kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,332
- 12,647
Kama wewe ulivyokuwa mdogo kula kulala tu nyumbani ulishindwa kusoma na kufaulu mtihani je, ukubwani ukiwa na majukumu mengi akili zilitoka wapi? Kama kweli akili bado unazo kwanini usiende kurudia kusoma yale masomo uliyoshindwa utotoni kutokana na sababu mbalimbali? Badala yake unataka utafutiwe uchochoro mpya hafifu wa kupita hadi ufike PhD na kupata uprofessor. Kama akili zipo na fursa ya kurudi darasani kwenda kusoma tena Chemistry, Physics na Maths ipo kwanini hamtaki kuitumia? Prof. Ndalichako yuko sahihi kwa 100% hata kama waliopita vichochoro hivyo wanamjia juu. Ndiyo maana tuna maprofessor nchini ambao wanadhani kufanya tafiti zisizo na matokeo kwenye jamii inatosha na ni usomi.
Wasomi walioungaunga kwenye elimu zao hawapendi kuwaona wasomi waliosoma moja kwa moja kwa kuwasingizia eti hawana uzoefu kazini, wasomi wa kuungaunga wengi wanatokea makazini na wakimaliza wanarudi makazini na kujichukulia nafasi kubwa kwenye Wizara, vitengo, na mashirika. Wakishazipata nafasi hizo watawatafuata kuwaajiri na kuwapa nafasi wenzao walioungaunga pia na kutengeneza ukuta dhidi ya wasomi waliosoma moja kwa moja kutoka form 6 hadi vyuo vikuu. Vijana wenye vipaji kama akina Makonda, January Makamba, Bashe, Mbowe, Mbatia, Zitto, n.k wanakosa fursa kwa sababu ya wazee walioungaunga elimu wametengeneza wigo wao. Hali hiyo ninaiona sana kwa wauguzi, wafamasia, madaktari, walimu na hata wahandisi. Matokeo yake ubunifu makazini unakuwa mdogo sana, watahakikisha kuwa wanazima ndoto, mawazo na kazi angavu za wasomi wenye akili za moja kwa moja kutoka utotoni zisichomoze kwenye jamii. Ndio maana ni rahisi kumuona Prof. asiyekuwa na msimamo na mchumia Tumbo, Prof. wa aina hii yuko tayari kuipotosha jamii akitetea maslahi yake au ya kundi lake na kuyapiga teke maslahi ya umma na taifa. Mzee Mkapa alikuwa akiwaita Maprofessor uchwara kama vile akina Prof. Nanihino anayemgunia Prof. Ndalichako sasa hivi. Ukiangalia vyuo vikuu vinatoa wanafunzi wabovu sana na baadhi ya Maprof wao wanaongea siasa zaidi kuliko taaluma.
Kama tunataka elimu yetu ikue sio kila mtu lazima afike chuo kikuu, kazi ziko nyingi sana, fanyakazi iliyo sawa na uwezo wako wa kufikiri. Kama unadhani akili zako bado zinachemka acha kutafuta foundation courses nenda kachanganye madawa upate credit za kusonga chuo kikuu. Kuungaunga huku ndiko kulikoshusha kiwango chetu cha elimu nchini ukilinganisha na nchi za jirani. kama Wewe hukufaulu form IV unawezaje kuwa na hasira na mwanafunzi asiyefanya vizuri darasani? hebu tuseme ukweli. Wewe una magari, nyumba na mshahara wakati mwalimu wa foundation kozi ana njaa, anatembea kwa miguu na kuishi nyumba ya kupanga utashindwa kufaulu mtihani wake wa hiyo foundation kozi? Nina ushahidi wa mwanafunzi wa mature entry kwenye chuo kimoja amemlipa fedha mwalimu mwalimu wa somo ili amuandikie research paper yake.
Ndalichako oyeee!!!