Elimu ya kuungaunga ilitupatia wasomi hafifu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Kama wewe ulivyokuwa mdogo kula kulala tu nyumbani ulishindwa kusoma na kufaulu mtihani je, ukubwani ukiwa na majukumu mengi akili zilitoka wapi? Kama kweli akili bado unazo kwanini usiende kurudia kusoma yale masomo uliyoshindwa utotoni kutokana na sababu mbalimbali? Badala yake unataka utafutiwe uchochoro mpya hafifu wa kupita hadi ufike PhD na kupata uprofessor. Kama akili zipo na fursa ya kurudi darasani kwenda kusoma tena Chemistry, Physics na Maths ipo kwanini hamtaki kuitumia? Prof. Ndalichako yuko sahihi kwa 100% hata kama waliopita vichochoro hivyo wanamjia juu. Ndiyo maana tuna maprofessor nchini ambao wanadhani kufanya tafiti zisizo na matokeo kwenye jamii inatosha na ni usomi.

Wasomi walioungaunga kwenye elimu zao hawapendi kuwaona wasomi waliosoma moja kwa moja kwa kuwasingizia eti hawana uzoefu kazini, wasomi wa kuungaunga wengi wanatokea makazini na wakimaliza wanarudi makazini na kujichukulia nafasi kubwa kwenye Wizara, vitengo, na mashirika. Wakishazipata nafasi hizo watawatafuata kuwaajiri na kuwapa nafasi wenzao walioungaunga pia na kutengeneza ukuta dhidi ya wasomi waliosoma moja kwa moja kutoka form 6 hadi vyuo vikuu. Vijana wenye vipaji kama akina Makonda, January Makamba, Bashe, Mbowe, Mbatia, Zitto, n.k wanakosa fursa kwa sababu ya wazee walioungaunga elimu wametengeneza wigo wao. Hali hiyo ninaiona sana kwa wauguzi, wafamasia, madaktari, walimu na hata wahandisi. Matokeo yake ubunifu makazini unakuwa mdogo sana, watahakikisha kuwa wanazima ndoto, mawazo na kazi angavu za wasomi wenye akili za moja kwa moja kutoka utotoni zisichomoze kwenye jamii. Ndio maana ni rahisi kumuona Prof. asiyekuwa na msimamo na mchumia Tumbo, Prof. wa aina hii yuko tayari kuipotosha jamii akitetea maslahi yake au ya kundi lake na kuyapiga teke maslahi ya umma na taifa. Mzee Mkapa alikuwa akiwaita Maprofessor uchwara kama vile akina Prof. Nanihino anayemgunia Prof. Ndalichako sasa hivi. Ukiangalia vyuo vikuu vinatoa wanafunzi wabovu sana na baadhi ya Maprof wao wanaongea siasa zaidi kuliko taaluma.

Kama tunataka elimu yetu ikue sio kila mtu lazima afike chuo kikuu, kazi ziko nyingi sana, fanyakazi iliyo sawa na uwezo wako wa kufikiri. Kama unadhani akili zako bado zinachemka acha kutafuta foundation courses nenda kachanganye madawa upate credit za kusonga chuo kikuu. Kuungaunga huku ndiko kulikoshusha kiwango chetu cha elimu nchini ukilinganisha na nchi za jirani. kama Wewe hukufaulu form IV unawezaje kuwa na hasira na mwanafunzi asiyefanya vizuri darasani? hebu tuseme ukweli. Wewe una magari, nyumba na mshahara wakati mwalimu wa foundation kozi ana njaa, anatembea kwa miguu na kuishi nyumba ya kupanga utashindwa kufaulu mtihani wake wa hiyo foundation kozi? Nina ushahidi wa mwanafunzi wa mature entry kwenye chuo kimoja amemlipa fedha mwalimu mwalimu wa somo ili amuandikie research paper yake.

Ndalichako oyeee!!!
 
Jiulizeni kwa mtu aliyefeli bila mizengwe anaweza kufaulu kweli chuo kikuu bila kuwa disco tafiti zinaonyesha wapo waliongia chuo kikuu na madaraja mazuri lakini wakadisco na kuwaacha hao waliounga
 
Pale MUHAS Clinical Officer (CO) au tumuite Daktari mwenye diploma hutakiwa kuwa na principal pass mbili za ACSEE ndiyo adahiliwe MD ilhali wanajua sifa ya kusoma CO ni ufaulu wa CSEE.

Na hii ipo miaka mingi tu na si MUHAS tu hata UDOM,KCMCo,UDSM kote wanataka CO awe na pass za A level kama sifa ya ziada kusoma MD.

Sijui kama hao wanaopiga kelele wanalijua hili.
 
Jiulizeni kwa mtu aliyefeli bila mizengwe anaweza kufaulu kweli chuo kikuu bila kuwa disco tafiti zinaonyesha wapo waliongia chuo kikuu na madaraja mazuri lakini wakadisco na kuwaacha hao waliounga
inawezekana hata mtoto wa chekechea akaweza kujibu maswali ya TRUE and FALSE ya chuo kikuu na akafaulu kuliko mwanafunzi wa chuo kikuu mwenyewe, je, utasema mtoto ana akili kuliko yule mtu mzima? mtu fresh from school aliyedisco na aliyeungaunga akabakia vyuoni kuna sababu nyingi sana zinazoweza kuelezea hili, mojawako ni rushwa, kuiba mtihani, kuonyeshwa majibu, kuugua, starehe na ulevi, shida kama njaa, mimba, hofu, uchawi, n.k. Lakini hilo litakuwa ni kundi ndogo sana lisiloweza kufuta ubaya wa elimu ya kuungaunga. Mtu aliyeungaunga kuna stage ameiruka ambayo ni muhimu sana kwenye kufikiri na kutenda mambo ukubwani. Unajua akili huwa inajengeka kwenye kipindi cha utoto kutoka shule za awali, ile miaka 2 ya form V na VI ni muhimu sana kwenye ubongo wa mtoto kama msomi utaikosa lazima hitilafu itajitokeza tu kwenye maisha yako ya elimu zinazofuata na hata kazini.
 
Chuo kikuu hakuna true na false ni presentation na essay question na ikiwepo weight yake haizidi 10% ya total na baadhi ya vyuo unapigwa penalty kwa guessing kama umeandika true wakati false unapoteza 2 marks kwa kudanganya nakuhakikishi kuna vyuo utamuhonga nini mhadhili wakati ana kila kitu
 
Hati elimu ya kuunga unga hata sijui watu wanaongelea nini. Kuna watu wanaamini kuna njia moja tu ya kwenda Mwanza na ukipita njia yeyote nyingine wewe umeunga unga. Primary school unaunga secondary school unaunga high school unaunga chuo kikuu-hii siyo kuunga unga? Badala ya high school unaweza kwenda "college" ukatokea chuo kikuu. Zote mbili unaunga unga mpaka unafika uendako. Naona watanzania hamtaki tuwe na open university-basi tuifunge au tuibadilishe kwani bila foundation courses unafuta u-openess/uhuria wa chuo-kinakuwa sio chuo huria.

"Open universities are universities that are open to people without formal academic qualifications. Open universities offer distance education using specific didactics and media. The goal of open universities is to offer everyone equal opportunities to develop their competences, to raise their level of education and to receive retraining. On the other hand, it is also a way of attracting potential students that at one point, would like to enrol and pursue a degree" (What Are Open Universities? - DistanceLearningPortal.com). Wakati dunia inafungua elimu sisi tunafunga.
 
Hata Ulaya na Marekani wameifunga elimu yao, viko vyuo ambovyo wahitimu wake wanapewa heshima sana kuliko wa vyuo vingine kutokana na akili za wanafunzi na ubora wa elimu inayotolewa kwenye vyuo hivyo. Sisi hapa kwetu wahitimu wote kutoka vyuo vyote wanapata hadhi sawa kwenye jamii na makazini bila kubaguliwa. Hivyo kwa sababu hii ni bora ukadhibiti ubora wa wanafunzi wote na ubora wa vyuo vyote mapema ili upate wahitimu wenye ubora sawa na hadhi sawa na mishahara sawa. Kwanini upewe foundation course wakati fursa ya kusoma masomo uliyoshindwa huko nyuma ipo, unaogopa nini? maana yake unafahamu kuwa hautaweza kufaulu badala yake unataka upewe kitu hafifu lakini hupendi kupewa mshahara hafifu na kazi hafifu utakapohitimu chuo kikuu. Hii haiingii akilini, wote tunakwenda posta lakini aliyekwenda kwa baiskeli na aliyekwenda kwa taxi lazima wataonekana tutakapokutana huko posta, unachosema wewe unataka wasitofautiane ilihali unawaona kabisa mwingine amejaa mavumbi na majasho na mwingine yuko smart. Mi nadhani huyu JPM ana akili nyingi sana pamoja na Mh. Ndalichako, hizi PhD zao zinawasaidia sana kurusha mawe kwenye vichaka ambavyo watakurupusha viumbe vingi sana vibaya na vizuri. Nadhani hakuna ubaya wa kulipanga upya taifa ili lirudishe vidole kwenye mstari wa kukimbilia. Wanaolalamika hawana hoja kabisa, yaani huko ni sawa na kuamua kumuacha kumchukulia hatua kibaka uliyemgundua leo kuwa ndiye aliyekuibia TV yako sebuleni mwaka jana.
 
Hata Ulaya na Marekani wameifunga elimu yao, viko vyuo ambovyo wahitimu wake wanapewa heshima sana kuliko wa vyuo vingine kutokana na akili za wanafunzi na ubora wa elimu inayotolewa kwenye vyuo hivyo. Sisi hapa kwetu wahitimu wote kutoka vyuo vyote wanapata hadhi sawa kwenye jamii na makazini bila kubaguliwa. Hivyo kwa sababu hii ni bora ukadhibiti ubora wa wanafunzi wote na ubora wa vyuo vyote mapema ili upate wahitimu wenye ubora sawa na hadhi sawa na mishahara sawa. Kwanini upewe foundation course wakati fursa ya kusoma masomo uliyoshindwa huko nyuma ipo, unaogopa nini? maana yake unafahamu kuwa hautaweza kufaulu badala yake unataka upewe kitu hafifu lakini hupendi kupewa mshahara hafifu utakapohitimu. Hii haiingii akilini, wote tunakwenda posta lakini aliyekwenda kwa baiskeli na aliyekwenda kwa taxi lazima wataonekana tutakapokutana huko posta, unachosema wewe unataka wasitofautiane ilihali unawaona kabisa mwingine amejaa mavumbi na majasho na mwingine yuko smart. Mi nadhani huyu JPM ana akili nyingi sana pamoja na Mh. Ndalichako, hizi PhD zao zinawasaidia sana kurusha mawe kwenye vichaka ambavyo watakurusha viumbe vingi sana vibaya na vizuri. Nadhani hakuna ubaya wa kulipanga upya taifa ili lirudishe vidole kwenye mstari. Wanaolalamika hawana hoja kabisa, yaani huko ni sawa na kuamua kumuacha kumchukulia hatua kibaka uliyemgundua leo aliyekuibia TV yako sebuleni siku nyingi zilizopita.

Mkuu ukisoma mchango wangu utaona mimi nimejikita kwenye issue ya foundation courses za Open University na nadharia ya Chuo Huria. Soingelei kabisa hizo foundation courses za vyuo vingine. Tamko la waziri linakinzana na nadharia ya ya chuo huria. Ukisha funga uhuria wa chuo huwezi kukiita chuo huria. Kwa hiyo kama msimamo wa serikali ndio huo hakuna maana ya kukiita chuo kile OPEN UNiversity kwani hakitakuwa na viashiria cha open university.

Issue ya pili ni hii dhana ya kuwa Foundation course zinarahisishia watu kazi-kwa open university foundation course inatakiwa imtayarishe mtu kuendelea na masomo ya chuo kikuu. Na anapoanza masomo yake ya shahada chuo kitawadhibiti wanafunzi wake walioingia kwa foundation au kwa njia nyingine sawa sawa ili kuwa na viwango bora. Wanapofaulu na kutunukiwa shahada kunakuwa hakuna tofauti kati ya aliepitia Foundation au aliyepitia F6. Degree yao inakuwa na hadhi moja. Sasa labda uniambie foundation courses zetu (OPEN UNIVERSITY) ni nyepesi sana na wanapoingia kwenye shahada hakuna udhibiti-ndio nitakuelewa. Lakini hapo dawa yake sio kufuta foundation courses bali ni kuongeza ubora wake na kuzidhibiti. OPEN UNVERSITY inatakiwa iwe na milango wazi ya kuingia-huangalii kama amefeli form 4 au 6, unamdahili anafanya FOUNDATION anachujwa akishindwa, akiweza ana anza shahada pamoja na walio pitia ngazi ya F6 nakufaulu, na waliopitia diploma na kuwa na vigezo au waliopitia RPL. Mchakato wa degree ni sawa kwa wote. Narudia tena mimi nazungumzia OPEN UNIVERSITY tu.

Kwangu mimi wanaolalamika inategemea wanalalamimkia nini wanaweza kuwa na hoja. Bahati mbaya waziri ametoa matamko mengi na mengine yamekua yanabadilika na wanao lalamika wengi hawazungumzii kwa undani.
 
Huria maana yake non-formal, kwa maana kuwa hakuna kengele, meza, viboko, madarasa na mwalimu mbele ya wanafunzi. Uhuria huu sio lazima mtu apate degree au masters or PhD. Kwa neno huria maana yake unaweza kwenda kujifunza muziki, kuimba, kupiga gitaa, au kuboresha ujuzi wako kwenye sehemu/kipande tu kwenye taaluma yako uliyonayo kama ya ualimu, uhasibu, nk unaweza kwenda chuo huria na ku audit tu kipengele hicho na kupata certificate of attendance tu na kuondoka zako baada ya kupata hizo skills ambazo ulikuwa huna kwenye taaluma/kazi yako ya awali. Lakini uhuria na uholela unaosema wewe utakoma tu kama unataka kusoma na upewe formal cheti cha kitaaluma kwenye ngazi fulani kama certificate, diploma, degree kinachotambulika na kutumika kitaifa na kimataifa katika kufanya na kutoa maamuzi, hapo ni lazima kuwe na entry/pre-requisit qualifications za kusoma kozi hiyo ambazo ni za kitaifa na kimataifa, maana kilo ya pamba na kilo ya mawe zinatakiwa zote ziwe na uzito sawa kwenye mizani ingawa furushi la pamba litaonekana kubwa. UHURIA UTABAKIA TU KWENYE MODE OF DELIVERY OF THE KOZI sio kwenye entry qualifications kwasababu unatafuta fitting kama ya lock and key. Kama kufuli na ufunguo havitaoana kufuli halitafunga na kufunguka, foundation courses ni jitihada za kuchonga funguo bandia kungulia makufuli uliyokosa funguo zake. Chuo kikuu tunakwenda kuendeleza kile ulichokileta kwenye mafunzo yaliyotangulia (cognitive structure). ndio maana watataaluma wakabuni kitu kinachoitwa combinations, daktari atahitaji combination ya PCB (lock) ili aweze kupewa masomo ya udaktari (key), sasa kama hukufaulu PCB vizuri itakuwa vipi hapo, kwasababu ni OPEN University basi uruhusiwe kusoma udaktari? wewe unasema hata mwenye HGL ruksa kusoma udaktari si ndiyo? Ndani ya PCB kuna elimu nyingi sana muhimu kuwa nazo kwaajili ya masomo ya sayansi kama hukuyafaulu lazima utakuwa mbabaishaji tu sehemu fulani mbele ya safari.
 
Huria maana yake non-formal, kwa maana kuwa hakuna kengele, meza, viboko, madarasa na mwalimu mbele ya wanafunzi. Uhuria huu sio lazima mtu apate degree au masters or PhD. Kwa neno huria maana yake unaweza kwenda kujifunza muziki, kuimba, kupiga gitaa, au kuboresha ujuzi wako kwenye sehemu/kipande tu kwenye taaluma yako uliyonayo kama ya ualimu, uhasibu, nk unaweza kwenda chuo huria na ku audit tu kipengele hicho na kupata certificate of attendance tu na kuondoka zako baada ya kupata hizo skills ambazo ulikuwa huna kwenye taaluma/kazi yako ya awali. Lakini uhuria na uholela unaosema wewe utakoma tu kama unataka kusoma na upewe formal cheti cha kitaaluma kwenye ngazi fulani kama certificate, diploma, degree kinachotambulika na kutumika kitaifa na kimataifa katika kufanya na kutoa maamuzi, hapo ni lazima kuwe na entry/pre-requisit qualifications za kusoma kozi hiyo ambazo ni za kitaifa na kimataifa, maana kilo pamba na ya mawe zinatakiwa zote ziwe na uzito sawa kwenye mizani ingawa furushi la pamba litaonekana kubwa. UHURIA UTABAKIA TU KWENYE MODE OF DELIVERY OF THE KOZI sio kwenye entry qualifications.
OPEN
Tembelea vyuo vikuu huria kama The OPEN UNIVERSITY UK na vya mataifa mengine ndio utaona ya kuwa huria siyo mode of delivery bali ni OPEN ENTRY. Na kwa sababu hiyo hata OUT yetu ya sasa bila kuondoa Foundation courses bado ina vigezo vya kudahiliwa ukilinganisha na THE OU UK. Ukiondoa uhuria wa kudahiliwa basi huna OPEN UNIVERSITY una university tofauti hata kama zote zinatumia mifumo ya distance education etc.
University
Umeandika-"Uhuria sio lazima mtu apate degree au masters or PhD"(degree). Sawa, lakini kumbuka university (kitu ambacho tunaongelea hapa) hutoa elimu ya juu na itakuwa university ya ajabu kama haitoi bachelors, masters na mwishowe doctorates. Hizo qualification nyingine wanaweza kutoa lakini kama chuo kikuu bila degree hakiwi chuo kikuu (Angalia definitions za univerity hii kitu imeandikwa kwa uwazi kabisa).
 
OPEN entry!!, haha. Yaani hata mwenye combination ya HGL aruhusiwe kusoma engineering science kwakuwa ni open entry!!!! wewe umekula maharagwe ya wapi? Foundation courses ni sawa na jitihada za kuchonga funguo bandia (master key) ili kufungulia makufuli usiyokuwa na funguo zake halisi.
 
Kama anaweza goma la engineering anaruhusiwa ingawa kimantiki sijui ni wangapi watajaribu. Naona umegoma kwenda website ya OPEN UNIVERSITY UK-jaribu unaongeza upeo. Angalia Indira Gandhi National OPEN University ya India wanasema "The mandate of the University is to: Provide access to higher education to all segments of the society;........." Sisi ndio tunafunga. Waholanzi nao wana OPEN UNIVERSITY sababu ya kuianzisha ni "The Dutch government's purpose in founding the Open Universiteit Nederland was to make higher education accessible to anyone with the necessary aptitudes and interests, regardless of formal qualifications". Sintakuuliza kuhusu maharagwe.
 
duh.... all segments of the society (unlimited) can join the Faculty of Geology as they wish, ridiculous!!!
 
Back
Top Bottom