Elimu ya Tanzania Vs Elimu ya Kenya

Elimu ya Tanzania Vs Elimu ya Kenya

kwahiyo sisi tukiosoma nje tuamini kwamba ninyi mliosoma bongo ni vilaza? mbona mi wakati mwingine nikifanya nanyi kazi huwa naona mko fresh tu, pamoja na kwamba kuongea kimombo huwa ni msiba, mtu anatamani hadi kulia.
 
Lugha nayo nitatizo watanzania tuko viziri kwenye masomo yasiyo yakujieleza mf hesabu,chemistry ila ukija kwenye kujieleza na kujenga hoja tuko nyuma sana tungechagua lugha moja kama kiswahili iwe kuanzia primary hadi chuo na kama kiingereza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz tunakosea tu kwenye elimu ya msingi... masomo yote kuendeshwa kwa lugha ya kiswahili na mengine yote kwa kiingereza. Wangeongeza vipindi vya kiingereza ili wanafunzi wa elimu ya msingi zaidi ya kujua kiswahili pia kujua kiingereza. Hatuwezi kumfundisha sayansi ya kiswahili mwanafunzi wa msingi halafu sekondari tumfunze kwa kiingereza au historia kiswahili historia kiingereza itakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

Pia wanafunzi wetu wa msingi tuwajengee mfumo wa kujieleza kwa kujiamini. Tuwatengeee wasaa wa midahalo(debates) kati ya wanafunzi wenyewe wakiwa shule za msingi au shule kwa shule. Pia kucheza maigizo ya kwenye vitabu, story books, na simulizi za hapa na pale. Kuwepo na siku ya wazazi na watoto kutoa burudani.

Mi naamini kwa mifumo hii tutawatayarisha vema wanafunzi wetu kujiunga na sekondari.
Naikubali vema syllabus zetu za sekondari zetu na vyuo ni nzuri ila vinakosa kumfanya mwanafunzi kujieleza au kuwa mwajibikaji kwa elimu yake.
 
Elimu yetu ni nzuri ila inatolewa hovyo(kiujanjaujanja) , kwa hyo mwanafunz akili yake mwenyewe.
 
Ukitaka matunda mazuri lazima utunze mti wako wa matunda. Walimu wa Nchi hii wanadharauliwa hata na watoto wadogo kwa jinsi wanavyochukuliwa na jamii. Serikali haijawathamini walimu. Sasa utapata wapi daktari mwenye content ya kutosha,kama anaandaliwa na mtu mwenye stress za maisha.
 
Elimu yetu ni bora sema imekosa practical bado imebase kwenye theories ambapo ulimwengu wa theory ulishapita now ni mda wa practical cha pili wanfunzi wengi wamekuwa waoga hususani kwenye swala la competition

makinikia
 
Unajua Wakenya wanafikia hatua ya kuona watanzania wapo chini kielimu wanapoona statements kama. " watch it..!! "
Wanasema kabisa kwamba Mkulu wenu lugha imemkalia kushoto..!!

Kwa hiyo Wakenya wanataka kutuambia kwamba Mataifa kama: Ujapan, Urusi, Ujerumani, Uchina, Uitaliano nk wapo nyuma kimaendeleo kwa kuwa hawajui kuzungumza lugha ya Kingereza au? Naona kwa wenzetu itawachukuwa karne kujitambua - tatizo lao kubwa linasababishwa na remnant ya colonial mentality.
 
Hawana kitu nmewahi kufanya kaz na Dada mmoja kuto Kenya mbona alikuwa nipga bao hata ngel...nakumbuka kuna cku aliniulza ...ushirika maana yake ni nn kwa kiingereza? Ingawa yeye alikuwa meneja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Helimu yetu hina matatizo makubwa sana. Wizara ya helimu hinabidi hifanyiwe marekebisho makubwa sana.

Bila helimu himala nchi yetu ya fiwanda hahitafikiwa na malengo yetu kama hinchi hayatafikiwa. Nina himani na serikali hitafanya mapinduzi makubwa kwenye helimu.
 
Back
Top Bottom