kwa miaka 3 tena bila shida).

Wanafunzi wanaofeli darasa la saba yaani waliopata chini ya daraja la C wapewe nafasi ya kukariri shule (ukweli wa mambo ni kwamba viongozi wetu wengi na watunga sera wetu wa sasa wengi wao walirudia shule hadi mara 4 ndiyo wakafaulu, sasa kwanini waone ni nongwa kwa mwanafunzi wa sasa kurudia shule?). Kurudia shule kwa mwanafunzi anayetaka ikubalike kisera kabisa tena bila usumbufu kwa jina lake lile lile, ila wale ambao hawataki kurudia wapelekwe VETA.

Sera ya elimu ya VETA iwe huria kwa mwanafunzi au mtu yeyote anayetaka kujifunza elimu ya ufundi bila kujali umri ilimradi huyo mtu kahitimu elimu ya msingi na anataka kujiunga kwa hiari yake. KWA WANAOFELI DARASA LA SABA IWE NI LAZIMA KWENDA VETA KAMA HATATAKA KURUDIA SHULE. Hii itazuia kuolewa kwa umri mdogo na kupunguza raia wasio na ujuzi na kazi kwa siku za baadaye

Wanaofaulu elimu ya form four kwa daraja la kwanza na la pili wapelekwe form five na six kwa miaka 2, watakaopta daraja la tatu wapelekwe vyuo vya kati (cerificates baadaye diploma) pamoja na VETA kwa anayechagua lakini kwa wenye division 4 na zero wapewe nafasi ya kwenda VETA au kurudia kama private candidates kama ilivyo kwa sasa. Kwa vile elimu ya ufundi ni ya vitendo basi hata mwenye div zero anaweza kuisoma vizuri tu hivyo akiomba kusoma VETA apewe nafasi bila kujali kama ana ufaulu wowote wa elimu ya sekondari.

Kwenda chuo kikuu iwe ni kwa wanafunzi wanaopata daraja la kwanza na la pili tu baada ya kufaulu form six lakini wale wanaopata division THREE wapelekwe kusoma diploma ya anachokihitaji na kwenye ile ada yao serikali iwape mkopo kwa asilimia zisizopungua 70% ya ada maana wengi wao watakuwa ni watoto wa wale wanaoitwa wanyonge simaanishi kuwa watoto wa wanyonge ndiyo wanapata div 3 ila wanaweza kuwa wengi kuliko watoto wa wenye ahueni.

Mwanafunzi anayepata chini ya div 3 anaweza kwenda kusoma VETA kwa level yake au kurudia shule kwa mfumo wa elimu huria. Mwnafunzi wa chuo kikuu apewe mkopo si chini ya 70% pia.

FAIDA YA MFUMO HUU.

1. Kwa mfumo huu pendekezwa mwanafunzi atamaliza chuo kikuu akiwa na miaka 20 kwa watakaosoma chuo kikuu miaka 3.

2. Nchi itazalisha watendaji wengi sana (technicians) yaani watu wa level ya certificates na diploma kuliko ilivyosasa kila mtu ni graduate

3. Elimu ya ufundi itapewa wigo mpana kuliko ilivyo sasa hii itapunguza tatizo la ajira kwani watakaotoka VETA watakuwa na uwezo wa kutengeneza ajira wenyewe kuliko ilivyosasa ambapo graduates wengi hawawezi kujiajiri wenyewe hata baada ya kukaa miaka karibia 16 darasani

4. Uwekezaji kwenye vyuo vikuu utakuwa kidogo umepunguzwa maana watakaodahiliwa huko ni wachache hivyo serikali na wadau kufanya uwekezaji zaidi kwenye VYUO VYA UFUNDI PAMOJA NA VYUO VYA KATI.

5. Ndoa za utotoni zitapungua kwani wanaofeli darasa la saba watatakiwa kuendelea na VETA au kurudia shule (hii ikiratibiwa vizuri hawa bado watakuwa chini ya uangalizi wa serikali -hapa uratibu wa karibu utatakiwa kuanzia local government hadi juu kabisa)

6. Hakutakuwa na mtanzania ambaye hatakuwa na elimu au ujuzi lakini pia muda wa kukaa shule utapungua kutoka walau miaka 23 yasasa hadi 20

NB: Ni vizuri serikali iweke utaratibu wa ofisi ya mwenyekiti na mtendaji wa kijiji au mtaa kuwa na majina ya wanafunzi wote wanaotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba na baada ya matokeo wajue ni wangapi wamechaguliwa kwenda sekondari na kuhakikisha kwamba wale ambao hawajachaguliwa mzazi anaitwa kuamua kama mwanaye ataenda VETA au atarudia shule.

Serikali ya kijiji ihakikishe moja kati ya hayo yanafanyika kinyume chake wazazi au walezi wawajibishwe kikamilifu.

Unakaribishwa kutoa maoni yako, unaweza kuboresha ila si vizuri kukosoa bila kutoa walau maoni bora zaidi yenye kujenga.
 
Mbona wengine tumehitimu tukiwa na chini ya miaka 20.

Inategemea na kichwa cha mtu mzee. Wengine tukiwa na miaka 5 tupo darasa la kwanza.
 
Mbona wengine tumehitimu tukiwa na chini ya miaka 20.

Inategemea na kichwa cha mtu mzee. Wengine tukiwa na miaka 5 tupo darasa la kwanza.

Ndiyo maana mimi nimezungumzia issue ya sera siyo uepesi wa kichwa cha mtu. Mimi sijasoma darasa la tatu na darasa la sita nikamaliza chuo nikiwa na umri mdogo tu ila hiyo siyo sera ya elimu ya taifa hutokea tu kwa baadhi ya watu. Sasa ni vizuri kuwe na sera na sheria itayotumika kwa nchi nzima bwashee
 
Naunga mkono hoja, 23 - 26 naona inamnyima mtu nafasi ya kujaribu vitu vingi au kipindi cha kuwekeza katika ndoto yake. Mwisho wa siku tunajifunga kwenye ajira kama njia secured kwa wakati ujao
 
Halafu akishahitimu chuo na hiyo miaka 20 unampeleka wapi..?

Kwani kwasasa hivi wanaohitimu kwa miaka zaidi ya 20 wanapelekwa wapi? . Hawa hawatakuwa wengi sana kama ilivyosasa hivyo wanaweza kuajiriwa na kujiajiri pia.KWANZA LAZIMA UJUE LENGO LA ELIMU SI KUPATA AJIRA SERIKALINI NI KUTOA UJINGA, KUPATA UELEWA WA KUFANYA VITU VIZURI ZAIDI YA ASIYE NA ELIMU HUSIKA.
 
Mbona wengine tumehitimu tukiwa na chini ya miaka 20.

Inategemea na kichwa cha mtu mzee. Wengine tukiwa na miaka 5 tupo darasa la kwanza.
Ni kweli.mimi mwenyewe nilianza la kwanza Nina miaka mitano .Hilo sio swala la mtu kusema ohhh napendekeza mtoto aanze na miaka sota.Hilo Ni la Mzazi mwenyewe sio serikali
 
Ndiyo maana mimi nimezungumzia issue ya sera siyo uepesi wa kichwa cha mtu. Mimi sijasoma darasa la tatu na darasa la sita nikamaliza chuo nikiwa na umri mdogo tu ila hiyo siyo sera ya elimu ya taifa hutokea tu kwa baadhi ya watu. Sasa ni vizuri kuwe na sera na sheria itayotumika kwa nchi nzima bwashee

Watu wamekewa mfumo huu huu bado wanamaliza chuo wakiwa na miaka 27 wengine 30. Mtu anarudia hata mara tano darasa moja kwa ukilaza wake bado unataka wapunguze hiyo range.

Shida ni kichwa cha mtu.

Hata uwawekee mfumo wa kumaliza wakiwa na miaka 18 kuna watu watamaliza wakiwa na miaka 30 tuu.
 
Ni kweli.mimi mwenyewe nilianza la kwanza Nina miaka mitano .Hilo sio swala la mtu kusema ohhh napendekeza mtoto aanze na miaka sota.Hilo Ni la Mzazi mwenyewe sio serikali

Hatuwezi tukaacha maswala muhimu kama elimu kila mzazi ajiamulie anavyotaka tena kiholela. Sasa wewe ulianza ukiwa na miaka 5 halafu ndani ya darasa hilo mwingine kaanza akiwa na miaka 8 unaona ni sawa? huyu wa miaka nane anaweza hata kuwatia dole na kuwalawiti wengine maana ana upeo,utundu na nguvu kuliko wengine. Ndiyo maana ikiwa ni suala la sera inafunga watu wote nchi nzima kuwa darasa la kwanza ni miaka 6.
 
Nasema Ni swala la Mzazi sababu sio pia kila mtoto anasoma miaka Saba shule ya msingi mwingine Mzazi anamrusha madarasa.mfano mtoto anasoma darasa la kwanza na la pili akimaliza la pili anarushea darasa la nne anasoma anafanya mtihani wa darasa la nne akifaulu anarushwa Hadi darasa la sita anasoma la sita na la Saba anafanya mtihani huyo kidato Cha kwanza.

Hayo ya Sijui miaka Saba Ni shule za Serikali sio binafsi huko.labda ndiko uongelee
 
Watu wamekewa mfumo huu huu bado wanamaliza chuo wakiwa na miaka 27 wengine 30. Mtu anarudia hata mara tano darasa moja kwa ukilaza wake bado unataka wapunguze hiyo range.

Shida ni kichwa cha mtu.

Hata uwawekee mfumo wa kumaliza wakiwa na miaka 18 kuna watu watamaliza wakiwa na miaka 30 tuu.

kwani mkuu mimi nimesema mfumo huu mpya utalazimisha wanafunzi wote Tanzania kumaliza na umri wa miaka 20?, kama ningemaanisha hivyo hiyo abari ya kurudia darasa la saba, kurudia sekondary kama mwanafunzi huria ningeiweka yanini wakati ukirudia umri wako hausimami? mimi namaanisha miaka 20 kwa mwanafunzi ambaye hatapata kikwazo ya kumfanya arudie yaani anaanza na miaka 6 darasa la kwanza hadi chuo kikuu anamaliza akiwa na miaka 20 (kwa fani za miaka 3 chuo). Unajitoa kwenye kundi la vilaza wakati reasoning and understanding yako yanatia mashaka
 
Wazazi wako hawakuwa na uwezo wa Housegirl ila Sera yetu Inataka miaka 7 na mwaka huu wengi wamerudishwa nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu Wengine ndio.maana hawataki kupeleka watoto shule za Serikali sababu wanaona mtoto.kuanza la kwanza miaka Saba anakuwa tayari kikongwe .

Serikali inapenda kusomesha vikongwe.Miaka Saba mtoto kuanza la kwanza Ni Bibi na na babu huyo.

Miaka mitano sawa .Saba nintoo much
 
Nasema Ni swala la Mzazi sababu sio pia kila mtoto anasoma miaka Saba shule ya msingi mwingine Mzazi anamrusha madarasa.mfano mtoto anasoma darasa la kwanza na la pili akimaliza la pili anarushea darasa la nne anasoma anafanya mtihani wa darasa la nne akifaulu anarushwa Hadi darasa la sita anasoma la sita na la Saba anafanya mtihani huyo kidato Cha kwanza.

Hayo ya Sijui miaka Saba Ni shule za Serikali sio binafsi huko.labda ndiko uongelee

Mkuu hebu uwe unasoma comments kwa lengo la kuelewa siyo kujibu wakati hujaelewa kitu lakini kama umenielewa hata kwenye majibu niliyokupa kwenye comment yako ya awali basi uelewa wako unanipa mashaka. Narudia mtoto kuanza shule akiwa na miaka 5 au kumrukisha mtoto darasa SIYO SERA YA ELIMU YA NCHI HII ni mambo tu yanatokea sasa hatuwezi tukaacha sekta nyeti kama elimu kila mzazi au shule ijiamulie yenyewe. Kuna mzazi anaweza kumuona mwanye wa miaka 7 bado ni mdogo mwingine anaweza kuona kwa miaka 4 mwanaye anaweza akaanza shule halafu huko shuleni darasa la kwanza kukawa na wanafunzi wana miaka 10 wengine 9 wengine 7 halafu wengine 5 au 4. Hapo unyanyasaji na ushoga unaweza ukashamiri maana mtoto wa miaka 8 au 9 anaweza kuwafanyia wenzake mambo ya hovyo. USIPOELEWA TENA BASI HAPANA. Unajua kwanini ushoga Tanzania unakuja juu hasa kipindi hiki cha shule nyingi za private? hebu fanya tafiti hili la variation kubwa ya umri kati ya wanafunzi unaweza kuwa chanzo cha ushoga mashuleni
 
Hawakuwa na uwezo wa house girl anayelipwa kwa mwezi kwa kipindi kile 30,000/= lakini walinipeleka kusoma English medium kwa mwaka 800,000/=.

Upo sahihi kabisa.

Hapa hatuzunguzii uwezo wa kuweka house girl tunazunguzia kuhusu sera ya elimu inasemaje bosi
 
Ni kweli.mimi mwenyewe nilianza la kwanza Nina miaka mitano .Hilo sio swala la mtu kusema ohhh napendekeza mtoto aanze na miaka sota.Hilo Ni la Mzazi mwenyewe sio serikali

Mleta mada amezungumzia swala la sera za taifa katika elimu, wewe umeleta hoja ya mzazi. Sera ya taifa ni mtoto aanze pri akiwa na miaka saba, wewe uliwahishwa coz hamkuwa na housegirl wa kukuangalia wazazi wakiwa kazini.

Tuongee sera na sio matakwa ya mtu.
 
Back
Top Bottom