Elimu ya Tanzania Vs Elimu ya Kenya

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,894
IMENIUMA WAKENYA tena wengine wakiwa wanajulikana kabisa, ni wasomi, madaktari etc, wamewatukana watanzania kuwa ni low rated. Wale madaktari wameitwa low rated doctors from Tanzania. Nikajiuliza hivi ni kwanini wakenya wanatudharau sana watz kielimu, wanatuona kama hatujasoma, kama hatuna akili vile? why?, hivi university of muhimbili na university of nairobi kuna utofauti wowote hasa kwa mtu aliyesoma medicine?

Mbona kuna wakenya rundo wanaacha hospitali zao kule wanakuja kutibiwa hapa bongo? mfano, Aga Khan Dsm, pamoja na kwamba ipo na kenya lakini wakenya wengi tu nimeshuhudia wanacha hospitali zilizoko kenya wanakuja dsm kutibiwa.

Binafsi, nikiwa mkweli, wanachotuzidi wakenya ni lugha tu ya kiingereza, hasa nafurahi wanavyonifundishia watoto wangu. Wanaelewa kuliko wangefundishwa lugha na mbongo. Lakini kwenye contents za elimu zetu, huwa nawaona kama hatuko sawa basi tumewazidi. Ni kwanini wanadharau sana hivi? Ati ukitoka Tanzania wewe una law rated education.....
 
Mkuu tukitaka kubadilika basi ni sharti tukubali KUJISAHIHISHA.... hivyo lazma tukubali elimu yetu ina changamoto ili ndio ssa tutafute suluhu kuendelea kujitia moyo kuwa tumewazidi sidhani kma itatusaidia kusonga mbele.

Content Quality ya elimu ya kenya ni zaidi ya TZ kule mwanafunzi hta wa form 4 ya kule yupo compentent kuliko hata bachelors wa huku TZ.... Nafkiri unakumbuka hata Zain africa challenge wasomi wa vyuo Tz walivyokuwa wanaburuzwa na first years wa kutoka kenya ssa lazma tujue elimu yetu ina shida mahali flani ndio maana unakuta hata professions tunazotoa from vyuoni zinakuwa under performing kuliko wenzetu hta proposal tu mtu anashindwa andika hta mtu mwenye CPA ukimwambia akuandalie business plan anashindwa ssa hapo wasitudharau kweli!!!! mfano mdogo tu hta maofisi ya kikenya ukiingia ni kazi kazi na hta biashara zao ukifika mteja anakuchangamkia sana ila hapa tz nashuhudia mpaka wanasoma magazeti ya uwazi na kupiga umbea tu na hta kwenye pharmacy ukiingia unakuta wanaangalia tv no muda na mteja !!! yaani we r not serious hta kazini but kenyans wapo agressive.....

SULUHISHO: Kuliko tujikite kwenye madawati ni bora ssa tujikite kwenye kuboresha mfumo wa elimu hasa aina ya walimu na ufundishaji pia hta mtaala uboreshwe ili umjengee uwezo mwanafunzi wa kureason na kuwa more of problem solvers zaidi ya employment seekers......
 
Mwanzoni mwa miaka ya sabini, kuja themanini hadi mwishoni mwa miaka ya tisini elimu yetu ya kitanzania ni kweli ilikuwa nzuri tena nzuri kwa kiwango cha kuridhisha.

Elimu yetu tulianza kuiharibu na kuiharibu kabisa miaka ya elfu mbili. Nakumbuka mwaka 2006/7 tulipoanzisha mfuko wa shule za sekondari za kata, kulitokea uhaba mkubwa sana wa waalimu.

Matokea yake kilianzishwa kitu kinaitwa crush~programme, yaani walichukuliwa form six leavers wakawa brushed kwa mwezi mmoja then wakapangiwa vituo vya kazi kufundish. Na izingatiwe kwanga hao for six leavers waliokuwa brushed sio wale waliokuwa wame~perfom vizuri bali ni wale ambao performance zao hazikuwa za kuridhisha so kwa msingi huo huwezi kupata products zenye quality nzuri kwenye elimu.

Na curriculum yetu pia ina matatizo hilo tulikubali na kama hivyo ndivyo mfumo una kasoro basi hata output yake itakuwa na kasoro. Ni dhahiri ukienda kwenye vyuo vyetu vikuu si haba kukuta wanachuo wengi tu ambao hata kufanya presentations kwao ni taabu na hao ndio graduates wetu.

Nimalizie tu kwa kusema moja kati ya sababu kubwa iliyotufanya sisi watanzania kuwa waoga wakati wa mchakato wa kurudi upya kwenye jumuiya ya Africa Mashariki ni mfumo wetu duni wa elimu dhidi ya jirani zetu haswa hao wakenya. We are not competent enough to compete with them in various fields thats why ni rahisi sana kukuta wakenya wameajiriwa Tanzania kuliko kukuta watanzania wameajiriwa Kenya.
 
Niliwahi kufanya kazi na mkenya aliehitimu kidato cha nne shambani kwangu..sikujuta kuwa naye.anafahamu vitu ambavyo hata ma-bwana shamba wetu vinawatoa knock out.kwa kweli tuwe tu wawazi,kunahaja ya kuufumua mfumo wetu wa elimu uwe na uwezo wa kumjenga mtoto awe na uwezo wa kutatua na kuzikabili changamoto zake.
 
Unajua Wakenya wanafikia hatua ya kuona watanzania wapo chini kielimu wanapoona statements kama. " watch it..!! "
Wanasema kabisa kwamba Mkulu wenu lugha imemkalia kushoto..!!
Umeonyesha jinsi ulivyo kitumbua. Mkenya akiona comment kama yako ndo hutudharau zaidi. Elimu kwako ni kuongea lugha ya wazungu vizuri! Hovyo kabisa.
 
Umeonyesha jinsi ulivyo kitumbua. Mkenya akiona comment kama yako ndo hutudharau zaidi. Elimu kwako ni kuongea lugha ya wazungu vizuri! Hovyo kabisa.
Mara nyingine kukubali ukweli sio vibaya ukweli ni kwamba huwezi linganisha Darasa la Nane wa Kenya na Form Four ya hapa Tanzania
 
Tatizo la kwetu ni ile kama una PhD ya Law kama Mwakyembe basi wewe hujui kitu kingine nje ya hicho kitabu huwezi kujielezea huwezi kupambanua mambo na huna General knowledge. Ndio maana Lipumba ni Profesa lakini anafanya mambo ya hovyo
mwakyembe sio kwamba haelewi, walau yeye kasoma udsm na akaenda kusoma pia ujerumani kama sikosei. mwakyembe anaelewa sana ila si unajua tena mkate, ana watoto hapo wengine watakuwa wanasoma ulaya, ukifanya mchezo utakosa hela na hawezi tena kurudi udsm kufundisha na hapohapo bungeni hana uhakika kwasababu kule kyela 2015 alipita kwa ngekewa tu, alikuwa anapigwa chini na hana uhakika 2020 kama atapata ubunge tena. hivyo lazima atafute akili ya kupata pesa huko uwazirini walau asevu za kutumia kwenye kampeni au la akishindwa atumie kama mtaji kuanza maisha mapya 2020.
 
Kwan wakenya curriculum yao kwa watu wanaosoma medicine iko tofauti na ya kwetu?kama ndo hvyo,mbona pale kcmc wamejaa wagonjwa toka kenya,kwa nin hawakwenda kutibiwa kenyatta hospital?
Na kama elimu yetu ni mbovu,hao wakenya,wanyarwanda na waganda waliojazana hapo udsm wamekuja kutafuta nini Tanzania kama sio elimu?
Me binafsi sion kama wakenya wanatudharau,ila sisi watanzania wenyewe ndo huwa tuna tabia ya kujidharau kwa kila jambo,hatuna uzalendo na taifa letu kabisa.
 
madaktari wa kenya, wamewaita madaktari wa tz "low rated doctors" wakimaanisha ni madaktari ambao hawajasoma vizuri kama walivyosoma wao, au madaktari ambao elimu yao (pamoja na kwamba wapo level moja) ni ya chini kwasababu tu walisoma tz hawakusoma kenya. hili ni tusi kubwa mno.
 
Umeonyesha jinsi ulivyo kitumbua. Mkenya akiona comment kama yako ndo hutudharau zaidi. Elimu kwako ni kuongea lugha ya wazungu vizuri! Hovyo kabisa.
mkuu kuna uhusiano wa elimu na lugha..... ssa tunajua wote medium of instruction mashuleni ni english si ndio..... ssa kma medium of instruction huijui utawezaje kutuaminisha kuwa unakielewa kile unachofundishwa?? yaani un degree ya sheria ila hujui shall na will inatofauti gani je tutaaminije unaweza kuchambua miswada ya kisheria yenye vipengele kama " under this section the government shall"???? eti mkuu
 
madaktari wa kenya, wamewaita madaktari wa tz "low rated doctors" wakimaanisha ni madaktari ambao hawajasoma vizuri kama walivyosoma wao, au madaktari ambao elimu yao (pamoja na kwamba wapo level moja) ni ya chini kwasababu tu walisoma tz hawakusoma kenya. hili ni tusi kubwa mno.
eeeh na hyo ni kwa sababu wanajua quality ya elimu yao ni kubwa kuliko yetu so hilo sio tusi zaidi iwe changamoto kwetu kujirekebisha tulipokosea
 
Mkenya au Mrwanda kuja kusoma tz haimaanishi elimu ya tz ni bora zaidi,, kuna ata utaratibu wa kubadilishana wanafunzi(exchange)toka nchi moja kwenda nyingine.
 
Kwan wakenya curriculum yao kwa watu wanaosoma medicine iko tofauti na ya kwetu?kama ndo hvyo,mbona pale kcmc wamejaa wagonjwa toka kenya,kwa nin hawakwenda kutibiwa kenyatta hospital?
Na kama elimu yetu ni mbovu,hao wakenya,wanyarwanda na waganda waliojazana hapo udsm wamekuja kutafuta nini Tanzania kama sio elimu?
Me binafsi sion kama wakenya wanatudharau,ila sisi watanzania wenyewe ndo huwa tuna tabia ya kujidharau kwa kila jambo,hatuna uzalendo na taifa letu kabisa.
mkuu curicullum ya kimakaratasi inakuwa haina maana kma huwezi iapply kwenye field..... ssa hapa TZ unakuta mtu anahyo degree ya medicine ila application yake ni tofauti na mkenya atakavyoiapply..... unakuta wenzetu hta kwenye daladala anasoma novel hivyo anaongeza ujuzi nje ya elimu darasa ssa huyo akiingia field utalinganisha na degree holder wa medicine ya MUHAS???

heshimu sana mtu anayeanza bachelors ya medicine akiwa ametokea form 4 tu tofauti na aliyemaliza form 6 ndo akaingia bachelors afu wakitoka bado hamuwazidi lazma akudharau maana A level ambayo wwe umesoma yye hakusoma ssa iweje usimuache mbali????
 
Hamna Elimu Bongo ........Kenya wako juu tena juzi waliufumua mfumo wao wa elimu na sasa wamekuja na mwingine ambapo mtoto anafundishwa masomo anayoyaweza tu
 
Huwa naangalia mijadala ya wanafunzi katika channel ya The Citizen na KTN katika kipindi cha Great Debaters, nikilinganisha wale wanafunzi na wanafunzi wetu huku bila kupepesa ubora wa elimu yao ni mkubwa zaidi yetu.

Ila hatujachelewa tutumie hili kama changamoto, tuondoe siasa tuangalie tumejikwaa wapi turekebishe
 
Tulikataa Elimu tukakubali viwanda,tangu aondoke Mwl Nyerere aliondoka na kila kitu chake sasa hivi kila awamu inafanya mabadiliko ya elimu ambayo sio endelevu,tumeua elimu ya ufundi,tumeuwa elimu yakujitegemea tumetengeneza elimu ya utegemezi ndio maana tuna bachelor holders wengi tu hawana kazi,japokuwa mahitaji ya Taifa kwa watu wenye elimu ya juu lakini bado idadi kubwa ya wahitimu hawana ajira pia hatuna mfumo mzuri wakujiendeleza inahitaji nguvu ya ziada.mfano Bangladesh kiwango cha juu ya elimu pale ni masters na ni chuo kamasikosei nikimoja tu kinachotoa elimu hii lakini jamaa wako mbali kweli kiuchumi na nikati ya nchi tulizo kuwa tunashabiiana kimaendeleo nyakati hizo,ukiangalia zaidi sera walizo zitengeneza walizitekeleza sisi tunatengeneza sera za kuwaongopea watu majukwaani tu na kuombea pesa kwa wahisani baadae tunagawana kichama,maisha yetu tunaigiza sana sio wakweli hata kidogo japo tunauwezo mkubwa sana kiakili,kiuweledi,kiutendaji na kimsimamo sema utani na mizaha iliopitiliza hasahasa toka kwa watawala
 
Back
Top Bottom