SoC01 Elimu ya jumla kuhusu chanjo (yoyote inayotolewa hapa nchini)

Stories of Change - 2021 Competition

msugupendigwite

Senior Member
Dec 20, 2012
137
26
ELIMU KUHUSU CHANJO KWA UJUMLA

Habari za muda huu wana JF hususan wa jukwaa hili la “stories of Change”, Karibuni tushirikishane elimu kuhusu Chanjo zote zinazotolewa hapa nchini, iwe umewahi kuchanjwa au la halafu tujadiliane kwa pamoja kwenye uzi huu……..

CHANJO NI NINI??

Chanjo ni dawa ya kibaolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa Fulani. Chanjo hutengenezwa au kuzalishwa kutokana na kimelea (causative agent) kinachosababisha ugonjwa. Mfano wa chanjo zinazotolewa hapa kwetu ni chanjo za Kifua kikuu( BCG), Polio (OPV), Surua(Measles), Homa ya ini (Hepatitis B), Dondakoo, Kuharisha, Vichomi na sasa kuna hii ya UVIKO 19

AINA/MAKUNDI YA CHANJO.

1. Live Attenuated Vaccines


Hizi ni chanjo zinazotengenezwa kutoka kweny kimelea ‘hai’ cha ugonjwa lakini kimepunguzwa nguvu ya kusababisha ugonjwa husika, chanjo hii ikiingia mwilin kimelea kinajizalisha “replication” kwa kiwango ambacho kitaweza kupambana na kimelea hai chenye nguvu endapo kitaingia mwilini. Mfano wa chanjo hizi ni Polio, Surua na Kifua kikuu

2. Killed Bacteria/Toxins Vaccines

Hizi ni chanjo zinazotengenezwa kutokana na mdudu/kimelea kinachosababisha ugonjwa husika lakini kilichokufa . Kimelea hiki hakiwezi kujizalisha “replication” kikiingia mwilini hivyo chanjo yake inatakiwa kutolewa mara kwa mara ili kufikia dozi tarajiwa ili kujenga kinga. Mfano wa chanjo hizi ni Tetenasi na DpT (ile inachomwa mapajani kwa watoto wachanga)

3. Recombinant/Conjugate Vaccines

Hizi ni chanjo zinazotengenezwa kutokana na muunganiko ‘combination’ wa vinasaba ‘genes’ vya kimelea kinachosababisha ugonjwa husika. Chanjo hizi zikiingia mwilini hazijizalishi ‘replication’ hivyo nazo zinahitaji kutolewa zaidi ya mara moja ili ziweze kufikia dozi husika kujenga kinga. Mfano wa chanjo hizi ni homa ya ini ‘hepatitis B, Dondakoo,na Vichomi ‘Pneumococcal vaccine’.

NJIA “ROUTES” ZA UTOAJI CHANJO

Chanjo zilizo nyingi hutolewa kwa njia ya Mdomo ambapo ‘mteja’ hudondoshewa matone mdomon kutokana na dozi inayotakiwa, mfano wa chanjo hizi ni chanjo ya Polio, Kuzuia kuharisha kwa watoto “Rotavirus”. Pia chanjo nyingine (hutolewa kwa njia ya sindano kwenye msuli “intramuscular” yaweza kuwa misuli ya mapajani, begani au makalio kulingana na umri wa mteja. Mfano wa chanjo hizi ni Tetanus, Homa ya Ini, Dondakoo na ya hivi karibuni ya UVIKO 19.

UNAPOCHOMWA AU KUPEWA CHANJO NDANI YA MWILI INAENDA WAPI NA INAFANYA NINI?? AIM, DESTINATION & TARGET OF VACCINATION

Chanjo inapoingia mwilini shabaha ‘target’ au destination yake ni kwenye sli hai nyeupe za damu ambazo ndio ‘askari na walinzi’ wa mwili. Ndani ya seli hai nyeupe chanjo huingia katika Seli kuu 2; T-Lymphocytes na B- Lymphocytes hapo chanjo inatengeneza kinga ‘antibodies’ zenye kumbukumbu za kimelea cha ugonjwa husika hivyo baadae kimelea cha ugonjwa huo kikiingia tayari mwili unakua na kumbukumbu yake ‘askari wa mwili’ wanakishambulia.

Kutokana na teknolojia kukua duniani sasa kuna chanjo ambazo zina ‘target’ kwenye DNA moja kwa moja……, “ Chanjo za aina hii zikiingia kwenye DNA huchochea uzalishaji mwingi wa T na B-Lymphocytes zenye vinasaba vya ugonjwa husika hvyo inakua na kinga ya muda mrefu na ni rahisi kupambana na kimelea cha ugonjwa husika. Mfano wa chanjo zinazokwenda kwenye DNA moja kwa moja ni chanjo ya Homa ya Ini, Mafua makali “influenza Virus” na baadhi ya Chanjo za UVIKO 19 (tutazijadili huko mbeleni).

NI WAKATI GANI HUTAKIWI KUPEWA CHANJO IWAYO YOYOTE ILE? ‘CONTRAINDICATIONS’


Yapo mambo ambayo endapo mgonjwa au mteja anayo hatakiwi kupewa chanjo ama atapewa chanjo ila kwa tahadhari, pia mambo haya si ya jumla bali yatategemea chanjo husika. Kwa kimombo yamepewa majina Mawili PRECAUTIONS & CONTRAINDICATIONS TO VACCINATION. Mambo haya ni pamoja na Mzio ‘allergy’, kuumwa ugonjwa wowote kunakoambatana na/bila homa, Ujauzito, Upungufu wa kinga, Historia ya magonjwa ya ‘degedege’, majeraha katika eneo linalotakiwa kupitishia chanjo, Muda/umri wa kupewa chanjo husika kupita, kuumwa au kuwa na maambukizi ya ugonjwa husika( ugonjwa unaotakiwa kuchanjwa) n.k

MAUDHI MADOGO YANAYOWEZA KUTOKEA UKICHANJWA. "SIDE EFFECTS"
Wataalamu wa afya hupenda kutumia neno 'maudhi' na sio 'madhara' na hutoa tahadhari juu ya hili na jinsi ya kukabiliana nalo endapo litatokea (sio lazima litokee). Mfano wa maudhi haya ni pamoja na mzio au allergy, Homa, Mwili kuchoka, kuumwa misuli, Uvimbe na maumivu sehemu chanjo ilipochomwa, kichefuchefu na kutapika...... (kwa uchache).

Kwa leo niishie hapa tukijaaliwa siku zijazo tutashirikishana na kuzichambua chanjo za UVIKO 19 ili tuwekane kwani yanazungumzwa mengi.

Chanjo zinazotolewa kwa watoto

View attachment 1940379

REJEA:


MOHSW (2007). Immunization Safety and Data Quality Self Assessment. Dar es Salaam, Tanzania: Ministry of Health and Social Welfare
 
Back
Top Bottom