Elimu ya msingi sasa mwisho darasa la sita

Khakha

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
2,982
1,009
Wadau wa JF,
muda mchache uliopita nimesikia ktk kipindi cha magazeti redioni(rfa) kuwa serikali inabadilisha mfumo wa shule za msingi kwa kiwango cha juu cha elimu ya msingi mwisho kuwa ni darasa la sita. Utaratibu huu unaanza effective mwakani. Wenye access na magazeti ya leo amwage data zaidi hapa jamvini..
 
Wameanza kuchakachua kwa mitaala,saiv wanataka kupunguza muda..sidhani kama wanajua wanapoipeleka Tanzania..!!
 
Wameanza kuchakachua kwa mitaala,saiv wanataka kupunguza muda..sidhani kama wanajua wanapoipeleka Tanzania..!!
Ndugu yangu hawa watunga sera wanajali nini?? umeona wapi mtoto wa mbunge au waziri au mkuregenzi nasoma shule za msingi hizi za kawaida?? si wapo academy ndugu au nje ya nchi?? au umeshawaona kwenye shule za kata?? watoto wao wanaandaliwa kuwa ruling class wakati wetu wanaandaliwa kuwa watawaliwa!! Tuchukue hatua mapema!!!
 
Kama ni kweli naona hakuna tatizo. Ila wanapaswa kabla ya kubadili mfumo wazibadili silabasi ziendane na mfumo mpya.
 
hebu nieleze faida za kukaa shele miaka saba. Elimu ya msingi wanaweza kubalance mada zikatosha kwa miaka 6. Nashauri kuwa kwa mwakani ni mapema sana.
 
Kama ni kweli naona hakuna tatizo. Ila wanapaswa kabla ya kubadili mfumo wazibadili silabasi ziendane na mfumo mpya.

Excellent with such deep thoughts, hakuna haja ya hadi kufika std7, no need @ all, look worldwide primary education system, hapa ilikuwa kuwapotezea muda watoto mwaka mzima bure, na ukiangalia vijijini wengine wanaanza na 8 or 9 yrs std 1, unategemea nini? Safiii std 6 inatosha sana, tena wamechelewa sana
 
jambo hili si baya kama siasa itawekwe pembeni,mitaala ikabadilishwa kwa wakati,vitabu kwa wakati na semina elekezi kwa waalimu wote tz
 
Mimi naona ni bora wapunguze jamani lol!! Tunasoma miaka mingi mno jamani....angalia hii;
  1. Elimu ya msingi miaka 7 plus chekechea 1 year=8
  2. O-level miaka 4
  3. Advanced level miaka 2
  4. Elimu ya juu miaka 3 or 4 or 5
Total 17 or 18 or 19
Jamani miaka 17 unasoma tu? Na kibaya zaidi mfano elimu ya o-level na Advanced level hakuna tofauti sana.Nadhani cha msingi ni kuboresha elimu yetu katika mitaala yetu ili kuboresha elimu yetu...
 
Naunga mkono hoja ili watoto wetu wapate muda wa National Service aka JKT miaka 2 kabla ya kufikisha umri wa miaka 21. Ila mitaala iwekwe kwa maslahi ya taifa na si kwa maslahi ya kisiasa. Mfumo wa elimu ubadilishwe kote haukidhi mahitaji yetu, unasaidia lakini bado unaufa mkubwa.
 
ikibadilishwa matokeo yakiwa mabaya nomaaaaaaaaa! mie nadhani serikali ijitazame upya ktk hili. Hii kitu ya kubadili mitaaala ilishafanywa kwa sekondari kelele zikapigwa sana. Tulishindwa sekondari sasa ndo tunataka kuchakaza akili huku huku chini sijui itakuwaje. ikifika hapo wanangu ntawapeleka uganda wote, ujinga gani huu. Tumeshindwa kujifanyia majaribio watu wazima tunaona vitoto vyetu ndo vya kuanza navyo, mweeeeee!

Hivi matatizo ya nchi hii ni kweli yanaanzia na mfumo wa elimu ya msingi au ni suala zima la maadili?
 
yetu macho tu maana hatuna uwezo wa kurekebisha haya mambo ya kijinga jinga!
 
Maamuzi mazuri, lakini kama wanaanza mwakani wamejiandaa vipi na mabadiliko hayo? Au wanafuta kila kitu kinacho husu darasa la saba? N a kama ni hivyo, je hakuna vitu muhimu darasa la saba? Au wanafuta mwaka wa kwanza wa shule? maswali mengi inabidi watueleze kwa undani.
 
Wadau wa JF,
muda mchache uliopita nimesikia ktk kipindi cha magazeti redioni(rfa) kuwa serikali inabadilisha mfumo wa shule za msingi kwa kiwango cha juu cha elimu ya msingi mwisho kuwa ni darasa la sita. Utaratibu huu unaanza effective mwakani. Wenye access na magazeti ya leo amwage data zaidi hapa jamvini..

Basi kama ndo hivyo elimu ya msingi kwisha habari yake. La saba lenyewe hesabu ni kuchagua (multiple choice)!!!!!
 
Still ni makida makida. Maana sidhani kama wana vitu vinavyotakiwa in place!
A proper guding sylabaus, Vitabu vya kiada. Then Baada ya Darasa la Sita ina maana wote wataendelea na Darasa la 8 MPAKA FORM IV ama anayefeli anakaa nyumbani? Je kama mtoto wa miaka 11 anakaa nyumbani what arre we creating? Na still kama watafika Form IV atakuwa hajatimiza miaka 18 je hilo kundi linakwenda wapi endapo hawataendelea na vyuo ama high school. Huo umekuwa ni uozo wa elimu na mikakati ya nchi hii (Kuna kundi linasahauliwa sasa hivi darasa la saba bado ni watoto miaka 14 wasipoendelea hakuna kinachofanyika, afadhali wanaomaliza form iv ni watu wazima. ) Sasa kwa mtaala mpya ndo kundi litakuwa kubwa wanaomaliza darasa la 8 siijui iv watawapeleka wapi? Hpao serikali ingepanga mkakati hap[o ningewaunga mkono. Otherwise ni kuvurugavuruga tu!!!
 
Wadau wa JF,
muda mchache uliopita nimesikia ktk kipindi cha magazeti redioni(rfa) kuwa serikali inabadilisha mfumo wa shule za msingi kwa kiwango cha juu cha elimu ya msingi mwisho kuwa ni darasa la sita. Utaratibu huu unaanza effective mwakani. Wenye access na magazeti ya leo amwage data zaidi hapa jamvini..

Wasiwasi wangu tu hii ikipita, mwakani wataleta muswada kuwa elimu ya msingi mwisho darasa la nne
 
Back
Top Bottom